Mahakama Kuu yaamuru Polisi kumfikisha Mahakamani Neema Mwakipesile wa BAWACHA Agosti 12, 2021

Hivi ingetokea Polisi wamegoma kumuachia na kesho wasingeenda Mahakamani Mahakama ingekuwa na uwezo wa kuchukua hatua gani.

Nahitaji kuelewa tu.
Mahakama ipi? Na hilo tushukuru tu ni Nguvu na Neema ya Mungu wao kama wao hawana muda na mambo ya haki.
 
Polisi wenu wamemuachia HURU Bi. Neema Mwakipesile Sakalile baada ya mawakili wetu kupeleka Habeas Corpus mahakamani na kesi kupangwa tarehe 12/08/2021 (kesho) saa 03:00 asubuhi mbele ya Jaji Mgonya, Mahakama Kuu, DSM... Muda huu wamemuachia baada siku 15.. Huu ni UONEVU!

Mawakili wetu muda huu wamepata 'summons' (wito) ya kesi ya Neema Sakalile Mwakipesile. Ni case Number 156 ya mwaka 2021 imepangwa tarehe 12/08/2021 (kesho) saa 03:00 asubuhi mbele ya Mhe. Jaji Mgonya, Mahakama Kuu, DSM.

Hatua hii imekuja baada ya Mawakili wake kuripoti Mahakamani unlawful detention ya mteja wao na wakaiomba mahakama kutoa amri ya kuletwa mbele ya Mahakama. Kisheria inaitwa "Habeas corpus"
AIBU KWA SIRRO na Wahusika

Sent from my SM-J600F using JamiiForums mobile app
 
Kuna haja ya serikali kuunda tume hurusu ipitie na kukagua hali ya mahabusu zote nchini. Wakague mazingira yake yakoje pamoja na idadi ya mahabusu wanaowekwa.

Amandla....

Kwanini mahabusu tu? Hakuna anayestahili kudhalilishwa utu wake, hata kama angekuwa convicted murderer!
 
Bado nawaza kwanini CHADEMA on media ilhali iliangushwa vibaya kwenye uchaguzi Mkuu 2020 na kuambulia Jimbo Moja tu
 
Kwanini mahabusu tu? Hakuna anayestahili kudhalilishwa utu wake, hata kama angekuwa convicted murderer!
Mbona unaniwekea maneno mdomoni? Nimesema wapi kuwa kuna watu wanaostahili kudhalilika?
Kwa taarifa za wengi, jela ni afadhali kuliko mahabusu na inawezekana mahabusu ina afadhali kuliko vituo vya polisi ambavyo kisheria wanatakiwa kumweka mtu kwa muda mfupi kabla ya kumpeleka mahakamani ambako ama ataachiwa kwa dhamana au atapelekwa mahabusu.
Hali ya vituo vya polisi vingi vya polisi sio nzuri. Inabidi viboreshwe maana sio "mahabusu" peke yao wanaoathirika, hata polisi wanaofanya kazi katika mazingira yale wanaathirika.

Amandla...
 
kamwe Demokrasia ya Vurugu haikubaliki ktk nchi hii ya Tanzania.

Vyombo vyetu vya Ulinzi na usalama kamwe havito mvumilia mtu yeyote yule atakaye jifanya yeye anaijua sheria zaidi ya Jeshi la polisi.
lazima tujifunze adabu ya kuheshimu sheria zetu.

hakuna aliye juu ya sheria uwe ccm, uwe chadema au huna chama lazima uwe na adabu.

kama ange fanya mambo yake angepata usumbufu huu wa kulala mahabusu?

wakati mwengine ni kujitakia matatizo tu.
Kufanya mambo ya umma kunalipa pamoja na misukosuko yake,huyo mama yuko sawa,hata Nyerere aliwahi tiwa ndani.
 
Mbona unaniwekea maneno mdomoni? Nimesema wapi kuwa kuna watu wanaostahili kudhalilika?
Kwa taarifa za wengi, jela ni afadhali kuliko mahabusu na inawezekana mahabusu ina afadhali kuliko vituo vya polisi ambavyo kisheria wanatakiwa kumweka mtu kwa muda mfupi kabla ya kumpeleka mahakamani ambako ama ataachiwa kwa dhamana au atapelekwa mahabusu.
Hali ya vituo vya polisi vingi vya polisi sio nzuri. Inabidi viboreshwe maana sio "mahabusu" peke yao wanaoathirika, hata polisi wanaofanya kazi katika mazingira yale wanaathirika.

Amandla...

Hapana, sijakuwekea maneno mdomoni; utakuwa umeelewa vibaya. Hayo maneno yana connection ya moja kwa moja na swali nililoanza nalo.

Simulizi ambazo mimi nimewahi kuzisikia juu ya hali ilivyo kwenye magereza yetu ni heartbreaking. Prison system inahitaji decongestion strategy. Kuna wafungwa ambao sio threat kwa jamii. Hao wanaweza kutengenezewa njia mbadala ya kutumikia adhabu zao!
 
Naona nilikuelewa sivyo. Samahani. Hali kote ni mbaya sana. Advantages za prisons ni kuwa wafungwa wanatumikia kifungo na hivyo wanajua lini watatoka wakati inaelekea kwenye vituo mambo ni arbitrary tu, inategemea wameamkaje. Jela zina unataratibu wa kukaguliwa lakini sio vituo vya polisi. Unapoweka watu 70 kwenye chumba cha watu 10, sio tu kuna physical discomfort bali unawahatarisha afya zao. Aidha, vyoo na mabafua yaliyotengwa kwa ajili ya watu 10 haviwezi kuhudumia watu 70. Vilevile watu hawa ni vigumu kuwahudumia kwa chakula kwa sababu vituo vya polisi havina uwezo wa kupikia watu wote hao. Hao wanalishwa na ndugu zao kama hao ndugu wana habari na uwezo. Vinginevyo ni kuomba kwa wenzao Mbaya zaidi wengi wao hawakutakiwa kuwa humo kwa sababu walitakiwa kuachiwa au kupelekwa mahakamani.
Mimi nilistuka zaidi nilposikia msemaji wa polisi akinukuliwa kuwa alisema kuwa hali ni nzuri katika hivyo vituo!

Hiyo crisis iliyopo kwenye mahabusu za Police kwa kiasi kikubwa ni ya kujitengenezea. Police wakifuata matakwa ya sheria hilo tatizo litapungua sana, kama sio kuisha.
 
Polisi wenu wamemuachia HURU Bi. Neema Mwakipesile Sakalile baada ya mawakili wetu kupeleka Habeas Corpus mahakamani na kesi kupangwa tarehe 12/08/2021 (kesho) saa 03:00 asubuhi mbele ya Jaji Mgonya, Mahakama Kuu, DSM... Muda huu wamemuachia baada siku 15.. Huu ni UONEVU!

Mawakili wetu muda huu wamepata 'summons' (wito) ya kesi ya Neema Sakalile Mwakipesile. Ni case Number 156 ya mwaka 2021 imepangwa tarehe 12/08/2021 (kesho) saa 03:00 asubuhi mbele ya Mhe. Jaji Mgonya, Mahakama Kuu, DSM.

Hatua hii imekuja baada ya Mawakili wake kuripoti Mahakamani unlawful detention ya mteja wao na wakaiomba mahakama kutoa amri ya kuletwa mbele ya Mahakama. Kisheria inaitwa "Habeas corpus"
Utawala dhalimu na wakishetani kabisa
 
Narudia tena, tuna Jeshi la ajabu mno na linatia aibu sana sana, wamemshikilia kwa siku kibao, Mawakili wa Chadema wameenda mahakamani, Polisi wameona mambo yanakua magumu wamemuachia.

Polisi wenu wamemuachia HURU Bi. Neema Mwakipesile Sakalile baada ya mawakili wetu kupeleka Habeas Corpus mahakamani na kesi kupangwa tarehe 12/08/2021 (kesho) saa 03:00 asubuhi mbele ya Jaji Mgonya, Mahakama Kuu, DSM... Muda huu wamemuachia baada siku 15.. Huu ni UONEVU!
Polisi wakiwa wanawajibishwa na wanadaiwa fidia watajifunza kuheshimu sheria za nchi, maisha na haki za watu.
Katiba Mpya ndio jibu.
 
Hiyo crisis iliyopo kwenye mahabusu za Police kwa kiasi kikubwa ni ya kujitengenezea. Police wakifuata matakwa ya sheria hilo tatizo litapungua sana, kama sio kuisha.

Nionavyo mimi ni kuwa kuna matatizo makubwa mawili. La kwanza ndio hilo unalolizungumzia. Swali linabaki ni nani mwenye mamlaka na nia ya kuhakikisha polisi wanafuata matakwa ya kisheria maana haya malalamiko ni ya muda mrefu. Hili suala halipo kwenye ajenda yetu kwa sababu wengi wanaokumbwa nayo ni watu wasio na wakuwasemea.

Tatizo lingine ni mazingira wanayokaa "mahabusu". Humu ndani watu huwa wanafurahia wakisikia mtu anashikiliwa na polisi na wanambeza kuwa ataenda kujisaidia haja kubwa kwenye ndoo. Hii ina maana kuwa ni siri iliyo wazi kuwa selo za kwenye vituo vya polisi hazina vyoo, na kama kuna vyoo havitoshi au vina hali mbaya kutokana na kuharibika na kukosekana maji. Selo nyingi zina kunguni ambao ni dalili ya uchafu ulio kithiri. Hii hali inatakiwa iwe challenged ili wale wanaokuwa mno wawe mahali ambapo utu wao haudhalilishwi. Suala lingine ni kuwa ni muhimu sana kwa binadamu kuweza kupata jua na kunyoosha miguu yake ndio maana hata jela wafungwa wanatolewa kwenye selo na kupewa nafasi ya kuzunguka zunguka na kukaa kwenye yadi. Hilo haliwezekani kwenye vituo vya polisi. Ukisikia mtu amekaa wiki nzima kituoni, jua kwamba karibu muda wote huo amekuwa selo. Na kama selo imeshonana basi hata nafasi ya kunyoosha miguu haipo.

Hili suala lina umiza sana.

Nakubali, ni maumivu makali.
 
Neema Mwakipesile afunguka akiongea na VoA News kituo cha televisheni cha Marekani baada ya kuachiwa kutoka mahabusu ambapo alishikiliwa kwa siku 15 mfululizo

Africa 54 - Aug 18, 2021| Opposition in Tanzanian

Top Stories: When Tanzanian President Samia Suluhu Hassan took office in April, she vowed a U-turn in politics from her predecessor, the late John Magufuli.  But the arrest of opposition leader Freeman Mbowe in July has dimmed hopes that Hassan will her turn back on Magufuli's iron-fisted style of rule.  

Source : VOA Africa
 
Back
Top Bottom