Mahakama Kuu yafuta kifungo cha BAWATA: Justice was delayed...

Shadow

JF-Expert Member
May 19, 2008
2,897
671
This shows that the Judiciary is trying to hold its muscles and seek its independence. But why after 10 years? Just Delayed is justice denied! Mama Tibaijuka sasa waweza rudi kuendesha chombo ulichokianzisha.


Na Claud Mshana

MAHAKAMA Kuu imetengua uamuzi wa serikali kulifungia lililokuwa Baraza la Wanawake Tanzania (Bawata) na kwamba chombo hicho sasa kitaendela kuwepo na kufanya shughuli zake kisheria.

Wakitoa hukumu hiyo, majaji watatu wa mahakama hiyo, Lauren Kalegeya, Juxon Lay na Amir Manento walisema Bawata bado inatambulika kisheria na kuongeza kuwa ipo katika katika orodha ya msajili kwa kipindi chote cha miaka 13 ya kusikilizwa kesi hiyo.

Pamoja na kutangaza uamuzi huo, mahakama hiyo pia imelipa Sh20 milioni kwa baraza hilo kama fidia ya jumla.

Mwaka 1997, serikali iliishutumu Bawata kuwa inajihisisha na shughuli za siasa na hivyo kutaka ijisajili upya ili ifanye kazi na malengo inayokusudia.

Kufungiwa kwa Bawata kulisababisha malalamiko mengi sana kwa wadau wa haki za binadamu, waliodai kuwa serikali haikufuta haki na kwamba chombo hicho hakikupewa haki ya kusikilizwa.

Mara baada ya uamuzi huo wa Mahakama Kuu, wakili aliyekuwa akiitetea Bawata ambaye pia ni mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Prof Issa Shivji alisema watu wanapaswa kuwa na imani na mahakama zetu.

"Ninafurahi hasa jinsi kesi nzima ilivyoendeshwa, jinsi vipengele mbalimbali vya sheria vilivyotafsiriwa. Hii inaonyesha ni jinsi gani mahakama zetu zilivyo mstari wa mbele katika kutetea na kulinda haki za binadamu," alisema Prof. Shivji.

Bawata iliundwa mwaka 1994 ikiwa na lengo la kuwaunganisha wanawake wa aina zote kupigania usawa wa kijinsia hasa katika mfumo wa vyama vingi nchini.



Source: Mwananchi
 
Baada ya miaka 12 ya Bawata kufutwa na serikali, bawata imshida kesi yake na hakimu kuelekeza serikali kuilipa milion 20. Vipengele vilivyotumika kuifungia bawata vimeitwa vya kikoloni na viko nje ya katiba!

Mwenye habari zaidi atupe hukumu ya kesi, na kwani iishe baada ya miaka 12?
 
Nimefarijika maana hii kesi imemsumbua sana Prof. Shivji.
Ni moja ya kesi chache ambazo ilikuwa inachallenge government excecutive orders.
Ushindi huu inamaana kubwa sana kwa watetezi wa haki za binaadamu na taasisi za kiraia kwamba hata maamuzi ya serikali kwa mujibuwa sheria waliojiwekea, yanaweza kupingwa na mahakama. Na mimi naisubiri hukumu kwa hamu.
 
Naipongeza mahakama kuu kwa kutoa uamuzi wa haki. Hii itaongeza imani ya wananchi kwa mahakama zetu kwa kuwa inaonyesha mahakama ni muhimili wa dola unaojitegemea. Inaonyesha mahakama sasa ni huru,haipendelei serikali.
 
After more than 10 years!!!! Hapa ni uonevu sana. Nakumbuka shughuli za Bawata zilienea nchi nzima na walitumia fedha nyingi sana kwa set up ya offices na matumizi mengine ambayo kwa sasa ni kuanza upya. Je hiyo damage italipwa na nani?? Itabidi Prof. Shivji afungue kesi ya madai (fidia). Twenty million ni kichekesho kuwapa, hizo ni gharama za kesi au ni kitu gani. Wanasheria hebu tusaidieni hapa.
 
mahakama kuu ya tanzania imeamauru kurejeshwa kwa usajili wa BAWATA na kwamba hatua ya kuifuta ilikuwa kinyume na sheria.

kazi nzuri ya wakili profesa shivji
 
Hivi BAWATA ndiyo nini mkuu??????? Au ulimaanisha BAKWATA???

ni Baraza la Wanawake Tanzania ambalo lilianzishwa na kina profesa tibaijuika likafutwa na serikali 30/6/97 kwa sababu wanazozijua wao
 
Mods unganisha na ile thread nyingine inazungumzia jambo hili hili with the heading "Mahakama kuu yafuta Kifungo cha Baraza la Wanawake Tanzania". thanks
 
Unajua hii BAWATA ingeachiwa kufanya kazi yake ,wanawake wangekuwa wamefika mbali sana kiharakati. Hata haya masuala ya viti maalum yangekuwa ni historia sasa hivi....wanawake wangesimama majimboni kuchuana wa wanaume..... Tatizo serikali ilipata hofu, ikijua fika kwa uwingi wa wanawake, wangesimama pamoja, ulaji wa midume milafi ungepotea.
 
Unajua hii BAWATA ingeachiwa kufanya kazi yake ,wanawake wangekuwa wamefika mbali sana kiharakati. Hata haya masuala ya viti maalum yangekuwa ni historia sasa hivi....wanawake wangesimama majimboni kuchuana wa wanaume..... Tatizo serikali ilipata hofu, ikijua fika kwa uwingi wa wanawake, wangesimama pamoja, ulaji wa midume milafi ungepotea.

Umesahau kusema ukweli au umekwepa kusema ukweli makusudi tu. Kama BAWATA ingeachiwa kufanya kazi yake leo tusingekuwa na kitu ile wanaita UWT(ile ya SISI M.) ingeshakufa na kuzikwa na wanawake wote wangekuwa kitu kimoja si kama wanavyoishi kwa hawa opportunist wanajiita UWT wakati ni wake wa vigogo tupu! Yaani baba mwenyekiti jumuiya fualni na mama mwenyekiti kwa akina mama. Wizi mtupu.:D
 
Umesahau kusema ukweli au umekwepa kusema ukweli makusudi tu. Kama BAWATA ingeachiwa kufanya kazi yake leo tusingekuwa na kitu ile wanaita UWT(ile ya SISI M.) ingeshakufa na kuzikwa na wanawake wote wangekuwa kitu kimoja si kama wanavyoishi kwa hawa opportunist wanajiita UWT wakati ni wake wa vigogo tupu! Yaani baba mwenyekiti jumuiya fualni na mama mwenyekiti kwa akina mama. Wizi mtupu.:D

Hapa umegusa kwenyewe!! UWT clearly does not represent all tanzanian women..kazi kweli kweli.
 
Naomba kusaidiwa kopi ya kesi ya BAWATA na ile ya (Deputy Prime Minister) Augustine Lyatonga Mrema V. Managing Editor of Mtanzania Newspaper & another nimeitafuta nimeshindwa kuipata
 
Ninge shangaa kama hicho chombo kisinge lipwa fidia kwa usumbufu na kupotezewa mida!

Serikali maranyingi ushindwa kujipanga na kushindwa kupeleka ushahidi wa kutosha, muda wote huo wameshindwa kuthibitisha pasi na shaka chama hicho kina jihusisha na siasa!

Well done court!
 
Back
Top Bottom