Mahakama Kuu yaamuru madaktari kusitisha mgomo

Nimesikia taarifa ya habari tbc taifa (radio ya magamba) ya saa 0:00 kwamba ma-doctor wameamrishwa na mahakama kusitishe mgomo wa kuwashinikiza waziri na naibu waziri wa afya wajiuzuru.

Hii maana yake nini?


Kipi usichokielewa hapa? mbona ulichoandika kiko wazi tu na hakina utata wowote?
 
CV ya Judge Rweyemamu, tafadhari.

Hahaha wewe umefilisika kweli kimawazo! nilitegemea utaomba nakala ya mahakama usome maamuzi ya mahakama u challenge wewe unataka CV ya Judge. Unatumia akili zako za kuzaliwa ?
 
Source : HABARI LEO ,9 -03-2012

MAHAKAMA Kuu Divisheni ya Kazi imewaagiza madaktari walioitisha mgomo nchi nzima, kuusitisha mara moja.

Mbali na kusitisha mgomo huo, madaktari hao wameagizwa kutumia vyombo vya habari ilivyotumia kutangaza mgomo huo, kuutangazia umma kwamba mgomo huo haupo tena na kwamba wanarejea kazini.

Uamuzi huo umekuja siku moja baada ya madaktari hao kuanza rasmi mgomo wao wakishinikiza kujiuzulu kwa Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Hadji Mponda na Naibu wake, Dk. Lucy Nkya, kama moja ya sharti la kuendelea na mazungumzo na Serikali juu ya
madai yao mbalimbali ya maslahi.

Uamuzi wa Mahakama hiyo ulitolewa jana usiku na Jaji Regina Rweyemamu baada ya kusikiliza maombi ya Serikali yaliyowasilishwa mahakamani hapo Jumatano na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema, kupinga mgomo huo uliotangazwa juzi na madaktari hao, kinyume cha utaratibu.

Katika maombi yaliyowasilishwa mahakamani juzi chini ya hati ya dharura, Jaji Werema, alidai kuwa mgomo huo ni hatari kwa maisha ya watu na unafanyika wakati majadiliano yameanza kati ya madaktari na Serikali na huku kukiwa na kesi Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA) ambayo haijamalizika.

Pia alidai kuwa mgomo ni batili kwa kuwa haukufuata utaratibu kwani madaktari hao wana kiapo cha taaluma yao, ambacho kinaeleza kuwa wao ni sehemu ya taaluma ambazo haziruhusiwi kugoma.

Awali, Mwanasheria Mkuu wa Serikali alifungua kesi katika Tume ya Usuluhishi na Uamuzi, Jumanne iliyopita, lakini licha ya kupelekewa hati ya kuitwa katka shauri hilo, madaktari hao hawakutokea na zaidi ya hapo wakatangaza mgomo.

Kutokana na hilo, Serikali ililazimizika kwenda Mahakama Kuu Divisheni ya Kazi chini ya hati ya dharura juzi kuiomba izuie mgomo huo.

Mbali na kugoma, Mwanasheria Mkuu wa Serikali alidai madaktari hao walikuwa na njia za kufanya kabla ya kugoma ikiwemo, kwenda Tume ya Usuluhishi na Uamuzi au kwenda katika Kamati inayoshughulika Huduma Maalumu.

Washitakiwa katika kesi hiyo ni Chama cha Madaktari (MAT) na Jumuiya ya Madaktari ambayo
Serikali inadai kuwa ni batili kwa kuwa haijasajiliwa.

Katika kesi hiyo, Serikali iliwakilishwa na Wakili Mwandamizi, Edson Mweyunge na walalamikiwa, MAT walihudhuria katika shauri hilo.
Mwishoni mwa wiki, madaktari walitangaza kuanza mgomo juzi baada ya Serikali kukataa matakwa yao ya kujiuzulu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Hadji Mponda na Naibu wake, Dk. Lucy Nkya.

Katika hatua nyingine, Rais Jakaya Kikwete leo anatarajia kuzungumza na Taifa kupitia Wazee wa Mkoa wa Dar es Salaam.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Mecky Sadiki alisema jana kwenye maadhimisho ya Siku
ya Wanawake Duniani kimkoa kuwa Rais Kikwete atazungumza na Watanzania wote kupitia wazee hao na kuwataka wafungulie vyombo vya habari kumsikiliza.

