MAMA POROJO
JF-Expert Member
- Nov 22, 2007
- 4,974
- 785
Kwani mahakama ndio mwajiri wa madokta.
Mahakama ni chombo cha kutafsiri sheria ambapo itajulikana ni nani anakiuka sheria kati ya pande mbili zinazovutana.
Kwani mahakama ndio mwajiri wa madokta.
Waziri mponda mbishi, anasema mbona waziri wa ulinzi na JKT ameshakutwa na mabalaa mara nying tu, yakiwemo ya gongolamboto na mbagala, pia waziri wa mambo ya ndani, polis wake wanaua raia kila kukicha, yeye kutofautiana na madaktar imekuwa nongwa!
Uliandika vizuri sana lakini sentensi yako ya mwisho imechafua maana nzima, nimekudharau sana! hivi nchi hii yenye wakaazi zaidi ya milion 44 haina watu wengine wanoweza uongozi zaidi ya kutegemea mafisadi walishindwa kuongoza wakalazimishwa kujiuzulu, mbona kuna vijana wengi tu wenye uwezo na upeo na makini wasio na chembe za ufisadi na wizi?? Think twice before you put your rubbish here!!
Mahakama ina mamlaka gani kutoa amri kama hiyo?
Dhambi ya kuiba kura 2010 ndiyo hiyo.
Huyu aliyeleta hii topic ametumwa atest zali kama wakiingia na hiyo singo ya mahakama, madaktari watakuwa wamejipangaje?
Madaktari na nyie kama hamjajipanga na hili, hakikisheni mnakuwa hatua mbele yao. Watafuteni watu kama kina Tundu Lisu wasiohongeka ili wawashauri.
NANUKUU...
mahakama kuu kitengo cha kazi imewaamuru Madaktari kurudi kazini mara moja na kutoa ufafanuzi kuwa majadiliano ya haraka yanatakiwa kufanyika kati ya upande wa serikali na upande wa madaktari ili kuweza kumaliza tofauti zilizopo...
MWISHO WA KUNUKUU...
Mitaani kwenye vijiwe vya kahawa...Kwenye red hapo.......... mitaani wanasema mgomo una mkono wa wanasiasa wa Chama Cha Maandamano. chunga kauli zako.
kwa hapa ilipofikia ni kuwa serikali imeshindwa kufanya maamuzi pamoja na kutimiza majukumu yake.Umeona hee gwalu niaje lakini!
"mende Kaangusha kabati"this government ain't serious at all...the only open and easy solution to this matter iz to suck mponda na nkya, and not to use mahakama to intimidate doctors. very silly
Kenya imewafukuza madakatari waliogoma Jk fumba macho fukuza wauaji hawa
kinachonitisha hasa ni kuwa suala hli ambalo kwa kweli ni la kisiasa lingeweza kumalizwa nje ya mahakama. Kuiingiza mahakama kwenye hili ni kutaka kuleta matatizo kwa mahakama vile vile. Hivi, madaktari wakiamua kudharau amri hiyo ya mahakama kwa sababu wanaamini siyo halali nini kitafanyika? Well, inaweza kuwasaidia serikali kufanya mambo fulani fulani "kwa sababu madaktari wamekataa amri halali ya mahakama" lakini haiwezi kufanya serikali ionekane kuwa inahoja. Kwa kukimbiliaa mahakamani imeonesha tu kuwa serikali imeshindwa hoja ya kushawishi.
Ndio uzuri mmoja wa migomo kama hii kwani hapa POlisi au FFU hawawezi kutumika. Hawawezi kwenda kwenye nyumba za madaktari na kuwaburua kwenda hospitali! Hawawezi kutumia vikosi vya jeshi kuwalazimisha madaktari kuandika tiba na kufanya uchunguzi. Njia pekee ni kuwashawishi. Sasa hata tukiassume kuwa madaktari - technically - wanarudi kazini kutii amri ya mahakama je mahakama inaweza kuwalazimisha kufanya kazi? Itakuwaje kama madaktari wote as strategic move wanaamua kurudi kazini lakini hawafanyi kazi mahakama itawaagiza nini "watibu"?