Mahakama ni mhimili uliojificha zaidi? Majaji wa Tanzania wanaweza kutoa maoni yao binafsi?

Yoda

JF-Expert Member
Jul 22, 2018
37,548
46,090
Serikali yetu inaundwa na mihimili mitatu ambayo ni Dola (Executive), Bunge na Mahakama.

Viongozi wakuu na watumishi wanaosimamia mihimili miwili ya Dola na Bunge huwa tunawasikia kila siku kupitia vyombo vya habari katika matukio mengi rasmi ya kiserikali na yasiyo rasmi wakitoa matamko, mawazo, ufafanuzi, wakihoji n.k kuhusu mambo mbalimbali yanayoendelea nchini.

Hii ni kuanzia wabunge bungeni,viongozi wa serikali na wabunge kupitia vipindi vya redio, TV, Twitter, Instagram, magazeti. Kupitia matukio ya kijamii kama sherehe, ibada, misiba n.k

Marais wetu kuanzia Kikwete mpaka Samia wamekuwa wana accounts za Twitter ambazo huhabarisha mambo mbalimbali, mawaziri na wabunge wengi wanazo accounts za Twitter na Instagram. Hata Spika wa bunge angetaka kuwa na account Twitter anagekuwa nayo muda wowote au huenda anatumia account ya bunge.

Kwa upande wa mahakama hali haiko hivyo, tofauti na jaji mkuu ambaye mara nyingi huongea zaidi katika matukio ya ikulu na siku chache zinazohusu maadhimisho ya kisheria ni nadra kusikia jaji mwingine yoyote akitoa neno lolote kuhusu hali ya nchi au mwenendo wa hali ya kisheria/mahakama katika nchi.

Kuna matukio mengi yanayohusu mambo ya Kisheria lakini huwezi kuwasikia wameshiriki au wametoa neno huko.

Hivi ndivyo wanatakiwa kuenenda kwa mujibu wa kazi yao au ni utamaduni tu uliojengeka kwamba hawapaswi kushiriki katika kutoa maoni juu ya nchi yao?

Kama wanaruhusiwa kuzungumzia yanayoendela katika nchi yao basi mahafali ya vyuo katika vitivo vya sheria na Taasisi mbalimbali za kisheria ingekuwa ni majukwa mazuri kwao kuongelea uwanja mpana wa sheria na haki nchini kwa weledi.

Pia makala katika magazeti ni jukwa lingine ambalo majaji katika nchi zilizoendelea hupenda kutumia kutoa maoni yao kuhusu mambo mbalimbali.

Nimetoa maoni yangu nikiwa sijui taratibu zinazuongoza mhimili wa mahakama katika kufanya "interactions" na umma. Tuliambiwa Dola ni mhimili uliojichimbia chini zaidi, huenda mahakama ni mhimili uliojificha zaidi.
 
Back
Top Bottom