Mahakama Kuu yafuta mashtaka 14 kati ya 25 ya Masheikh wa Uamusho

Bismillahir Rahmaanir Rahiim

SHURA YA MAIMAMU TANZANIA

LEO TAREHE 23/04/2021, MAHAKAMA KUU AMEFUTA MASHTAKA 14 YA MASHEIKH.

Mawakili wanaowatetea Masheikh wamezoa ushindi mkubwa leo Mahakani katika mapingamizi waliyoweka dhidi ya upande wa Jamhuri.

Mapingamizi hayo yalikuwa dhidi ya ukiukwaji wa sheria ulio wawezesha upande wa Jamhuri kufungua kesi nzito (Criminal Session Na. 121/3020), dhidi ya Masheikh hao.

Katika shauri hilo la Jinai Mahakama imekubaliana na hoja zilizojengwa na Mawakili hao kutoka katika katiba ya Jamhuri ya Muungano Tanzania na pia Katiba ya Zanzibar na sheria nyingine ikiwemo sheria ya Kuzuia Ugaidi.

Kwa muktadha huo Mahakama Kuu imeyafuta mashitaka 14 kati ya mashitaka 25 yanayowakabili Masheikh hao.

Mashtaka 11 yaliyobaki yataanza kusikilizwa Mahakama Kuu Dar es Salaam jumanne tarehe 27.4.2021.

Wananch mnaombwa kuwa karibu na kesi hizi ambazo zina mafundisho na mambo mengi ya kuzingatiwa.

Ibrahim Z. Mkondo
Msemaji wa Shura ya Maimamu Tanzania.
0713118812
Sawa

Sent from my Infinix X680 using JamiiForums mobile app
 
Nadhani hao mashehe wa uamsho wamejifunza mengi kwa kukaa rumande hata wakiachiwa huru leo hatutasikia tena watu wakipigwa risasi na kuuawa ovyo ovyo kama wakati ule walipoanzisha uamsho wao
Lete ushahidi
 
Kesi na kushikiliwa kws masheikh wa uamsho kunafikirisha sana (iwe Wana hatia au hawana). Iweje baada ya hao masheikh kukamatwa na kuhamishiwa Bara, Zanzibar kumekuwa shwari, yale mashambulio ya tindikali na risasi kwa wageni yamekoma kabisa.

Vv
 
Kesi na kushikiliwa kws masheikh wa uamsho kunafikirisha sana (iwe Wana hatia au hawana). Iweje baada ya hao masheikh kukamatwa na kuhamishiwa Bara, Zanzibar kumekuwa shwari, yale mashambulio ya tindikali na risasi kwa wageni yamekoma kabisa.

Vv
Ndio ujue hao watu ni hatari kwa usalama wa nchi,shein na kikwete hawakuwa wajinga kuwasweka ndani.
 
Back
Top Bottom