Mahakama Kuu yatengua hukumu dhidi ya Joseph Mbilinyi (Mb)

Informer

JF-Expert Member
Jul 29, 2006
1,582
6,627
Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Mbeya leo tarehe 11 October 2019 imetengua Hukumu, Mwenendo na Kifungo alichohukumiwa Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi aka Sugu kwa kile ambacho Mahahaka Kuu imeeleza kuwa ni ubatili wa mwenendo katika kesi hiyo.

Akisoma Uamuzi wa Rufaa Nambari 29 ya Mwaka 2018 iliyowasilishwa na Sugu kupitia Mawakili Peter Kibatala na Faraji Mangula, Jaji Utamwa amesema kwamba kulikuwa na Makosa yasiyotibika katika mwenendo wa shauri hilo, hasa pale ambapo aliyekuwa Hakimu Mwandamizi Mteite wa Mahakama ya Hakimu Mkazi ya Mbeya aliposhindwa kuwasomea Mashtaka Washtakiwa katika hatua ya usikilizaji wa awali (Preliminary Hearing).

Katika Hukumu yake iliyosomwa na Naibu Msajili wa Mahakama wa Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya, Jaji Utamwa alisema kwamba hakubaliani na hoja za upande wa Serikali ambao ni Wajibu Rufaa kwamba mapungufu hayo yanatibika, na badala yake Jaji Utamwa amesema kwamba makosa hayo yanaathiri mwenendo mzima wa kesi iliyopelekea kufungwa kwa Sugu na mwenzake Emmanuel Masonga.

Jaji Utamwa ametengua Hukumu, Mwenendo mzima wa kesi na adhabu ya kifungo waliyohukumiwa Sugu na Masonga.

Zaidi soma;

Mbunge wa Mbeya Joseph Mbilinyi "Sugu" na Emmanuel Masonga, Wahukumiwa kwenda jela miezi Mitano kwa kosa la Uchochezi
 
Nimekusoma. Inaonekana unakubaliana na aliyesema hawa jamaa ni waonevu na wanajimwambafai...
Maana gani? Lengo lao ilikuwa Sugu afungwe. Alishafungwa. Hukumu ya leo ina maana gani tena wakati wameshamnyoosha kama walivyotaka? Hata kina Mbowe hakimu/judge atakuja aseme hawana kesi ya kujibu. Lakini walishalala sana ndani. Tunza hii comments
 
Pamoja na yote JOGWE jera alikaa msoto alipata hiyo ndio ilikuwa dhamira yetu tumnyooshe kidogo ili kumkata wenge na tulifanikisha so endeleeni kupiga makofi next episode ni mwenyekiti na genge lake wale wataenda ndani miaka miwili miwili tu wakitoka uko tushachukua jimbo hai, kawe na kibamba hii ndio adhima yetu

Kidumu chama cha mapinduzi
Kama wewe mada kama Mimi like hapa viva magu viva
 
Back
Top Bottom