Mahakama Manyara yamfunga miaka 20 jela kwa kukutwa na Meno ya Tembo

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Manyara imemtia hatiani na kumhukumu kifungo cha miaka 20 jela Alais Layeni kwa kosa la kukutwa na meno ya tembo.

Hukumu hiyo imetolewa leo Jumatatu Agosti 10,2020 mbele ya Hakimu Mkazi ,Mheshimiwa Simon Kobelo baada ya mahakama kuridhishwa na ushahidi uliotolewa mahakamani hapo.

Wakili wa serikali ambaye pia ni Mwendesha mashtaka mkuu wa mkoa wa Manyara Mutalemwa Kishenyi, alieleza kuwa mshtakiwa huyo alikamatwa Desemba 17/2019 katika kijiji cha Njoro wilaya ya Kiteto mkoa wa Manyara akiwa na meno manne ya tembo yenye thamani ya fedha za kitanzania shilingi Milioni 69,000,00 pasipo kuwa na kibali cha mkurugezi wa wanyamapori.

Wakili Kishenyi amesema katika shauri hilo la uhujumu uchumi namba 2 ya mwaka 2020, upande wa mashtaka ulikuwa na mashahidi wanne ambapo Mshtakiwa alijitetea na kuita shahidi mmoja.
 
Hiyo bei mbona nzuri, watuambie soko lake ni wapi kwenye mpunga namna hiyo!
 
Back
Top Bottom