“Naomba nitoe tangazo muhimu sana, wanawake wote na Watanzania wote kwa ujumla kesho
(leo) mfungue televisheni na redio zote, mumsikilize Rais Jakaya Kikwete atazungumza na Taifa kupitia Wazee wa Dar es Salaam, tafadhali mfanye hivyo,” alitangaza Sadiki aliyekuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo ya wanawake iliyofanyika kimkoa katika Viwanja vya Mnazi
Mmoja, Dar es Salaam.

Sadiki alitoa tangazo hilo kwa msisitizo mara baada ya kuhutubia hadhara hiyo ambayo pamoja na mambo mengine, yeye (RC) alizungumzia suala la mgomo wa madaktari na kuhamasisha wanawake kushiriki katika maoni ya Katiba mpya pindi mchakato utakapoanza.

RC Sadiki alisema Rais Kikwete atazungumza na wazee hao asubuhi, lakini hakueleza atakutana nao wapi wala maudhui ya kukutana nao, ingawa imekuwa ni kawaida ya kiongozi huyo wa nchi kukutana na wazee wa mikoa mbalimbali ikiwemo ya Dar es Salaam na Dodoma na kupitia kwao, huzungumzia masuala ya kitaifa.

Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Salva Rweyemamu alipoulizwa kuhusu Rais kukutana na wazee hao wa Dar es Salaam, alisema kama Mkuu wa mkoa ametangaza hivyo, basi anukuliwe alivyosema.

Kwa sasa, suala la mgomo wa madaktari ulioanza jana nchini kote ndilo linalogonga vichwa kwa sasa na limetokea licha ya rai ya Serikali kupitia kwa Waziri Mkuu Mizengo Pinda, kuwasihi madaktari hao kutogoma kwa sababu matatizo yao yanashughuliwa.

Katika hatua nyingine, Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) na Chama cha Wafanyakazi wa Afya na Serikali Kuu (TUGHE), vimewanasihi madaktari wanaogoma na kuwataka wazingatie kiapo chao cha kuhudumia jamii na kurejea kazini.

Katibu Mkuu wa Bakwata, Shehe Suleiman Lolila, alisema jana kwamba pamoja na madaktati hao kuwa na hoja ya msingi kuhusu madai yao, jambo la msingi zaidi wangeweka maslahi ya Watanzania mbele.

“Tayari Serikali imeonesha dalili ya kuzungumza nao, kuhusu madai waliyoyawasilisha, wangetumia fursa hiyo na kurejea kazini, kwa kuwa wao bado wanabaki kuwa watu muhimu na kugoma kwao kunaweza kuleta maafa makubwa katika jamii,” alisema.

Aliwataka kuangalia kiapo chao, lakini pia kujifunza kuwa na subira wakati masuala yao yakishughulikiwa, kwani hata dini imeweka wazi kuwa mtu anapokuwa na subira hupata mafanikio na thawabu kubwa.

Katibu Mkuu wa Tughe, Ali Kiwenge, alisema mgogoro wa madaktari kwa sasa unaumiza zaidi
wananchi hasa kisaikolojia.

“Kwa sasa mtu hata ukipigiwa simu tu ukaambiwa mtoto, baba au mama anaumwa, unaanza kuwaza utafanyaje, kwa mgogoro huu nchi iko kwenye wasiwasi mkubwa bila sababu za msingi,” alisema.

Naye Katibu Mkuu wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA), Nicholaus
Mgaya, alipotakiwa kutoa maoni na ushauri wake, alisema atazungumza na vyombo vya
habari leo kuhusu mgomo huo.

Kwa upande wa hali katika hospitali nchini, Taasisi ya Tiba ya Mifupa ya Muhimbili (MOI) jana ilisitisha huduma za wagonjwa wa nje kutokana na kupungukiwa madaktari.

Ofisa Uhusiano wa MOI, Almas Jumaa, alisema katika taasisi hiyo wameathirika sana na mgomo kwani wamebaki madaktari 10 ambao ni wakuu wa vitengo na Idara kati ya madaktari 72 waliopo.

Katika hospitali nyingine za Dar es Salaam, wagonjwa walirudishwa nyumbani na kutakiwa kurudi hospitalini baada ya kusikia kwenye vyombo vya habari kuwa huduma zimerejea.

Katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, wagonjwa walikutwa wamekaa nje kwenye viti vyao
huku ndugu wakitafuta jinsi ya kuwahamishia katika hospitali zingine za binafsi.

