Mahakama:Mali za Mtikila zinadiwe


MziziMkavu

MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Messages
39,987
Likes
5,376
Points
280
MziziMkavu

MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined Feb 3, 2009
39,987 5,376 280
KIONGOZI wa chama cha kisiasa cha DP, Christopher Mtikila anakabiliwa na hatari ya kufungwa jela baada ya mahakama kuamua kuwa iwapo zoezi la kuuza mali za mchungaji huyo ili kufidia deni la Sh8.8 milioni litashindikana, ombi la kumfunga litazingatiwa.
Awali Mahakama ya Wilaya ya Ilala ilikuwa imeamua kuwa nyumba ya mchungaji huyo iliyo Mikocheni jijini Dar es salaam iuzwe ili kufidia deni hilo, lakini Hakimu Hakimu Afumwisye Kibona jana alisitisha uamuzi huo na kuagiza mali zake nyingine ziuzwe kufanikisha malipo ya deni hilo.
Mtikila na mwenzake Mariam Issa wanadaiwa zaidi ya Sh8 milioni na Pascazia Matete ambaye anadai aliwakopesha wawili hao kwa ajili ya kufanyia biashara. Matete alishinda kesi namba 78 ya mwaka 2008 aliyoifungua katika Mahakama ya Mwanzo ya Kariakoo mbele ya Hakimu Benjamin Mwakasonda.
Akitoa amri hiyo, Hakimu Kibona alisisitiza kuwa iwapo ombi hilo la kutafuta mali mbadala za Mtikila ziuzwe kwa ajili ya kulipa deni hilo halitafanikiwa, ombi la kumfunga jela litafuatia. Alisema uamuzi huo wa kumfunga au kutomfunga utatolewa Machi 18 na Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Ilala, Joyce Minde.
Hatua hiyo ilifikiwa jana baada ya Matete kuomba mahakama iamuru nyumba ya Mtikila yenye namba MKC/MCB 1135 iliyo kwenye kiwanja namba 237, Kitalu C Mikocheni ambayo ni mali ya Mwenyekiti huyo iuzwe ili alipwe deni lake.
Matete alifungua kesi hiyo katika Mahakama ya Mwanzo ya Kariakoo na baadaye Mtikila kufanikiwa kuiahamishia Mahakama ya Wilaya ya Ilala kutoka na kutoridhika. Pamoja na kesi hiyo kuhamishiwa Ilala, Matete alishinda kutokana na Mchungaji Mtikila kutofika mahakamani.
Hata hivyo, ombi la kuuza nyumba hiyo lilishindikana baada ya kampuni ya kimataifa ya Cielmac kuwasilisha pingamizi ikieleza kuwa ilishanunua nyumba hiyo kwenye mnada uliofanywa na benki ya NBC baada ya Mtikila kushindwa kurejesha mkopo wa Sh15 milioni aliouchukua katika benki hiyo. Pingamizi hilo lilikuja wakati kampuni ya Comrade Auction Mart Court Brokes ikiwa imeshatangaza kuwa itaiuza nyumba hiyo kwenye kwenye mnada uliopangwa kufanyika Februari 6 mwaka huu.


http://www.mwananchi.co.tz/newsrids.asp?id=18346
 
M

major mkandala

Member
Joined
Mar 6, 2010
Messages
74
Likes
0
Points
0
M

major mkandala

Member
Joined Mar 6, 2010
74 0 0
hii ni aibu mwanasiasa na kelele zake kushindwa kulipa million 15
 
Kituko

Kituko

JF-Expert Member
Joined
Jan 12, 2009
Messages
9,557
Likes
7,452
Points
280
Kituko

Kituko

JF-Expert Member
Joined Jan 12, 2009
9,557 7,452 280
Alafu mtu kama huyo ndio awe Raisi wa nchi hii, au hata kaUwaziri tu si itakuwa balaa, madeni kila kona, hivi huyu uwaga ni mchungaji kweli au ni jina tu kama wengine wanavyojiita maprofesa na madokta?
 
