Mahakama Kuu yafuta mashtaka 14 kati ya 25 ya Masheikh wa Uamusho

Ibrahimu Zuberi Mkondo

Verified Member
Sep 19, 2019
33
400
Bismillahir Rahmaanir Rahiim

SHURA YA MAIMAMU TANZANIA

LEO TAREHE 23/04/2021, MAHAKAMA KUU AMEFUTA MASHTAKA 14 YA MASHEIKH.

Mawakili wanaowatetea Masheikh wamezoa ushindi mkubwa leo Mahakani katika mapingamizi waliyoweka dhidi ya upande wa Jamhuri.

Mapingamizi hayo yalikuwa dhidi ya ukiukwaji wa sheria ulio wawezesha upande wa Jamhuri kufungua kesi nzito (Criminal Session Na. 121/3020), dhidi ya Masheikh hao.

Katika shauri hilo la Jinai Mahakama imekubaliana na hoja zilizojengwa na Mawakili hao kutoka katika katiba ya Jamhuri ya Muungano Tanzania na pia Katiba ya Zanzibar na sheria nyingine ikiwemo sheria ya Kuzuia Ugaidi.

Kwa muktadha huo Mahakama Kuu imeyafuta mashitaka 14 kati ya mashitaka 25 yanayowakabili Masheikh hao.

Mashtaka 11 yaliyobaki yataanza kusikilizwa Mahakama Kuu Dar es Salaam jumanne tarehe 27.4.2021.

Wananch mnaombwa kuwa karibu na kesi hizi ambazo zina mafundisho na mambo mengi ya kuzingatiwa.

Ibrahim Z. Mkondo
Msemaji wa Shura ya Maimamu Tanzania.
0713118812
 

Attachments

  • File size
    11.7 MB
    Views
    13

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom