Mahakama Kuu yatupilia mbali kesi ya kupinga Ndugai kujiuzulu Uspika. Yasema hakuna ukiukwaji wa Katiba uliofanywa

Vipi kuhusu rais kushinikiza spika kujiuzulu na kuondoa dhana nzima ya uhuru na kujitegemea kwa mihimili kwa minajili ya kuleta checks and balance, hii yenyewe haijavunja katiba...
 
Nilishasema Mbatia ni malaya sawa tu na wale wa Corner Bar Sinza tofauti ni yeye anavaa suruwali tu.

Hivi unapata wapi guts za kumtetea NDUGAI ambaye amenajisi Bunge kwenye miaka yake ya Uspika 2015-21?
 
Mwanasiasa Mbatia lengo lake limetimia.
Alijua tokavmwanzo hawezi shinda, ila jina lake limetajwa saba na vyombo vya habari na litakuwa kwenye kumbukumbu za mahakama!
Kapata kiki
Mjini mipango,na mjini ukiona umepotea kwenye ramani unatafuta pa kutokea..
 
Dar es Salaam. Mahakama Kuu ya Tanzania imetupilia mbali kesi iliyofunguliwa na Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia akipinga utaratibu aliotumia kujiuzulu aliyekuwa Spika wa Bunge, Job Ndugai.

Uamuzi huo umetolewa leo Ijumaa Januari 28, 2022 na jopo la majaji watatu wakiongozwa na Jaji John Mgeta ambao wamesema Ndugai alifuata utaratibu kwa kuwa aliwasilisha barua kwa mujibu wa ibara ndogo (1) (2) hakuna na shaka kwamba ibara hiyo inatoa taratibu ambazo Spika akitaka kujiuzulu lazima azifuate.

Jaji Mgeta amesema Bunge ni taasisi yenye maofisa wenye wajibu wa kutekeleza shughuli za kila siku moja ya maofisa hao ni Katibu wa Bunge.

"Kwa mujibu wa ibara ya 149 kifungu kidogo cha 2 imetajwa katibu kwamba notice ya kujiuzulu inaweza kuwasilisha kwake, kama Ndugai alikuwa na nia ya kujiuzulu Bunge siku hiyo halikukaa kikao je Ndugai angewasilisha wapi notice yake," amesema Mgeta

Amesema kwa mujibu wa ibara hiyo aliyetajwa ni katibu ndiye aliyepokea barua siku hiyo nakala ya kujiuzulu iliwasilishwa kwa mtu sahihi hivyo wamebaini taarifa aliyotuma Mbatia ilikuwa ni taarifa.
 
Hata mimi nimeishangaa hii barua. Au walibadili gia angani ili kunlfunika kombe mwanaharam apite?

Katibu wa bunge alipohojiwa alisema yeye hajaandikiwa barua bali amepata nakala ya barua ya spika kwenda kwa katibu mkuu wa chama chake kwa ajili ya kujiengua katika nafasi hiyo.
Hii barua itakuwa imechongwa usiku wa manane
 
Mbatia ana haki kikatiba kufanya alichofanya, ila angesoma vizuri ibara ya 149 (1-2) asingesumbuka. Kinachotajwa ni taarifa kwa mtu au kikao husika, na hakuna palipokatazwa nakala.

Aidha, shauri lake halina tija kabisa kisiasa. Tukomae kudai katiba mpya na bora, basi!
 

Leo tarehe 28.01.2022 Mahakama Kuu ya Tanzania chini ya majaji watatu wakiongozwa na Jaji Mgeta, imetupilia mbali kesi ya kikatiba Na 2 ya 2022 iliyofunguliwa na Mwenyekiti wa chama cha NCCR Mageuzi, Francis Mbatia dhidi ya aliyekuwa Spika wa bunge, Job Ndugai.

Mahakama imeeleza kuwa kesi hiyo haina mashiko kwa kuwa hakuna ukiukwaji wa Katiba uliofanywa. Mahakama imetambua barua iliyotolewa mahakamani na Wakili mkuu wa Serikali kuonesha kuwa Ndugai aliandika barua ya kujiuzulu kwenda kwa Katibu wa Bunge na nakala kwa Katibu Mkuu wa CCM ni halali na hivyo alifuata taratibu zote.

Nakala ya barua iliyotambuliwa na Mahakama ni hii hapa.


Pia soma

Ameamua Kuandika barua upya kurekebisha makosa mawili. Moja kuandika barua yote kwa herufi kubwa, na Pili kumwandikia barua ya kujiuzulu Katibu wa Bunge badala ya Katibu Mkuu wa CCM kama alivyofanya mwanzo.
 
K3si Dhaifu na isiyo na maslahi yeyote kwa umma

Ndugai alishaachia ngazi na Chama chake yaani CCM pamoja na Bunge vimeridhia

Hakukuwa na mgogoro wowote kuhusu kujiuzulu kwa ndugai na hata yeye hajawahi kanusha kuwa hakuwahi kujiuzulu

Aidha Mbatia hakuwa na ushahidi kuwa ndugai hakuwahi muandikia KATIBU wa Bunge moja kwa moja akieleza kusudio la kujiuzulu Kwake

Nimalizie kwa kusema kuwa Bunge ndilo lenye takwimu rasmi za kujiuzulu kwa ndugai na hakuna namna Mahakama inaweza pingana nalo
 
Mbatia ana haki kikatiba kufanya alichofanya, ila angesoma vizuri ibara ya 149 (1-2) asingesumbuka. Kinachotajwa ni taarifa kwa mtu au kikao husika, na hakuna palipokatazwa nakala. Aidha, shauri lake halina tija kabisa kisiasa. Tukomae kudai katiba mpya na bora, basi!
Nafikiri una kitu cha kujifunza zaidi! Soma hizi nakala then rudi tena utuambue ilikuwa sawa? Hii barua imendikwa tu katikati hapa baada ya kuona wataumbuka ila barua aliandikiwa katibu wa CCM na sio Katibu wa Bunge na mpaka Katibu wa Bunge alitoka kueleza kuwa anasubiri Katibu Mkuu wa Chama amjulishe ndo atasema kitu na barua zipo! Na ndiyo maana ata wameamua kufuta kwenye website zao za bunge na page social mediaView attachment 2098606
20220128_133025.jpg
KT.PNG
 
Vipi kuhusu rais kushinikiza spika kujiuzulu na kuondoa dhana nzima ya uhuru na kujitegemea kwa mihimili kwa minajili ya kuleta checks and balance, hii yenyewe haijavunja katiba...
Inavunja katiba, lakini hiyo mihimili ya Bunge na Mahakama ilikwijisalimisha miguuni mwa serikali na kujiua. Ni ya wasaka tonge.
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom