Mahakama Kuu yaridhia mbunge mteule wa Singida Mashariki, Miraji Mtaturu(CCM) kuapishwa. Maombi ya Lissu kupinga mambo kadhaa kutolewa uamuzi Sept 9

Mimi jamani sijaelewa vizuri.
Inawezekana kuwa ni kweli Mahakama haina uwezo wa kuzuia shughuli za Bunge ikiwemo hili swala la kuapishwa mbunge mteule.
Lakini je, Bunge nalo linaweza kuendelea na swala lililoko mahakani?
Huku sio kuingilia Mahakama?
Naomba wataalam wa sheria wanijuze.
 
Attachments

  • 1566837386572.jpeg
    1566837386572.jpeg
    89.3 KB · Views: 21
Mimi jamani sijaelewa vizuri.
Inawezekana kuwa ni kweli Mahakama haina uwezo wa kuzuia shughuli za Bunge ikiwemo hili swala la kuapishwa mbunge mteule.
Lakini je, Bunge nalo linaweza kuendelea na swala lililoko mahakani?
Huku sio kuingilia Mahakama?
Naomba wataalam wa sheria wanijuze.

Katiba imefanyiwa badiliko, Bunge linauwezo wa kujadili na kufanya maamuzi ya suala lililoko Mahakamani.

AWAMU YA TANO OYEE!!!!!!!!!??????
 
Mhe Jaji: Wewe Unaelewa Nini ?

Wakili wa Serikali
Anasoma Tena Na Paragraph Hiyo Na Kusema Mnamo Tar... Tajwa Hapo Mhe Spika Aliandikia Tume ya.Uchaguzi Barua na Kuitararifu Kiti Cha Ubunge singida Mashariki Kipo wazi Kwa Mujibu Wa Kanuni.

Mhe Jaji: Hamna Barua Yoyote ya Lissu Ikiwajuza Yupo Wapi !?

Wakili wa Serikali: Katika Ambatanisho hizi Mhe Lissu kashaliandikia Bunge jumla Ya Barua 6 akiwa Hospitali na Katika Kifungu F ameanisha Viongozi waliomtembelea akiwepo Mhe Samia Suluhu Hassan, Makamu wa Rais JMT

Mhe Jaji: Barua aliziandika Akiwa wapi?

Wakili wa Serikali: Aliandika Nyingine akiwa Nairobi na Nyingine Akiwa Ubelgiji

Mhe Jaji: Huko Alikuwa anafanya Nini?

Wakili wa Serikali: Hatujui, hakulitaarifu Bunge

Wakili wa Serikali anaendelea, Kiapo Cha Allute Mughwai Lissu hakijakamilika sababu hakijaonyesha mleta Maombi Alikuwa na Interest Gani Kuleta Shauri Hili Katika Mahakama Hii Tukufu, In Case Mtaturu akiapishwa mlalamikaji ataumia kwa kiasi gani.

Kesi za Jamhuri zilizoainishwa na Wakili Kibatala zilishatenguliwa maamuzi hayo.

Mhe Jaji sio mara ya kwanza kwa Mahakama hii kupuuzia ombi la mtu yeyote aliyeshindwa kuainisha interest zake. Anarejea baadhi ya kesi zilizopita.

Mhe Jaji: Mlalamikaji alikuwa Mbunge wa Singida Mashariki?

Wakili wa Serikali:Hilo sina Ubishi Nalo

Mhe Jaji: Nini Kilitokea Tarehe 28/06/2019

Wakili wa Serikali: Kilichotangazwa Ubunge wa Lissu Ulikoma kwa mujibu wa sheria za Tanzania

Mhe Jaji: Nendea Kwenye Sheria kifungu Cha 83 Katiba ya JMT inasemaje?

Wakili wa Serikali: Nimepaona na inaelekeza kukoma kwa Ubunge wa Mbunge

Mhe Jaji: Ombi la Mlalamikaji Linasemaje ?

Wakili wa Serikali anajibu

Mhe Jaji: Sasa Hapo Umesoma Nini Na Unatetea Nini Hapa ? Kasome Katiba Kifungu Cha 71 katiba ya JMT inasemaje...

Wakili wa Serikali: Inasema Mbunge atakosa Sifa za Kuwa Mbunge kwa Kukosa Vigezo Vifuatavyo
(A)Atakosa kuhudhuria Vikao 3 mfululizo.

Mhe Jaji: Nitawabana Maswali Mengi sana. Je, Mpo Tayari?

Wakili wa Serikali: Anakubali Kujibu
 
Toa post yoyote niliyosifia maamuzi ya wiki iliyopita, najua fika kwenye kesi ya mpinzani hasa hiyo ya Lissu hakuna haki kutendeka. Hizo mahakama zinasimamia maamuzi ya watawala na sio haki.
So week iliyopita watawala waliagiza maombi ya upande wao yatupiliwe mbali?
 
So week iliyopita watawala waliagiza maombi ya upande wao yatupiliwe mbali?

