MAHAKAMA, Mhimili unaotumiwa Kuficha Kuhojiwa? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

MAHAKAMA, Mhimili unaotumiwa Kuficha Kuhojiwa?

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by Sambwisi, Jul 17, 2012.

 1. S

  Sambwisi Senior Member

  #1
  Jul 17, 2012
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 166
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Tunayo mihimili mitatu ya Dola ambayo ni Serikali, Bunge na Mahakama. Katika miaka ya karibuni kumekuwapo na mtindo ambapo mambo ambayo yanaonekana na watawala kuwa nyeti na kwamba yatahojiwa sana na Umma hupelekwa Mahakamani haraka haraka hata kama uchunguzi bado!!

  Katika kuliangalia swala hilo nimegundua kwamba hiyo hufanywa makusudi ili mhimili wa Mahakama uwe kichaka cha kukataa kuhojiwa zaidi. Mfano halisi ni ule uliotumiwa na Kamanda Kova. Nimejiuliza katika sakata la Dr. Ulimboka ambalo uchunguzi wake bado kulikuwa na uharaka gani wa kumpeleka mtuhumiwa mahakamani ambaye ameonekana ana matatizo ya akili? Kwa nini asichukuwe hatua za kujiridhisha kuwa yule ni mtu timamu? Kwa nini kabla ya kumpeleka mahakamani asiwasiliane na wale walioripoti na kumpeleka Polisi? Kuna mambo mengi hayapelekwi Mahakamani utaishia kusikia faili limepelekwa kwa DPP. Je hili la Joshua halikupaswa kupelekwa kwa DPP?

  My take: Mahakama zinatumiwa kuficha na kukataa Umma kuhoji zaidi. Mifano ni mingi km Richmond, sakata la Maliasili n.k.

  Kwa hali hii tuziombe Mahakama zetu zifute kesi kama hizi pale ambapo itadaiwa uchunguzi haujakamilika ndani ya siku 60.

  Naomba kuwasilisha.
   
 2. Mjuni Lwambo

  Mjuni Lwambo JF-Expert Member

  #2
  Jul 18, 2012
  Joined: Apr 25, 2012
  Messages: 5,481
  Likes Received: 691
  Trophy Points: 280
  Kwa muda sasa nimekuwa na mashaka makubwa juu ya suala hili, inapofikiwa suala la shauri kuwa mahakamani, nina wasiwasi wa kutumiwa vibaya kwa mantiki nzima ya kuingilia uhuru wa mahakama, itafikia kipindi kuna suala nyeti linalotakiwa kupatiwa ufumbuzi haraka lakini chombo chenye mamlaka ya kuisimamia serikali(bunge) kitashindwa kutafuta ufumbuzi kwa sababu za kuingilia uhuru wa mahakama. solution ni pamoja na mhimili wa executive kupunguziwa mamlaka.
   
Loading...