Mahakama nchini Ufaransa yaamuru Mwanamuziki Koffi Olomide akamtwe upesi kwa ubakaji na udhalilishaji

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,544
108,871
Kumekucha!

Muda mfupi uliopita Mahakama nchini Ufaransa imeamuru Mwanamuziki Koffi Olomide akamatwe haraka na apelekwe nchini humo kujibu mashtaka ya Kupiga, Kubaka na Kuwadhalilisha Kingono Wanenguaji wake kati ya mwaka 2003 hadi 2006.

Hii imekuja baada ya Wanenguaji hao ambao ni Wanne ( 4 ) kudai kwamba kati ya hiyo miaka tajwa hapo juu Koffi Olomide alikuwa akiwadhalilisha mara kwa mara walipokuwa huko Jijini Paris nchini Ufaransa kwa kuwalazimisha kufanya ' Ngono ' na Wanaume ambao Koffi alikuwa akipokea Pesa kutoka Kwao kama malipo yake na kwa wale waliokuwa wakikataa basi alikuwa akiwapiga sana hadi kuwaumiza.

Madai yao hawa Wanenguaji hayakuishia tu hapa bali walienda mbele zaidi na kudai kwamba kuna nyakati ambapo walipokuwa nchini DRC wakirekodi mida ya Usiku Koffi Olomide alikuwa akiwalazimisha kufanya nao ' ngono ' na kwa aliyekuwa akigoma alikuwa akifukuzwa usiku huo huo hapo Studio au akinyimwa ' Ujira ' wake na kupoteza haki zake ndani ya Bendi hiyo.

Kilichowaumiza hawa Wanenguaji hadi wamefikia hatua hii ya Kudai haki yao Kisheria ni Kitendo cha Bosi wao za zamani Koffi Olomide pamoja na wale Wanaume aliokuwa akiwalazimisha kufanya nao Ngono kutotumia Kinga ( Condom ) kiasi kwamba kuna ambao walibebeshwa Mimba na hawana msaada wowote na kuna Wenzao wawili waliambukizwa Virusi vya UKIMWI na sasa hali zao bado ni mbaya sana.

Upuuzi huu wa Koffi Olomide huwezi kuukuta kwa Jean Bedele Tshituka Mpiana ( JB Mpiana ) na ndiyo maana ndiyo Mwanamuziki pekee nchini Congo DR hadi duniani kote anayependwa na Kuheshimika sana na Watu kwakuwa ni Mtu mwenye nidhamu ya hali ya juu, anajiheshimu na amelelewa maisha ya Kistaarabu mno kutoka kwa Mama yake Kipenzi aitwae Lusambo ( Mama Lusambo )

GENTAMYCINE huwa sipendagi ' Mijitu ' ya hovyo hovyo na daima milele nitampenda na kumuombea mafanikio sana Kimuziki ' Kipenzi ' changu JB Mpiana pamoja na Bendi yake mahiri na kabambe kabisa ya Wenge Bon Chic Bon Genre ( Wenge BCBG ) wazidi kuwa bora ili kuweza kumfundisha Koffi Olomide jinsi ya kuwa Mwanamuziki mstaarabu na asiwe kila siku anawaaibisha Wenzie.

Team JB Mpiana na Wenge BCBG wenzangu tuzidi tu Kufurahi na Team Koffi Olomide na Quarter Latin yake poleni sana na labda niwashaurini hamieni upesi kuanza kumpenda na kumshabikia JB Mpiana kwani hamtojutia na hamtozidi ' Kuaibishwa ' na Koffi wenu kila uchao / siku.

Nawasilisha.
 
Nilihisi tu ktk uzi huu jb mpiana hutaacha kumzungumzia hahaha!!Mzee wa EKOTITE anatafutwa!!ila yeye amesema ni hukumu aliyokuwa anaitegemea!!!!
 
Mapenzi yangu makubwa kwa JB Mpiana na Bendi yake ' tukuka ' ya Wenge BCBG ni sawa ya yale niliyonayo kwa Mtandao wangu huu pendwa kabisa wa JamiiForums Mkuu.
 
Huwa sichoki kuwaangalia/kuwasikiliza hawa BCBG!
Lakini nao hao, walikuwa wapi siku zote hizo! ?
 
Back
Top Bottom