G

Ghati Makamba

Member
Joined
Jun 29, 2009
Messages
37
Likes
0
Points
0
G

Ghati Makamba

Member
Joined Jun 29, 2009
37 0 0
Kuna vitu ambavyo wanadamu ni lazima tuvikumbuke na kuvichukulia kwa uzito unaostahili. Mtikila anaitwa Mchungaji, kila kukicha yeye na majalada yake uelekeo mahakamani, hiyo huduma ya Kimungu anatoa saa ngapi? ama ndiyo kusema anawatangazia walipo pale neno la Mungu kwa mfumo anaoujua yeye. Kukopa na kushindwa kulipa kwake ni haki maana matumizi ya haya madeni siyo sahihi. Nilimsikia anahojiwa BBC anadai akishindwa uteuzi ndani ya chama chake kugombea Urais, atasimama kama mgombea binafsi! Inachekesha!. Kama Mtikila hana watoto wanaostahiri kuridhi walau kipande cha ardhi tu alichonacho, basi mke wake afungue tu kesi mahakamani apewe walau kipande tu, ili siku Mtikila akifa kwa msukumo wa damu apate sehemu ya kuandalia mazishi. Hii ni kama laana, Mtikila hataisha mahakamani mpaka kiama chake.
 
MNDEE

MNDEE

JF-Expert Member
Joined
Jul 10, 2009
Messages
494
Likes
22
Points
0
MNDEE

MNDEE

JF-Expert Member
Joined Jul 10, 2009
494 22 0
Alafu mtu kama huyo ndio awe Raisi wa nchi hii, au hata kaUwaziri tu si itakuwa balaa, madeni kila kona, hivi huyu uwaga ni mchungaji kweli au ni jina tu kama wengine wanavyojiita maprofesa na madokta?
Mkuu, kama tutamjaji kwa kubezi kwenye maneno yanayotoka kimnywani mwake huyu ni mchungaji wa mshahara.
 
Buchanan

Buchanan

JF Diamond Member
Joined
May 19, 2009
Messages
13,211
Likes
385
Points
180
Buchanan

Buchanan

JF Diamond Member
Joined May 19, 2009
13,211 385 180
Katika kesi ya madai mshtakiwa kama akifungwa atakuwa ni 'Civil Prisoner' ambapo mlalamikaji anatakiwa amhudumie mfungwa kwa chakula, sabuni, nk mpaka amalize kifungo chake! Kwa hiyo mlalamikaji mifuko yake itaendelea kutoboka zaidi! Hivyo mlalamikaji ashughulikie kulipwa chake kuliko kifungo!
 
MziziMkavu

MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Messages
39,987
Likes
5,376
Points
280
MziziMkavu

MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined Feb 3, 2009
39,987 5,376 280
Mtikila sasa achague mali zake ziuzwe au aende jela Mahakama ya Wilaya ya Ilala, jijini Dar es Salaam, imeamuru mali za Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha Demokrasia Nchini (DP), Mchungaji Christopher Mtikila zikamatwe na kuuzwa ili zifidie deni la Sh. milioni 9.8 analodaiwa na mdai wake, Paskazia Matete.
Aidha, mahakama hiyo imeamuru kuwa, endapo zoezi hilo litashindikana, basi ombi lililotolewa na mdai Matete la kuomba Mchungaji Mtikila afungwe kifungo cha miezi sita gerezani, litatekelezwa.
Amri hiyo ilitolewa na Hakimu Mkuu Mkazi wa mahakama hiyo, Afumwisye Kibona, alipokuwa akisoma hukumu ya pingamizi la kesi ya madai lililofunguliwa na mdai, kampuni ya kimataifa ya CIELMAC.
Kampuni hiyo iliweka pingamizi mahakamani ili kusitisha mnada wa kuiuza nyumba inayodaiwa kuwa ya Mchungaji Mtikila aliyeshtakiwa kwa kesi ya madai ya fedha za Matete.
“Uchunguzi umebaini kuwa nyumba iliyoko kwenye kiwanja namba 273 Block ‘C’ kilichopo eneo la Mikocheni chenye umiliki wa hati namba 186311/ 37 inamilikiwa kihalali na Kampuni ya CIELMAC hivyo haiwezi kuuzwa na badala yake mali zingine za Mtikila zitafutwe zilipo ili zikamatwe na kuuzwa kufidia deni la Matete, ikishindikana ombi la kifungo litatekelezwa,” alisema Hakimu Kibona. Hakimu huyo alisema analipeleka jalada la kesi hiyo kwa Hakimu Mfawidhi wa mahakama ili kuandaa maombi hayo.
Awali, Matete aliiomba mahakama imfunge Mchungaji Mtikila miezi sita gerezani kwa madai kwamba anaisumbua mahakama na pia hataki kulipa deni lake analomdai alilomkopesha tangu Julai, 2007.CHANZO: NIPASHE
 

Forum statistics

Threads 1,250,043
Members 481,189
Posts 29,718,972