Aidha, RC Sadiki aliwaondoa hofu madaktari wanaoendelea kutoa huduma katika hospitali za
mkoa huo, licha ya kushinikizwa wagome, na kusema Serikali itawapa ulinzi, kwa kuwa wamekuwa wakipokea vitisho.

Aliwaomba waendelee kuokoa maisha ya Watanzania wenzao, kulingana na kiapo walichokula
kwa kuwa tayari Serikali imekubali kushughulikia madai yao hivyo kugoma si ufumbuzi.
 
Waziri si mtendaji na wala si mwajiri wa hao madaktari. hawa watumishi kudai aondelewe ni kuanzisha migogoro ya ushari!

This is one of the most aoutregeous statements I have ever heard. Mahakama kuu inaingilia vipi mgomo wa madaktari? Mtoa mada, rudi shule ujifunze kuandika . Kumbukeni hawa wanagoma kudai madiliko ya kiutendaji.

Ni kweli hii serikali ya kikwete kila kitu kinawezekana. Jembe apone arudi nyumbani kuiongoza nchi
 
Hizi dalili za kutapatapa za serikali, badala ya kutumia akili kwenye utatuzi wa huu mgogoro wanaingiza ubabe na kutojali..!Acha tuone kama hiyo amri pia itahusisha kuondoka kwa Haji Mponda na mwenzake Nkya..
 
Kila mara nawaza jinsi serikali ilivyofanikiwa kutugawa mafungu, mafungu hali ambayo inapelekea kudai haki zetu kimafungu mafungu na hivyo kudhoofisha nguvu ya madai. Laiti wote tungelichukulia hili kama LETU na si la madaktari peke yao mbona sasa hivi Mponda na huyo Lucy wangekuwa historia!. Badala ya kukaa na coca na makopo ya popcon kuangalia movie au mieleka kati ya madaktari na serikali, wote tungesimama kwa sauti moja na kudai hawa wawili waondoshwe ili ndugu na jamaa zetu wapate matibabu huko mahospitalini.

Hata hao wazee wanaokutana na Rais leo, walitakiwa kugoma ili kumfanya rais aelewe ukubwa wa tatizo. Kama walikuwa wanajua hawatotekeleza matakwa yao kwa nini waliwaahidi??
 
News flash kwenye tv ilikuwa kwamba Mahakama inataka mgomo uishe mara moja,haikutaja mgomo unahusu nini.
 
Mar 9th 2012, 05:55
Kwa: Wahariri wote;
TV,
RADIO,
MAGAZETI,
BLOGU,


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Mahakama Kuu, Divisheni ya Kazi, leo (*Alhamisi Machi 8, 2012) *imetoa uamuzi wa kusitishwa mara moja kwa mgomo wa Madaktari ulioitishwa nchi nzima tangu jana (*Jumatano Machi 7, 2012).

Katika amri yake ya pili, Mahakama Kuu pia imekitaka Chama cha Madaktari Tanzania na Jumuiya ya Madaktari kuwatangazia wanachama wao mara moja kupitia Vyombo vya Habari kusitishwa kwa mgomo huo nchi nzima kama
walivyowatangazia wakati wanauitisha mgomo wenyewe.

Mahakama Kuu pia imeamuru pande zote mbili, yaani Serikali kwa upande mmoja na Chama cha Madaktari na Jumuiya ya Madaktari, kwa upande mwingine, kutumia fursa zilizopo katika kutatua mgogoro wa kikazi uliopo kati yao kwa
haraka.

Uamuzi huo wa Mahakama Kuu imetolewa na Jaji R.M. Rweyemamu, baada ya kusikiliza ombi la Mwanasheria Mkuu wa Serikali dhidi ya Chama cha Madaktari na Jumuiya ya Madaktari kuitaka itoe zuio kwa mgomo huo.

Akitoa uamuzi huo, Jaji Rweyemamu alisema anazingatia madhara ambayo mgomo huo ungeleta kwa jamii kwa vile huduma za tiba ambazo madaktari walitaka kugoma kuzitoa ni miongoni mwa huduma muhimu zilizotajwa kwenye Sheria ya
Ajira na Mahusiano Kazini, Namba 6 ya Mwaka 2004.

