Mahakama nchini Brazil yamuamuru Rais Jair Bolsonaro kuvaa barakoa. Atakiwa kuheshimu sheria za nchi

FRANC THE GREAT

JF-Expert Member
May 27, 2016
5,416
7,828
Habari!

Kutokana na kushamiri ama kuongezeka kwa maambukizi ya virusi vya corona nchini Brazil, Mahakama nchini humo imemuamuru Rais wa nchi hiyo Jair Bolsonaro kuvaa barakoa ya kinga la sivyo 'kukiona cha mtema kuni'.

c1_3589205.jpg

Jair Messias Bolsonaro.

Taarifa kamili:
Katika uamuzi uliotolewa Jumatatu, Jaji wa Mahakama ya Shirikisho nchini Brazil, Renato Borelli alisema kuwa Rais wa nchi hiyo kubwa zaidi katika bara la Amerika ya Kusini lazima avae barakoa mbele ya umma la sivyo atalazimika kulipa faini ya karibu dola 400 kwa siku.

"Rais ana jukumu la kikatiba la kuzingatia sheria zinazotumika nchini," mahakama ilisema katika uamuzi wake. "Utafutaji rahisi katika mtandao wa Google unatosha kupata ushahidi wa picha nyingi za Jair Messias Bolsonaro akizunguka mjini Brasilia na wilaya za karibu bila barakoa ya kinga."

Licha ya maambukizi ya virusi vya corona kuongezeka, Rais Bolsonaro amejitokeza mara kwa mara mbele ya umma bila barakoa wakati akisalimiana na wafuasi wake.

Bolsonaro alirekodiwa katika mkutano mmoja akikohoa bila kufunika mdomo wake na tukio jingine alionekana akipiga chafya katika mkono wake kisha kumshika mkono mwanamke mmoja.

Sharti la matumizi ya lazima ya barakoa lilitolewa Brasilia mnamo Aprili 30 na kutiliwa mkazo zaidi mnamo Mei 11 ambapo wale wote wenye kukiuka sharti hilo kutozwa faini ya real za Kibrazili 2,000 sawa na dola za Kimarekani 387.

Maamuzi ya mahakama yanamaanisha kuwa Bw Bolsonaro hayuko juu ya sheria hiyo na kwamba rais na maafisa wengine wote wa umma ambao hawatozingatia sharti hilo pia watapigwa faini.

Vyanzo: ABC, BBC
 
My take on this: Zile nchi 'zetu' fulani fulani zinapaswa kujifunza hapa katika kuheshimu na kulinda utawala wa sheria.
 
Hizi ndio mahakama zinazotakiwa, sio zile za wakata viuno na kuselebuka tu kwa mapambio
Najaribu tu ku-imagine, hivi mahakama zetu zinaweza zikapata ujasiri huo wa kumuamuru Rais Magufuli, avae barakoa na yeye mwenyewe akatii?

Ninajaribu tu kufikiria
 
Back
Top Bottom