Mahakama Kuu yatoa zuio la kufanyika kwa Mkutano Mkuu wa CUF ulioandaliwa na Lipumba

Quinine

JF-Expert Member
Jul 26, 2010
19,425
2,000
Leo Tarehe 28/2/2019 Mahakama Kuu ya Tanzania Masjala Kuu ya Dar es salaam Mbele ya Mheshimiwa Jaji Stephen Magoiga, imetoa uamuzi wa kuzuia kufanyika kwa Mkutano Mkuu wa Chama cha Wananchi CUF uliopangwa na upande unaomuunga Mwenyekiti wa chama hicho Prof. Ibrahim Lipumba.

Uamuzi huo wa Mahakama Kuu unatokana na shauri Na. 248 la mwaka 2018 lililofunguliwa kwa pamoja na Manaibu Katibu Wakuu Mhe. Joran Lwehabura Bashange (Tanzania Bara) na Mhe. Nassor Ahmed Mazrui (Zanzibar) chini ya mawakili wa Chama hicho waheshimiwa Juma Nassoro Dovutwa, Daimu Halfani na Loveness Denis.

Hili ni pigo la pili kwa kambi hiyo ya Mwenyekiti baada ya wiki iliyopita Mahakama Kuu kuifuta bodi yake ya wadhamini kupitia shauri Na.13 la mwaka 2017 lililofunguliwa na Mhe. Ally Saleh (Mbunge) dhidi ya RITA na wengine 17.

Katika uamuzi wake Mhe. Jaji Magoiga amesema, mahakama imejiridhisha kuwa kwa kutolewa zuio hilo wadaiwa (Respondents) hawatadhurika chochote, lakini kinyume chake zuio lisipotolewa waleta maombi (Applicants) watapata madhara makubwa ikiwemo kufukuzwa uongozi, uanachama wao na hivyo kukosa haki zao za msingi za kikatiba.

Mahakama imepanga shauri Na. 284 la mwaka 2018 liitwe Tarehe 3/4/2019 kwa ajili ya usikilizwaji wa awaji (Pre trial conference).
 

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,260
2,000
KUHUSU MAHAKAMA KUU KUZUIA KUFANYIKA KWA MKUTANO MKUU FEKI WA LIPUMBA:

THE CIVIC UNITED FRONT
(CUF – Chama Cha Wananchi)

TAREHE: 28 FEBRUARY, 2019

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI NA UMMA

KUHUSU MAHAKAMA KUU KUZUIA KUFANYIKA KWA MKUTANO MKUU FEKI WA LIPUMBA:

 CUF yambwaga tena Lipumba na genge lake.
 Mahakama yashangazwa na wakili wa Lipumba Mashaka Ngole kupingana na AMRI YA MAHAKAMA (Clear Abrogation of Court Orders).
 Ni ushindi wa Shauri la 15 kati ya mashauri 37 yaliyofunguliwa Mahakamani.
 Sasa Chama kimo katika mikono salama.
 Kisiki cha Mpingo (Lipumba) chageuka Mpapai, kifo cha mende, chaliiii.

Leo Tarehe 28/2/2019 Mahakama Kuu ya Tanzania Masjala Kuu ya Dar es salaam Mbele ya Mheshimiwa Jaji Stephen Magoiga, imetoa uamuzi wa kuzuia kufanyika Mkutano Mkuu feki wa Lipumba na genge lake uliopangwa kwa shinikizo la Msajili wa vyama vya siasa Jaji Francis Katabazi Mutungi kwa lengo la kumfukuza Katibu Mkuu Maalim Seif Sharif Hamad na viongozi wenzake halali wa CUF-Chama cha Wananchi, waliopatikana kupitia Mkutano Mkuu wa Taifa wa CUF uliofanyika Tarehe 23 – 27 Juni, 2014 katika ukumbi wa Blue Pearl Hotel wa Ubungo Plaza jijini Dar es salaam.

