Mahakama Kuu yatoa maelekezo maridhiano familia Bilionea Msuya

Suley2019

JF-Expert Member
Oct 7, 2019
1,811
4,533
Mahakama Kuu kanda ya Arusha imetoa miezi kwa pande mbili za familia za aliyekuwa mfanya biashara Marehemu Erasto Msuya maarfu kama Bilionea Msuya zenye mgogoro wa kugombea mali zilizoachwa na Bilionea huyo kukaa meza moja kuondoa tofauti. Kadhalika, Mahakama hiyo imezielekeza pande hizo kupeleka mrejesho mahakamani baada ya muda huo kupita.

Akitoa uamuzi huo, Jaji wa Mahakama hiyo, Johannes Masara, alisema mahakama imeridhia ombi la upande wa mleta maombi Ndeshukulwa Msuya, la kuomba mahakama kuondoa shauri lake la mirathi kwa muda ili familia hizo zifanye mazungumzo.

Alisema mahakama baada ya kupokea ombi la mleta maombi, imekubali pande hizo, kukaa meza moja kupitia Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Jerry Muro, na imetoa miezi miwili kupata mrejesho.

Akizungumza na waandishi wa habari nje viwanja vya mahakama, Ndeshukurwa alisema uamuzi wa mahakama umetenda haki, na umezingatia maslahi mapana ya pande zote mbili na anaamini jambo hilo, litamalizika na watoto wa Bilionea Msuya watapata haki yao ya msingi.

Alisema suala la maridhiano liliibuliwa na DC Muro na aliwataka ndugu hao, waondoe kesi iliyopo mahakamani ili wakae meza moja ya mazungumzo, na aliahidi kusaidia kusimamia mazungumzo hayo.

Awali, wakili wa upande wa wajibu maombi, Shilinde Ngalula, alipinga hatua ya mahakama hiyo kukubali ombi la kuondoa kesi hiyo, kwa muda na alitaka mahakama ifute kabisa kesi hiyo, na kusiwapo shauri hilo, mahakamani wakati wa maridhiano nje ya mahakama.

Hata hivyo, Jaji Masara alikataa ombi hilo, na kukubali ombi la upande wa waleta maombi la kuondoa kesi hiyo kwa muda bila kuifuta kisha kurejea meza ya mazungumzo na iwapo familia hizo hazitakubaliana watarejea mahakamani kuendelea na shauri hilo kwa ajili ya kutolewa uamuzi.

Ndeshukurwa, mama mzazi wa Bilionea Msuya anapinga Miriamu Mrita, ambaye ni mke wa Msuya kuwa msimamizi wa mirathi, akidai kuwa ameshindwa kugawanya mali za mumewe kwa wanufaika kwa kipindi cha miaka saba tangu kifo cha Msuya.

Bilionea Msuya aliuawa kwa kupigwa risasi zaidi ya 20 mwaka 2013 wilayani Hai, mkoani Kilimanjaro.

Ndesgukurwa anadai kwamba Miriamu ambaye ndiye msimamizi wa mirathi, yuko mahabusu gerezani kwa muda mrefu akikabiliwa na kesi ya mauaji ya wifi yake, Anet Msuya, hivyo hatua hiyo imesababisha baadhi ya mali za Bilionea Msuya kupotea na watoto wake kushindwa kupatiwa mgawanyo wa mali zao.

IPP Media
 
Back
Top Bottom