Tafuta post yoyote ya kwangu ya hiyo wiki iliyopita kama kuna popote nilishangalia hiyo Hadaa ya mahakama. Kwa taarifa yako wapinzani wanaenda kwenye mahakama hizi za ndani,sio kwakuwa wanategemea kupata haki, bali ni kwakuwa hawana namna. Wangeweza wangetumia mahakama za nje kama wawekezaji. Hilo halina mjadala boss.
 
Mbona mkishinda hatusikii habari za muhimili kuingiliwa zaidi ya kuwasifu mawakili wenu kuwa ni wazuri na kumsifu jaji?

Wapinzani wakishinda huko mahakamani huwa hawashangilii au kukiri kutendewa haki, bali huwa wanashangaa mahakama zimethubutu vipi kutenda haki. Na mara nyingi mahakimu au majaji waliowapa haki wapinzani huchukuliwa kuwa sio wazalendo kwa wanaojisifu kuwalipa. Habari ndio hiyo.

Ukitaka kujua serikali hii inaingilia mambo ya mahakama na mifumo ya kutoa haki, rejea vitisho vya msemaji wa serikali dhidi ya mawakili wa mzungu wa ndege ya rais.
 
Jaji kaamtendea haki Lisu kaahirisha kesi yake Hadi tarehe 9 septmba.Lisu Kuna kinachosemekana anarudi tarehe 7 septemba.Kwa hiyo tatehe 8 atapumzika bila shaka siku ya kesi tarehe 9 ataenda mwenyewe mahakamani akajieleze badala ya kuachia wengine.Mawakili hakikisheni mnaenda naye na dereva wake akimsindikiza
 
Watanzania wenzangu wazalendo na wapenda nchi hii ya amani salaamu kwenyu nyote.
Rais wetu John Pombe Magufuli amekuwa akisema Watanzania siyo wajinga lakini kiuhalisia kauli hii haitoki moyoni baali mdomoni tu. Unaposoma katikati ya mistari huyu Rais anasema kwa sauti kubwa kabisa kuwa WATANZANIA NI WAJINGA SANA! Nitaeleza.

Jana katika mnyukano wa Mawakili 19( 14-Serikali na 5- Utetezi wa Lissu)tulitegemea kwamba Jaji MATUPA angelitoa maamuzi ya kuzuia kuapishwa kwa Mbunge mteule Jumanne Mtaturu kuwa Mbunge wa Singida Mashariki kwa vile KUNA KESI YA MSINGI MAHAKAMANI mpaka itakaposikilizwa na kutolewa hukumu lakini haikuwa hivo. Leo tarehe 3/9/2019 katika kikao cha Bunge mkutano wa 16 Spika asiye na haya wala aibu Job Ndugai ameamua kumwapisha Mtaturu kwa jeuri na kibri kwa vile anajua kinachoendelea na maamuzi yatakayotolewa tarehe 9/9/2019.

Kuna vitu havihitaji kupiga ramli wala kusoma nyota kama walivokuwa wakifanya kina merehemu Sheikh Yahya. Tangu kufunguliwa kwa kesi hii ya Lissu kudai Ubunge wake kumekuwa na mikakati ya kuhakikisha Tundu Lissu harudi Bungeni hata kama ni kwa mtutu!!! Kilichofanyika jana ilikuwa ni dilly dallying tu ya kuzunga na kupoteza muda ili Mtaturu aapishwe halafu tarehe 9 Septemba Jaji Matupa anamaliza mchezo.

Jaji Matupa tayari ana maelekezo toka juu(inaeleweka kwa utawala huu) kwamba piga ua Tundu Antipas Lissu asirudi Bungeni. Kwanza ilikuwa kuchelewesha hukumu ya kesi ili kutoa nafasi kwa Mbunge mteule kuapishwa na kitakachofuata ni kumaliza mchezo kwa kupangua hoja zote za Wakili msomi Peter Kibatala ili kuhalalisha kuwa maamuzi ya Spika kumvua Ubunge Tundu Lissu yalikuwa sahihi. Kwa kuhitimisha niseme kwamba tusitegemee mabadiliko yoyote katika hukumu hiyoo ya tarehe 9 Septemba, 2019 kwani hukumu ilishaandikwa mapema hata kabla ya tarehe husika. KInachokuwa kinaendelea Mahakamani na kilichofanyika Bungeni leo hakika ni uthibitisho ya kitakacho amualiwa tarehe 9. Ukweli ni kwamba Mahakama, Bunge na Serikali wanajua wanachokifanya kwa kucheza na akili za Wadanganyika ili kuendelea kuwafanya wajinga kila siku.Kwa nchi yeyote yenye kufuata utawala wa Katiba ba sheria SPIKA WA BUNGE ALITAKIWA LEO ASIMWAPISHE MTATURU mpaka kesi ya msingi itakapotolewa maamuzi. Kulikuwa na haraka gani kusubiri mpaka hiyo tarehe 9 Septemba ambayo ni wiki ijayo tu???!!!!Kuna kitu hakiko sawa hapa...!!!

Tusubiri uamuzi wa Jaji Matupa kama utakuwa kinyume na haya niliyoyasema. Na kama itatokea akafanya maamuzi kinyume na maelekezo hatutashangaa kusikia akianza kuhojiwa uraia na uzalendo wake. Time gonna tell!
 
Ni vema kusubiri , ikumbukwe kwamba Mahakama inatambua kwamba Lissu anatibiwa nje ya nchi na ndio maana imesimamisha kesi zinazomkabili
 
Jibu liko wazi tu.... Mahakama ni mhimili unaojitegemea kama ulivyo muhimili wa Bunge, Siyo rahisi hivyo mahakama kuingilia maamuzi ya kibunge bila kuanzisha mgogoro. Naamini hata huyo wakili anaesimamia hiyo kesi anafahamu hivyo ila maamuzi tayari yako wazi. Ila kuchangia maduhuri ya muhimili wa Mahakama siyo vibaya pia... kama pesa unazo za kutosha.
 
Watanzania wenzangu wazalendo na wapenda nchi hii ya amani salaamu kwenyu nyote.
Rais wetu John Pombe Magufuli amekuwa akisema Watanzania siyo wajinga lakini kiuhalisia kauli hii haitoki moyoni baali mdomoni tu. Unaposoma katikati ya mistari huyu Rais anasema kwa sauti kubwa kabisa kuwa WATANZANIA NI WAJINGA SANA! Nitaeleza.

Jana katika mnyukano wa Mawakili 19( 14-Serikali na 5- Utetezi wa Lissu)tulitegemea kwamba Jaji MATUPA angelitoa maamuzi ya kuzuia kuapishwa kwa Mbunge mteule Jumanne Mtaturu kuwa Mbunge wa Singida Mashariki kwa vile KUNA KESI YA MSINGI MAHAKAMANI mpaka itakaposikilizwa na kutolewa hukumu lakini haikuwa hivo. Leo tarehe 3/9/2019 katika kikao cha Bunge mkutano wa 16 Spika asiye na haya wala aibu Job Ndugai ameamua kumwapisha Mtaturu kwa jeuri na kibri kwa vile anajua kinachoendelea na maamuzi yatakayotolewa tarehe 9/9/2019.

Kuna vitu havihitaji kupiga ramli wala kusoma nyota kama walivokuwa wakifanya kina merehemu Sheikh Yahya. Tangu kufunguliwa kwa kesi hii ya Lissu kudai Ubunge wake kumekuwa na mikakati ya kuhakikisha Tundu Lissu harudi Bungeni hata kama ni kwa mtutu!!! Kilichofanyika jana ilikuwa ni dilly dallying tu ya kuzunga na kupoteza muda ili Mtaturu aapishwe halafu tarehe 9 Septemba Jaji Matupa anamaliza mchezo.

Jaji Matupa tayari ana maelekezo toka juu(inaeleweka kwa utawala huu) kwamba piga ua Tundu Antipas Lissu asirudi Bungeni. Kwanza ilikuwa kuchelewesha hukumu ya kesi ili kutoa nafasi kwa Mbunge mteule kuapishwa na kitakachofuata ni kumaliza mchezo kwa kupangua hoja zote za Wakili msomi Peter Kibatala ili kuhalalisha kuwa maamuzi ya Spika kumvua Ubunge Tundu Lissu yalikuwa sahihi. Kwa kuhitimisha niseme kwamba tusitegemee mabadiliko yoyote katika hukumu hiyoo ya tarehe 9 Septemba, 2019 kwani hukumu ilishaandikwa mapema hata kabla ya tarehe husika. KInachokuwa kinaendelea Mahakamani na kilichofanyika Bungeni leo hakika ni uthibitisho ya kitakacho amualiwa tarehe 9. Ukweli ni kwamba Mahakama, Bunge na Serikali wanajua wanachokifanya kwa kucheza na akili za Wadanganyika ili kuendelea kuwafanya wajinga kila siku.Kwa nchi yeyote yenye kufuata utawala wa Katiba ba sheria SPIKA WA BUNGE ALITAKIWA LEO ASIMWAPISHE MTATURU mpaka kesi ya msingi itakapotolewa maamuzi. Kulikuwa na haraka gani kusubiri mpaka hiyo tarehe 9 Septemba ambayo ni wiki ijayo tu???!!!!Kuna kitu hakiko sawa hapa...!!!

Tusubiri uamuzi wa Jaji Matupa kama utakuwa kinyume na haya niliyoyasema. Na kama itatokea akafanya maamuzi kinyume na maelekezo hatutashangaa kusikia akianza kuhojiwa uraia na uzalendo wake. Time gonna tell!
Kwani mbunge akishaapishwa hawezi kutenguliwa?!!!!

Mbona Dr Abdallah Possy aliapishwa na Spika Ndugai huyu huyu na baadae ubunge wake ukatenguliwa na muhimili mwingine?!
 
Back
Top Bottom