sijui wanakuja au ilikuwa danganya toto.
nasijui Baba Riz1 atalonganini leo
Kenya imewafukuza madakatari waliogoma Jk fumba macho fukuza wauaji hawa
Serikali imeamua kutumia sheria ya kazi no. 6 (FORCED LABOUR)
section 6-(1) Any person procures, demands or imposes forced labour, comits an offence.
(2) For the purposes of this section, forced labour includes bonded labour or any work exacted from a person under the threat of a penalty and to which that person has not consented but does not include
a) Any work exacted under the National Defense Act, 1966 for work of a purely military character;
b) Any work that forms part of the normal civic obligations of a citizen of the United Republic of Tanzania;
c) Any work exacted from any person as a consequence of a conviction in a court of law, provided that the work is carried out under the supervision and control of a public authority and that the person is not hired to, or placed at, the disposal of private persons;
d) Any work exacted in cases of an emergency or a circumstance that would endanger the existence or the well-being of the whole or part of the population;
e) Minor Communal services performed by the members of a community in the direct interest of that community after consultation with them or their direct representatives on the need for the services.
My Take:
Ni aibu kwa Serikali kuogopa na kuona haya kukaa na madaktari kumaliza huu mgogoro kwa amani. huu ubabe wa serikali hautamaliza mgogoro zaidi ya kupalia moto. Kikwete ameshindwa kuongoza nchi.
Mar 9th 2012, 05:55
Kwa: Wahariri wote;
TV,
RADIO,
MAGAZETI,
BLOGU,
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Mahakama Kuu, Divisheni ya Kazi, leo (*Alhamisi Machi 8, 2012) *imetoa uamuzi wa kusitishwa mara moja kwa mgomo wa Madaktari ulioitishwa nchi nzima tangu jana (*Jumatano Machi 7, 2012).
Katika amri yake ya pili, Mahakama Kuu pia imekitaka Chama cha Madaktari Tanzania na Jumuiya ya Madaktari kuwatangazia wanachama wao mara moja kupitia Vyombo vya Habari kusitishwa kwa mgomo huo nchi nzima kama
walivyowatangazia wakati wanauitisha mgomo wenyewe.
Mahakama Kuu pia imeamuru pande zote mbili, yaani Serikali kwa upande mmoja na Chama cha Madaktari na Jumuiya ya Madaktari, kwa upande mwingine, kutumia fursa zilizopo katika kutatua mgogoro wa kikazi uliopo kati yao kwa
haraka.
Uamuzi huo wa Mahakama Kuu imetolewa na Jaji R.M. Rweyemamu, baada ya kusikiliza ombi la Mwanasheria Mkuu wa Serikali dhidi ya Chama cha Madaktari na Jumuiya ya Madaktari kuitaka itoe zuio kwa mgomo huo.
Akitoa uamuzi huo, Jaji Rweyemamu alisema anazingatia madhara ambayo mgomo huo ungeleta kwa jamii kwa vile huduma za tiba ambazo madaktari walitaka kugoma kuzitoa ni miongoni mwa huduma muhimu zilizotajwa kwenye Sheria ya
Ajira na Mahusiano Kazini, Namba 6 ya Mwaka 2004.
Uamuzi huo, ni kama ifuatavyo:
Leo, tarehe 8, Machi 2012, Mahakama Kuu, Divisheni ya Kazi, mbele ya Jaji R.M. Rweyemamu, baada ya kusikiliza Ombi No. 24 la 2012 lililowasilishwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (Mwombaji) dhidi ya Chama cha Madaktari Tanzania na Jumuiya ya Madaktari (Walalamikiwa), imetoa uamuzi ufuatao:
i) Chama cha Madaktari Tanzania na Jumuiya ya Madaktari pamoja na Wanachama wao, kusitisha Mgomo waliouanzisha rasmi tarehe 7 Machi 2012 nchi nzima na kurejea kazini mara moja kwa kuendelea na kazi zao kama kawaida, mara tu Amri hii itakapowafikia. Aidha, waombaji watatakiwa kutoa Kiapo cha kuthibitisha kwamba wamewasilisha Amri hiyo kwa Walalamikiwa na kuwasilisha Kiapo hicho Mahakama Kuu Divisheni ya Kazi kesho tarehe 9, Mach 2012.
ii) Mara baada ya Amri hii kuwasilishwa kwa Walalamikiwa (Chama cha Madaktari Tanzania na Jumuiya ya Madaktari) watatakiwa kuwatangazia Wanachama wao kupitia Vyombo vya Habari kusitishwa kwa Mgomo huo Nchi nzima kama walivyowatangazia wakati wa kuitisha Mgomo huo;
iii) Mahakama inaamuru pande zote mbili (Serikali na Chama cha Madaktari Tanzania pamoja na Jumuiya ya Madaktari) kutumia fursa za Kisheria zilizopo katika kutatua Mgogoro wa Kikazi uliopo kati yao kwa haraka.
(mwisho)
Imetolewa na:
Ofisi ya Waziri Mkuu,
S.L.P. 3021
DAR ES SALAAM.
Alhamisi Machi 8, 2012
Au maDaktari wagome kweli sio kimaigizo kama ilivyo sasa.Kama kina Mponda wangekuwa wanajali wananchi kweli wangejiuzulu. Lakini wanajali maslahi yao wala hawana utu.
Cha kushangaza zaidi huyo Hakimu aliyetoa hiyo Hukumu wiki ijayo nae anagoma kudai maboresho ya maslahi ya kazi yake. Nadhani wote tumeskia juu ya Mgomo wa Mahakimu jamani!
Wakipuuza amri hii halali ya mahakama itakula kwao sana tu. Nawahurumia zaidi ma-Interns ambao hata ajira rasmi hawana.Madaktari walisha resolve kugoma hata angeondoka Pinda madarakani, kwahiyo hamna jinsi ni vizuri waendelee na mgomo kwakuwa hamna tatizo ambalo halina utatuzi.