Uamuzi huo wa Mahakama Kuu unatokana na shauri Na. 248 la mwaka 2018 lililofunguliwa kwa pamoja na Manaibu Katibu Wakuu Mhe. Joran Lwehabura Bashange (Tanzania Bara) na Mhe. Nassor Ahmed Mazrui (Zanzibar) Tarehe 15 Mei, 2018 baada ya kupata taarifa za maandalizi ya Mkutano huo FEKI. Lipumba na genge lake kwa kushirikiana na Msajili wa vyama vya siasa Jaji Mutungi walipanga kufanya mkutano huo kama njia ya kujinusuru na maamuzi ya Mahakama Kuu kutokana na kesi kadhaa zilizofunguliwa na Bodi ya Wadhamini, viongozi, Wabunge na wanachama mbali mbali.

Hatua hiyo ya kufanya Mkutano Mkuu ni jaribio la pili la kutaka kuingilia uhuru wa Mahakama katika kutenda haki, baada ya hatua ya mwanzo ya kutaka kufuta mashauri yote mahakamani kwa kutumia bodi yao feki iliyosajiliwa na RITA kushindikana. Bodi hiyo FEKI IMEFUTWA NA MAHAKAMA KUU TAREHE 18 FEBRUARI, 2019 kupitia shauri Na. 13 la mwaka 2017 lililofunguliwa na Mhe. Ally Saleh (Mbunge) dhidi ya RITA na wengine 17.

Katika uamuzi wake Mhe. Jaji Magoiga, amefanya uchambuzi wa maombi yaliyowasilishwa mahakamani na waheshimiwa Manaibu Katibu Wakuu wa CUF Mhe. Joran na Mhe. Mazrui na kusema yamekidhi vigezo vyote vya kisheria (filed on the enabling provions of law). Aidha katika kupitia hati ya kiapo (Affidavit) iliyowasilishwa na Mhe. Joran Bashange kwa niaba ya waleta maombi (Applicants) imedhihirika kuwa wadaiwa (Respondents) ambao ndio wamejumuika kuandaa mkutano huo FEKI WAPO KATIKA MAKUNDI YA AMA WAMEFUKUZWA, WAMESIMAMISHWA AU SI VIONGOZI WALIOCHAGULIWA AU KUTEULIWA NA VYOMBO VYA KIKATIBA VYA CUF-CHAMA CHA WANANCHI.

Katika kupitia hoja za waleta maombi (Applicants Written Submissions in chief) zilizofafanua kwa nini Mahakama itoe zuio kwa Mkutano Mkuu feki wa Lipumba, Mahakama imeridhishwa na hoja nzito na zenye mashiko zilizoungwa mkono na vielelezo (authorities) mbali mbali zikiwemo hukumu za;

 American Cynamid Co (No.1) vs Ethicon Ltd(1975) AC 396
 Prestor vs Luck (1884) Ch. D 497
 The State of Karnataka and Others vs S. Venkarataj, 1975(1) KaLJ 142 (India)
 Kiyimba Kaggwa vs Katende (1985) UGHCCD 1
 Harbib Singh vs Shaheed UdhamSingh Smarak, I.A.NOS.11323/2008 (India)
 Atilio vs Mbowe (1969) H.C.D. No. 284 (Court of Appeal of Tanzania)
 Ndema and others vs Mubiru, Misc. Application No. 225 of 2013 (Uganda)
 Giella vs Cassman Brown and Co. Ltd. (1973) EA 358 (Mahakama ya Afrika Mashariki) miongoni mwa nyinginezo nyingi.

Kwa kuangalia athari zinazoweza kujitokeza kwa kutolewa au kutotolewa zuio (Balance of Convenience) mahakama imejiridhisha kuwa kwa kutolewa zuio wadaiwa (Respondents) hawatadhurika chochote, lakini kinyume chake zuio lisipotolewa waleta maombi (Applicants) watapata madhara makubwa ikiwemo kufukuzwa uongozi, uanachama wao na hivyo kukosa haki zao za msingi za kikatiba.

