Mahakama Kuu yatupilia mbali pingamizi la awali dhidi ya maombi ya kuizuia kufanya kazi Bodi ya Wadhamini wa CUF

kirerenya

JF-Expert Member
Aug 27, 2013
1,696
2,252
CUF.jpg

Dar es Salaam. Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam imetupilia mbali pingamizi la awali dhidi ya maombi ya kuizuia kufanya kazi Bodi ya Wadhamini wa CUF, kambi ya mwenyekiti anayetambuliwa na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, Profesa Ibrahim Lipumba.

Uamuzi huo umetolewa leo Alhamisi na Jaji Wilfred Dyansobera aliyetupilia mbali hoja za pingamizi zilizotolewa na wajibu maombi wakipinga maombi yaliyofunguliwa na Mbunge wa Malindi(CUF), Zanzibar, Ally Saleh.

Kutokana na uamuzi huo, Mahakama itaanza kusikiliza maombi ya mbunge huyo anayeomba zuio dhidi ya Bodi ya Wadhamini wa CUF ambayo wajumbe wake waliteuliwa na Profesa Lipumba.

Akizungumza na waandishi wa habari mmoja wa mawakili wa CUF, Juma Nassoro kwa upande wa katibu mkuu wa chama hicho, Maalim Seif amesema Jaji Dyansobera ameamuru usikilizwaji ufanyike kwa njia ya maandishi.

Nassoro amesema muombaji ametakiwa kuwasilisha hoja zake Oktoba 19 na wajibu maombi wametakiwa wawe wamezijibu ifikapo Oktoba 27.

Amesema Jaji Dyansobera ameelekeza iwapo muombaji atakuwa na hoja za nyongeza awe ameziwasilisha ifikapo Novemba 4 na shauri litatajwa Novemba 6.

Mbunge Saleh alifungua maombi hayo kutokana na kesi ya msingi aliyoifungua mahakamani hapo akipinga uhalali wa wajumbe wa bodi walioteuliwa na Profesa Lipumba.

Anaiomba Mahakama itoe amri ya zuio la muda dhidi ya wadaiwa, wakala wao na watu wote wanaofanya kazi kwa maagizo yao kutokujihusisha kwa namna yoyote na masuala ya chama hicho mpaka uamuzi wa shauri lake la msingi utakapotolewa.

Wajibu maombi ni Ofisa Mtendaji wa Wakala wa Usajili, Udhamini na Ufilisi (Rita), aliyewakilishwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Wengine ni Bodi ya Wadhamini ya chama hicho, mwenyekiti wa bodi hiyo, Peter Malebo na wajumbe

Chanzo: Mwananchi
 
pic+CUF.jpg


Dar es Salaam. Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam imetupilia mbali pingamizi la awali dhidi ya maombi ya kuizuia kufanya kazi Bodi ya Wadhamini wa CUF, kambi ya mwenyekiti anayetambuliwa na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, Profesa Ibrahim Lipumba. Uamuzi huo umetolewa leo Alhamisi na Jaji Wilfred Dyansobera aliyetupilia mbali hoja za pingamizi zilizotolewa</a> na wajibu maombi wakipinga maombi yaliyofunguliwa na Mbunge wa Malindi(CUF), Zanzibar, Ally Saleh.

Kutokana na uamuzi huo, Mahakama itaanza kusikiliza maombi ya mbunge huyo anayeomba zuio dhidi ya Bodi ya Wadhamini wa CUF ambayo wajumbe wake waliteuliwa na Profesa Lipumba. Akizungumza na waandishi wa habari mmoja wa mawakili wa CUF, Juma Nassoro kwa upande wa katibu mkuu wa chama hicho, Maalim Seif amesema Jaji Dyansobera ameamuru usikilizwaji ufanyike kwa njia ya maandishi. Nassoro amesema muombaji ametakiwa kuwasilisha hoja zake Oktoba 19 na wajibu maombi wametakiwa wawe wamezijibu ifikapo Oktoba 27.

Amesema Jaji Dyansobera ameelekeza iwapo muombaji atakuwa na hoja za nyongeza awe ameziwasilisha ifikapo Novemba 4 na shauri litatajwa Novemba 6. Mbunge Saleh alifungua maombi hayo kutokana na kesi ya msingi aliyoifungua mahakamani hapo akipinga uhalali wa wajumbe wa bodi walioteuliwa na Profesa Lipumba.

Anaiomba Mahakama itoe amri ya zuio la muda dhidi ya wadaiwa, wakala wao na watu wote wanaofanya kazi kwa maagizo yao kutokujihusisha kwa namna yoyote na masuala ya chama hicho mpaka uamuzi wa shauri lake la msingi utakapotolewa. Wajibu maombi ni Ofisa Mtendaji wa Wakala wa Usajili, Udhamini na Ufilisi (Rita), aliyewakilishwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali. Wengine ni Bodi ya Wadhamini ya chama hicho, mwenyekiti wa bodi hiyo, Peter Malebo na wajumbe wa bodi hiyo.
 
Hakuna mahakama hapo,Maalim aangalie njia nyingine ya kupata haki,awe na plan B ya 2020 in case
 
Mnafikiri baada ya Mauaji ya Ally Juma Selemani yaliyotokea Zanzibar Lipumba nitakuwa awe wameamua kwa dhati kabisa kuacha kuifanyia kazi CCM.

Mauaji haya indirect Lipumba na wenzake ni washirika
 
Back
Top Bottom