Uamuzi huo, ni kama ifuatavyo:

Leo, tarehe 8, Machi 2012, Mahakama Kuu, Divisheni ya Kazi, mbele ya Jaji R.M. Rweyemamu, baada ya kusikiliza Ombi No. 24 la 2012 lililowasilishwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (Mwombaji) dhidi ya Chama cha Madaktari Tanzania na Jumuiya ya Madaktari (Walalamikiwa), imetoa uamuzi ufuatao:

i) Chama cha Madaktari Tanzania na Jumuiya ya Madaktari pamoja na Wanachama wao, kusitisha Mgomo waliouanzisha rasmi tarehe 7 Machi 2012 nchi nzima na kurejea kazini mara moja kwa kuendelea na kazi zao kama kawaida, mara tu Amri hii itakapowafikia. Aidha, waombaji watatakiwa kutoa Kiapo cha kuthibitisha kwamba wamewasilisha Amri hiyo kwa Walalamikiwa na kuwasilisha Kiapo hicho Mahakama Kuu – Divisheni ya Kazi kesho tarehe 9, Mach 2012.

ii) Mara baada ya Amri hii kuwasilishwa kwa Walalamikiwa (Chama cha Madaktari Tanzania na Jumuiya ya Madaktari) watatakiwa kuwatangazia Wanachama wao kupitia Vyombo vya Habari kusitishwa kwa Mgomo huo Nchi nzima kama walivyowatangazia wakati wa kuitisha Mgomo huo;

iii) Mahakama inaamuru pande zote mbili (Serikali na Chama cha Madaktari Tanzania pamoja na Jumuiya ya Madaktari) kutumia fursa za Kisheria zilizopo katika kutatua Mgogoro wa Kikazi uliopo kati yao kwa haraka.
(mwisho)

Imetolewa na:

Ofisi ya Waziri Mkuu,
S.L.P. 3021
DAR ES SALAAM.
Alhamisi Machi 8, 2012
 
Serikali haiingilii mgomo. Serikali ina nguzo tatu. Hili jambo ni unprecedented,hii midnight announcement kutoka Mahakama Kuu.lakini there is no reason why it should not be done.Muhimu ni kwamba kutokana na shinikizo la Jamii,Mahakama Kuu haitaki kuona mgomo unaendelea,whatever the reason for the doctor's strike.
 
Migomo ipo kisheria. Wanaogoma wanapaswa kufanya hivo kwa kuzingatia sheria. MAT haipaswi kuitisha mgomo hata kama ni kwa nia njema kiasi gani. Hongera serikali yetu kwa kuzingatia utawala wa sheria. Madaktari wetu wanagoma Muhimbili unawakuta TMJ, Tumaini, Hindu Mandal,...,wakiendelea na kazi hiyo tuliowasomesha kwa kodi zetu.
 
kinachonitisha hasa ni kuwa suala hli ambalo kwa kweli ni la kisiasa lingeweza kumalizwa nje ya mahakama. Kuiingiza mahakama kwenye hili ni kutaka kuleta matatizo kwa mahakama vile vile. Hivi, madaktari wakiamua kudharau amri hiyo ya mahakama kwa sababu wanaamini siyo halali nini kitafanyika? Well, inaweza kuwasaidia serikali kufanya mambo fulani fulani "kwa sababu madaktari wamekataa amri halali ya mahakama" lakini haiwezi kufanya serikali ionekane kuwa inahoja. Kwa kukimbiliaa mahakamani imeonesha tu kuwa serikali imeshindwa hoja ya kushawishi.

Ndio uzuri mmoja wa migomo kama hii kwani hapa POlisi au FFU hawawezi kutumika. Hawawezi kwenda kwenye nyumba za madaktari na kuwaburua kwenda hospitali! Hawawezi kutumia vikosi vya jeshi kuwalazimisha madaktari kuandika tiba na kufanya uchunguzi. Njia pekee ni kuwashawishi. Sasa hata tukiassume kuwa madaktari - technically - wanarudi kazini kutii amri ya mahakama je mahakama inaweza kuwalazimisha kufanya kazi? Itakuwaje kama madaktari wote as strategic move wanaamua kurudi kazini lakini hawafanyi kazi mahakama itawaagiza nini "watibu"?

Nilikuwa njue kisa cha mgomo hasa. Hapo kwenye nyekundu umesema kweli.

