Mahakama Kuu yazizuia Kanuni za Maudhui Mtandaoni kutumika hadi Mahakama itoe uamuzi

View attachment 765380

Wakuu,

Mahakama Kuu kanda Mtwara leo imetoa zuio la muda(Temporary Injuction) dhidi ya matumizi ya Kanuni za Maudhui ya Kimtandao (Online Content Regulations) ambazo matumizi yake yamekwishaanza na tarehe ya mwisho ya bloga na mitandao kuridhia ilikuwa kesho tarehe 5 May 2018.

Maombi hayo yaliyowalishwa mahakamani na waombaji 6 wakiwemo Jamii Media, Legal and Human Rights Cente(LHRC), THRDC, MCT, TAMWA na TEF.

Katika kesi ya msingi ya mapatio ya kanuni hizo(Judicial review) washitakiwa ni Waziri wa Habari, Tanzania Communication Authority (TCRA) na Mwanasheria Mkuu wa Serikali(AG).

Katika maombi ya msingi waombaji wameiomba Mahakama kufanya mapitio ya kanuni hizo kwa vigezo hivi:
i) Waziri ametumia nguvu ya kisheria nje ya mamlaka yake (Ultra vires)
ii) Zinakiuka kanuni za usawa (Natural justice)
iii) Kanuni hizo zinapingana na Uhuru wa kujieleza (Freedom of Expression) Haki ya kusikilizwa(Rights to be heard) na haki ya usiri( Right to Privacy)

Kesi ya msingi imepangwa kusikilizwa tarehe 10 Mei 2018
View attachment 765463 View attachment 765462

Saafi sana kwa Judge Twais.
Hivi huyu atakua ni mmoja wa wale wateule 10 wa JPM hivi majuzi au ni mwIningine...!!
 
Watashindana lakini hawatashinda...Mungu akiwa upande wetu ninani aliye juu yetu...
 
Safari imeanza...

Lakini, si Mwakyembe alishawahi kukiri mwenyewe kuwa Mitandao ni vijiwe haziwezi kuwa controlled hivi?

Historia ni mwalimu mzuri sana. Wakati anatamka hayo Dr. Mwamyembe hope hakujua kijacho. Lakini Dr. Mwakyembe kapata maagizo kutoka JUU kuhusu kusajili blogs na yuotube channels, angefanyaje? Akatae kutii ili wanae wafe njaa?
 
Safi sana lakini huyo dhalimu anaweza kabisa kumfukuza kazi huyo hakimu au kumtisha ili hukumu iandikwe Ikulu.
Hongereni sana Maxence Melo na Jamii Forums yote.

04052018.jpg
 
44 Reactions
Reply
Back
Top Bottom