Informer
JF-Expert Member
- Jul 29, 2006
- 1,577
- 6,582
Mahakama Kuu (Dar) imebatilisha vifungu vya sheria vinavyowapa mamlaka Wakurugenzi wa Halmashauri kusimamia Uchaguzi.
Kesi hiyo namba 6 ya mwaka 2018, ilifunguliwa na Bob Wangwe dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG).
Katika kesi hiyo, Bob Chacha Wangwe aliyekuwa akiwakilishwa na Wakili Fatuma Karume, anapinga Wakurugenzi wa Halmashauri za Wilaya na Manispaa kuwa wasimamizi wa uchaguzi kwa niaba ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).
Anadai kuwa hiyo ni kinyume cha Ibara ya 74 (14 ) ya Katiba ya Nchi ambayo inapiga marufuku kwa mtu yeyote anayehusika na uchaguzi kuwa mwanachama wa chama chochote cha siasa na kwamba ana haki ya kupiga kura tu.
Aidha, alidai kuwa wakurugenzi hao ni wateule wa Rais ambaye pia ni mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM).
SHERIA INASOMEKAJE?
Mwezi Juni 2018, akiwa Bungeni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Utumishi na Utawala Bora), George Mkuchika, alisema Mbunge yeyote anayeona kuwa si sahihi Wakurugenzi wa Halmashauri kutosimamia uchaguzi, apeleke hoja Bungeni ili sheria hiyo ibadilishwe.
Mkuchika aliongeza kwa kusema “Tunayo Mahakama, pale ambapo mtu anaona hakutendewa haki aende Mahakamani,”
Ilikotoka:
LHRC, Fatma Karume, Bob Chacha Wangwe kufungua kesi kupinga makada wa chama kuteuliwa kuwa wakurugenzi wa uchaguzi
Wakili Fatma Karume na Mtoto wa aliyekuwa Mbunge Tarime, Chacha Wangwe, Bob Wangwe wamefunguka na kusema kuwa wamepanga kufungua kesi kupinga Wakurugenzi kusimamia uchaguzi nchini. Akiongea na waandishi wa habari Fatma Karume amesema kuwa Tanzania sasa baadhi ya viongozi waliwahi kusikika...
www.jamiiforums.com
Baadhi ya mijadala ndani ya JamiiForums:
2016
Hatutaki wakurugenzi wasimamie uchaguzi 2020
Tunataka tume ya taifa ya uchaguzi ijitegemee yenyewe kusimamia zoezi la uchaguzi ifikapo 2020, tume ipeleke wawakilishi wake kwa kila wilaya na sio kuweka wakurugenzi wa halmashauri na manispaa kusimamia uchaguzi kuepusha biases. Hatuwezi kua na uchaguzi huru na wa haki hata siku moja...
www.jamiiforums.com
Julai 2018:
LHRC: Asilimia 80 ya Wakurugenzi wa Halamashauri wanaopaswa kusimamia uchaguzi waliwahi kugombea uongozi kupitia CCM
Hii ni habari iliyotolewa na Mkurugenzi wa Kituoa cha Sheria na Haki za Binadamu nchini ambapo amesema taarifa hiyo ni kulingana na utafti wao walioufanya mwaka jana ambapo wengi wao waligombea nafasi mbalimbali kupitia CCM ila kura hazikutosha. Mkurugenzi huyo hakutaka kufafanya zaidi kwani...
www.jamiiforums.com
NEC wenyewe walishaona haya:
NEC yatahadharisha Wakuu wa Mikoa, Wilaya na Wakurugenzi kutojihusisha na siasa maeneo ya uchaguzi wa marudio
TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), imewaandikia barua za kuwatahadharisha wakuu wa mikoa, wilaya na wakurugenzi kutojihusisha na siasa katika maeneo yao ambayo yanafanya uchaguzi wa marudio ya ubunge. Kauli hiyo, ilitangazwa Dar es Salaam jana na Mkurugenzi wa NEC, Ramadhan Kailima, wakati wa...
www.jamiiforums.com
2016
Madhara ya kuteua makada kwenye nafasi za Ukurugenzi wa Halmashauri
UTEUZI WA WAKURUGENZI WA HALMASHAURI ZA WILAYA, MIJI, MANISPAA NA MAJIJI. Katika ngazi ya wilaya tulizoea kuona Raisi akiteua DC pekee huku nafasi zingine za makatibu tawala na wakurugenzi wakichaguliwa na watu wengine. Nafasi ya Mkurugenzi ni nafasi muhimu sana na inatakiwa kupewa kwa njia ya...
www.jamiiforums.com
2014
Uchaguzi Serikali za Mitaa: Wakurugenzi waendeleza rafu
TARIME; Muda huu tunavyowasiliana kuna sintofahamu kubwa mjini Tarime katika mitaa ya Msati highway, Iganana,Binafsi na Nyangai, ambako DED aliahirisha uchaguzi na akatangaza kwa vipaza sauti ufanyike leo Jumanne. Wananchi kwa wingi wameamkia vituoni. Hakuna kitu kinaendelea. Wamefuatilia...
www.jamiiforums.com