Mahakama Kuu yatupilia mbali ombi la Mbowe kutokamatwa na Polisi

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,572
26,885
FB_IMG_1488455485917.jpg

Mwanasheria nguli Tanzania Generali Ulimwengu atinga mahakamani kama wakili wa Freeman Mbowe kwenye kesi yake dhidi ya Mkuu wa mkoa wa Dar es saalam.


MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam, imetupilia mbali maombi yaliyowasilishwa na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe ya kutaka asikamatwe hadi kesi yake ya kikatiba dhidi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda itakapomalizika.

Maombi hayo yalitupwa kwa sababu kifungu cha sheria kilichotumika kuyafungua si sahihi na kwamba hutumika pale ambapo sheria ziko kimya.

Uamuzi huo wa majaji umefikiwa kutokana na pingamizi la jamhuri lililowasilishwa na Wakili wa Serikali Mkuu Gabriel Malata kuiomba kuyatupilia mbali maombi hayo kwani hayana msingi kisheria.

Katika hatua nyingine, mwanahabari nguli nchini Jenerali Ulimwengu, ameungana na jopo la mawakili Tundu Lissu, Peter Kibatala na John Malya katika kumtetea Mbowe.

Mbowe amefungua kesi hiyo ya kikatiba namba 1, ya mwaka 2017 dhidi ya wadaiwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam na Ofisa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Kanda Maalumu ya Dar es Salaam. Kesi hiyo itasikilizwa tena Machi 8, mwaka huu.

CHANZO: Mtanzania
 
nimesikia mahakama imetoa maamuzi yake, vipi, tunaomba ruling ya mahakama jamani
 
Kwa hiyo serikali imeshinda pingamizi la kumkamata Mbowe? Hivyo imefurahi kwa kuwa sasa watamkamata bila shaka? Na hivyo ndivyo watampekua kuona kama anahusika na madawa ya kulevya,,kwa muda wote huu!!! Serikali itakuwa na lengo lingine labda zaidi ya hili la kumhusisha na madawa.Ngumu kumeza!!
 
Kwa hiyo serikali imeshinda pingamizi la kumkamata Mbowe? Hivyo imefurahi kwa kuwa sasa watamkamata bila shaka? Na hivyo ndivyo watampekua kuona kama anahusika na madawa ya kulevya,,kwa muda wote huu!!! Serikali itakuwa na lengo lingine labda zaidi ya hili la kumhusisha na madawa.Ngumu kumeza!!
Tulieni muone
tulisema Mbowe Mungu Ufipa na Chadema pekee
kwa serikali ya sasa ni Mtanzania kama watanzania wengine.
HAKUNA KUANGALIA SURA
 
Back
Top Bottom