Mimi sikatai kabisa madaktari kugoma. Lakini sheria za migogoro ya kazi lazima zifuatwe. Kwa bahati mbaya kabisa nchi yetu kwa sasa sheria hazifuatwi. Kila kitu kinakwenda kisiasa. Hiii inaashilia kuingizwa fujo katika nchi yetu. Mimi binafsi nasema kama kweli madaktari wanagoma kisiasa basi hilo ni kosa kubwa kabisa. Ni mbegu mbaya inapandikizwa. Wapinzani nao watakapochukua nchi basi Chama cha Magamba nacho kitajikita kwenye migomo. Nchi haitatawalika. Anayeingiza siasa katika hili haitakii mema nchi yetu.

Katika hili Serikali haina haja ya kutumia POLISI au FFU. Watawafukuza kazi madaktari waliogoma, kwa kuwasomea vifungu vya kisheria vilivyotumika kuwafukuza kazi. Kumbuka kuwa kila Daktari ni binadamu na ana mahitaji tofauti kabisa. Wengine wana watoto wanasomesha, wengine wana mikopo, wengine karibu wanastaafu. Wengi wa hawa madaktari watpiga magoti kurudi kazini. Hili nimeliona likifanyika mara nyingi hapa Tanzania na hata nchi nyingine.

Haya ni maoni yangu.
 
Achana na mahakama za china kwani zipo makini kwenye hukumu zinazo husu taifa lao. Mahakama ya tz ni mahakama ya kipuuzi au kijinga au ya kitahila ulitakiwa kusema hivyo

Hii inadhihirisha kuwa Mahakama na si mhimili unaojitegemea bali ni chombo cha serikali.
 
Leo, tarehe 8, Machi 2012, Mahakama Kuu, Divisheni ya Kazi, mbele ya Jaji R.M. Rweyemamu, baada ya kusikiliza Ombi No. 24 la 2012 lililowasilishwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (Mwombaji) dhidi ya Chama cha Madaktari Tanzania na Jumuiya ya Madaktari (Walalamikiwa), imetoa uamuzi ufuatao:

i) Chama cha Madaktari Tanzania na Jumuiya ya Madaktari pamoja na Wanachama wao, kusitisha Mgomo waliouanzisha rasmi tarehe 7 Machi 2012 nchi nzima na kurejea kazini mara moja kwa kuendelea na kazi zao kama kawaida, mara tu Amri hii itakapowafikia. Aidha, waombaji watatakiwa kutoa Kiapo cha kuthibitisha kwamba wamewasilisha Amri hiyo kwa Walalamikiwa na kuwasilisha Kiapo hicho Mahakama Kuu – Divisheni ya Kazi kesho tarehe 9, Mach 2012.

ii) Mara baada ya Amri hii kuwasilishwa kwa Walalamikiwa (Chama cha Madaktari Tanzania na Jumuiya ya Madaktari) watatakiwa kuwatangazia Wanachama wao kupitia Vyombo vya Habari kusitishwa kwa Mgomo huo Nchi nzima kama walivyowatangazia wakati wa kuitisha Mgomo huo;

iii) Mahakama inaamuru pande zote mbili (Serikali na Chama cha Madaktari Tanzania pamoja na Jumuiya ya Madaktari) kutumia fursa za Kisheria zilizopo katika kutatua Mgogoro wa Kikazi uliopo kati yao kwa haraka.

When I was a Scout Boy, tulikuwa tunafundishwa kujiandaa kwa kila saa na kwa suala lolote, na salaam yetu ilikuwa (mpaka leo) SCOUT, tunajibu BE PREPARED. Itashangaza sana kama MAT hawakuwa wamejiandaa kwa vitisho na mambo kama haya ya kutumua sheria na mahakama. Aristotle alipata kusema, "even when laws have been written down, they ought not always to remain unaltered"

I support the Doctors
 
Hakuna vitisho,hii ni warning kwa wanaoleta mgomo kwamba they are in a precarious position,and they must not presume on the sympathy of the High Court. Remember,hii ni mara ya pili unawaomba wagonjwa wawe patient.
 
Hizi dalili za kutapatapa za serikali, badala ya kutumia akili kwenye utatuzi wa huu mgogoro wanaingiza ubabe na kutojali..!Acha tuone kama hiyo amri pia itahusisha kuondoka kwa Haji Mponda na mwenzake Nkya..
Ingependeza zaidi.
 
sijui wanakuja au ilikuwa danganya toto.
nasijui Baba Riz1 atalonganini leo
 
Hakuna mtu yoyote anayeongea kuhusu watu wawili kutimuliwa,kinachozungumziwa hapa ni adha tu wanayoipata wagonjwa.
 