Kwa upande mwingine Mahakama haikupokea majibu ya hoja (Reply Submissions) kutoka wadaiwa wote jambo lililothibitisha kuwa hawakuwa na chochote cha kupinga au walihemewa na hoja nzito na zenye mashiko zilizojengwa na upande wa waleta maombi. Mdaiwa Na. 2 ambaye ni wakili Mashaka Ngole aliwasilisha hoja zake akijitambulisha kuwa ni wakili wa wajibu maombi wote (Counsel for all Respondents) jambo ambalo linapingana na amri ya Mahakama Kuu iliyotolewa Tarehe 13 Julai, 2018 na Jaji R.K.Sameji ikimzuia kuwa hawezi kuwa wakili wa wadaiwa kwa sababu sheria inakataza wakili mdaiwa kuwatetea wadaiwa wenzake. Na kama yeye anasimama kujitetea anasimama kama mdaiwa na sio wakili (where an advocate is a party in the litigant he does so as a litigant, and he is not entitled to conduct his case from the bar as an advocate).

Msimamo huo ni kwa mujibu wa Mahakama ya Rufaa ya Tanzania katika shauri la Laemthong Rice Co. Ltd. Kwa msingi huo majibu ya wakili wa Lipumba Mashaka Ngole yametupwa kwa kukinzana na matakwa ya sheria na uamuzi wa Mahakama Kuu na hivyo naye kuhesabika kushindwa kujibu hoja za waleta maombi (Applicants).

Kwa uchambuzi huo, MAHAKAMA KUU IMETOA AMRI YA ZUIO kwa Prof. Ibrahim Haruna Lipumba, Mashaka Ngole, Magdalena Sakaya, Abdul Juma Kambaya, Jafari Mneke, Thomas D.C. Malima, Omar Mhina Masoud, Salma Masoud, Haroub Mohamed Shamis, Khalifa Suleiman Khalifa, Mohamed Habib Mnyaa, Nassor Seif Amour, Thiney Juma Mohamed, Rukia Kassim Ahmed, Kapasha H. Kapasha, Maftaha Nachuma na wote wanaofanya kazi chini yao, amri yao au kwa maelekezo yao kuitisha Mkutano Mkuu wowote kwa jina la CUF-Chama Cha Wananchi mpaka hapo shauri la msingi Na. 84 la mwaka 2018 litakaposikilizwa na kutolewa uamuzi.

Mahakama imepanga shauri Na. 84 la mwaka 2018 liitwe Tarehe 3/4/2019 kwa ajili ya usikilizwaji wa awaji (Pre trial conference).

Pongezi nyingi ziwaendee wasomi mawakili wa Chama waheshimiwa Juma Nassoro Dovutwa, Daimu Halfani na Loveness Denis kwa umakini na umahiri wao kubwa katika kusimamia mashauri ya Chama. Aidha Chama kinawapongeza Manaibu Katibu Mkuu waheshimiwa Joran Lwehabura Bashange na Nassor Ahmed Mazrui kwa kuchukua harua za haraka na kwa wakati muafaka, kuwazuia WASALITI na VIBARAKA kuendeleza uharibifu wao ndani ya CHAMA.


HAKI SAWA KWA WOTE

Imetolewa na Kurugenzi ya Habari CUF-Taifa

SALIM BIMAN
MKURUGENZI HABARI.
+255777 414112
+255655 314112

MBARALA MAHARAGANDE
NAIBU MKURUGENZI HABARI.
maharagande@gmail.com
+255715 062577
+255767 062577
 

kandamatope

JF-Expert Member
May 19, 2018
536
1,000
Kila wanapo fungua kesi upande wa Maalim seif ndio unaokata tamaa,kesi wanazifungua wao kwa shangwe zote alafu wanapukutika wao kwa kukata tamaa
Kaaanza kuondoka mwenyekiti wa kamati
Kisha akafuhatia mbunge wa kinondoni
akafuhatia mbunge wa temeke mzee wa kwenda kufagia Buguruni kisha akajifagia mwenyewe
Akafuhatia mbunge wa Liwale kuchauka kutoka kambi hiyo hiyo
hiyo ni kesi ya 41
Mwisho wa hii movie ni 2025..

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom