Mahakama nchini Uganda yatoa hati ya kumkamata Mwandishi wa Vitabu

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,500
9,279
Mahakama ya Uganda imetoa hati ya kumkamata mwandishi wa vitabu aliyetoroka nchi baada ya kushtakiwa kwa makosa ya kumtusi Rais Yoweri Museveni na mwanawe, Jenerali Muhoozi Kainerugaba, wakili wake alisema Jumatano.

Kakwenza Rukirabashaija alikamatwa muda mfupi baada ya siku kuu ya Krismasi na kushtakiwa kwa mawasiliano ya kukera, kesi ambayo ilizusha wasiwasi katika jumuia ya kimataifa, huku Umoja wa Ulaya na Marekani wakiomba aachiliwe huru.

Kakwenza alisema aliteswa wakati akizuiliwa kwa muda kwa kipindi cha mwezi mmoja na alitoroka nchi mwezi uliopita kutafuta matibabu nje ya nchi kutokana na majeraha aliyokuwa nayo.

Lakini Jumatano, waendesha mashtaka waliiomba mahakama ya mjini Kampala kutoa hati ya kumkamata mwandishi huyo wa riwaya za kukejeli baada ya kushindwa kufika mahakamani kusikiliza kesi inayomkabili.

Wakili wake Samuel Wanda ameliambia shirika la habari la AFP kwamba “Jaji aliamuru akamatwe na afikishwe Mahakamani.”

Haikubainika mara moja ikiwa hati hiyo itajumuisha ombi la kurejeshwa nchini kutoka Ujerumani ambako Kakwenza alisema aliomba hifadhi.

Mashtaka dhidi yake yanahusu maoni yasiyopendeza kwenye ukurasa wake wa Twitter kumuhusu Museveni ambaye ametawala Uganda tangu mwaka wa 1986, na mtoto wake mwenye ushawishi mkubwa Muhoozi Kainerugaba.
 
Back
Top Bottom