Nimesikia taarifa ya habari tbc taifa (radio ya magamba) ya saa 0:00 kwamba ma-doctor wameamrishwa na mahakama kusitishe mgomo wa kuwashinikiza waziri na naibu waziri wa afya wajiuzuru.

Hii maana yake nini?


Soma hapa:

[h=1]Tanzania: Court - Docs Go Back to Work[/h]9 March 2012
The Labour Division of the High Court on Thursday declared the doctors' strike illegal and ordered them back to work immediately.
High Court Judge Regina Rweyemamu also ordered the Medical Association of Tanzania (MAT), which used the mass media to call the nationwide strike, to use the same means to call off the strike.
The application for the order was filed under a certificate of urgency by the Attorney General, Judge Frederick Werema in Dar es Salaam on Wednesday, following failure of MAT to appear before the Commission for Mediation and Arbitration (CMA).
The AG had filed a case against the doctors at CMA on Tuesday. In the petition before Judge Rweyemamu, the AG submited that the ongoing strike is illegal, contrary to doctors' oath of service and endangers the lives of innocent people. The AG further stated that the MAT, which is purported to be the coordinator of the strike, has no legal status because it is not registered.
Meanwhile President Jakaya Kikwete has booked a meeting today with Dar es Salaam elders, a forum usually used to address the nation on pertinent national issues, it was learnt yesterday. The meeting comes two days after resumption of the strike by doctors, which is threatening to paralyze medical services throughout the country, but it was not immediately certain if the President would dwell on the subject.
"I have no idea what the president is going to speak about, he asked for a meeting with the Dar es Salaam elders and we have arranged it for him," the Dar es Salaam Regional Commissioner, Mr Said Meckb Sadick told the 'Daily News' yesterday.
The Director of Communications in the President's Office, Mr Salva Rweyemamu, said he had no official confirmation for the meeting but added that if the RC says it has been booked since he is an authority. Analysts said it would be a misnomer if the President held such meeting today and omitted to address the doctors' strike, which is expected to enter the third day today, despite
pleas by Prime Minister Mizengo Pinda, civil society and religious leaders.
The strike was called off early last month after Mr Pinda announced the suspension of the Permanent Secretary in the Ministry of Health, Ms Blandina Nyoni and the Chief Medical Officer, Dr Deo Mtasiwa. A committee formed to sort out the doctors' demands has submitted a report to the government, but the doctors last week walked away from negotiations coordinated y the Prime Minister's Office, arguing that they cannot sit around the same table with other medical workers.
They further gave 72 hours from last Saturday for Health Minister Dr Hadji Mponda and his deputy, Dr Lucy Nkya to resign or be sacked, failing which they would resume the strike. The demand was rejected by Mr Pinda. Some of the doctors in Dar es Salaam hospitals have ignored the strike call and continued working, but the RC said yesterday that they were receiving death threats. "They have been receiving threats through text messages.
I want to promise you that the government will use all means to protect them," he said during celebrations to mark Women's Day at Mnazi Mmoja grounds. Mr Sadick commended the doctors' decision of not joining the striking doctors, noting that they have chosen to save lives of those in need of medical services. He explained that district hospitals have made contingent arrangements to handle serious cases should Muhimbili be forced to halt services.
A random survey by 'Daily News' at MNH and Temeke Hospital yesterday established that only admitted patients and those with emergency cases received medical care. "The nurses have told us to go home because most of the doctors are on strike," a patient at MNH, Ms Aurelia Lyoka, told this paper.
The Principal Welfare and Public Relations Officer of the Muhimbili Orthopaedic Institute(MOI), Mr Jumaa Almasi, told reporters yesterday that the institute had suspended OPD services until further notice. The institute has 72 medical doctors but hardly 10 were on duty yesterday, according to the public relations officer. As a result, he said it was MOI's head of departments and other specialists that were attending to about 250 patients admitted there.
"On average, MOI receives about 100 patients in OPD per day. The good thing is that nurses and other medical staff are on duty as usual," he said. The Trade Union Congress of Tanzania (TUCTA) Secretary General, Mr Nicholaus Mgaya, said yesterday the union will today hold a press conference on the doctors' strike.

Source: allAfrica.com: Tanzania: Court - Docs Go Back to Work
Daily News Tanzania.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom