Mahakama Kuu ya Tanzania yaamuru DOWANS kulipwa!

Glad

Member
Nov 29, 2010
25
1
Daa kumbe sakata la Dowans kulipwa bado linaendelea? nimesikia tu kwa mbali kwny taarifa ya habari ITV saa mbili hiii!! Wadau vp hii imekaaje?
Mahakama kuu ya Tanzania kupitia Jaji Emilian Mushi imeiamuru Tanesco kuilipa mabilioni ya fedha kampuni ya dowans kwa kigezo kuwa mahakama ya Tanzania haiwezi kupingana na Mahakama ya kimataifa, lakini pia mahakama imeiamuru Tanesco kulipa gharama zote za kesi hiyo ambazo bado hazijafanyiwa tathmini.
 
kwa nini usisikilize kwanza ndo ukaja na habari ya kueleweka.....uko tanzani lakini hata magazeeti husomi!!!!
 
Mahakama kuu ya Tanzania kupitia Jaji Emilian Mushi imeiamuru Tanesco kuilipa mabilioni ya fedha kampuni ya dowans kwa kigezo kuwa mahakama ya Tanzania haiwezi kupingana na Mahakama ya kimataifa, lakini pia mahakama imeiamuru Tanesco kulipa gharama zote za kesi hiyo ambazo bado hazijafanyiwa tathmini.
 
Ndugu wana JF, siko kwenye sehemu yenye mawasiliano ya uhakika na hapa nilipo mtandao unakatakata. kesi ya DOWANS iliamriwa leo, je nani mshindi?
 
Nimeamini nchi yetu ni ya Rostam Aziz anafanya anachokiamua. Wakili Fungamtama (Mfanyakazi wa Kulipwa wa Rostam) amemaliza kila kitu alichokiasisi.
 
Ndugu wana JF, siko kwenye sehemu yenye mawasiliano ya uhakika na hapa nilipo mtandao unakatakata. kesi ya DOWANS iliamriwa leo, je nani mshindi?

DOWANS walipwe bill94.. Hukumu hii imenikera sana nahic kukisa amani kabisa. Loo jamani hii country vp?
 
Sitta na Kamati ya Mwakiembe ama wajitoe serikalini kuprotest tozo hiyo kuridhiwa au wawaombe radhi Watanzania kwa kuidramatize issue hii!.
 
Jaji Mhe. Emilian Mushi, hukumu yako hii imewakandamiza Watanzania wote Maskini wa Nchi hii, kwani pamoja na sheria zenu kujifanya mnafata sana sheria, kwa hili umechemka. Wewe unajua kuwa toka utoaji wa zabuni kwa kampuni hii feki, uligumikwa na ukiukaji wa Haki za Binadamu kwa kutumia kodi ya walalahoi wa Tanzania kwa ajili ya kujinufaisha watu wachache, Au hilo hulijua?

Sasa wewe unasema sheria za Kimataifa, sisi zinatuhusu nini kwa maisha yetu? Iandike siku hii ya leo, nina uhakika utakujua kuijutia. Take My Word.
 
Wakuu tunaifahamu richmond na baadaye dowans, zilivo ingia tukatae uamuzi woote uliotolewa tusikubali kuibiwa.
 
Ccm mmeiangamiza tz mmeifanya kua shamba la bibi kila anaejisikia anakuja kujichukulia chake na kuondoka, chakutegemea ni sisi wananchi kufanya uamuzi thabiti wa kuikomboa nchi yetu ambayo imekua kama madada poa wa ohayo ambao kila mwanaume anaekuja ni halali yake, walianza richmond (richad monduli) wakajichukulia na ilivyobainika ufisadi uliokuwepo ndani yake wakawauzia dowans na serikali ya ccm ikatumia nguvu zake zote ktk kulifunika hili. Dowans nao wameka na pindi ufisadi uliokuwepo ndani yake kwa viongozi wetu kuingia mkataba ambao hata tahahira awezi ingia, baada ya serikali kuvunja mkataba dowans wamedai fidia kubwa ambayo ni mzigo kwa mtz wa hali ya chini na sasa dowans hii hii imeuzwa tena huku rais wetu akithubutu kusimama mbele ya umma na kutudanganya mmiliki wa dowans hamjui.

Ndugu zangu watz nataka niwajulishe ya kuwa tz haita jengwa na mgeni wala viongozi wetu wabadhilifu walioko madarakani bali sisi wenyewe.

Namalizia kwakusema Zambia wamethubutu kwanini sisi watanzania tushindwe?
 
Kama Tanesco waliweza kutoa milioni 50 ili watu wakanywe bia dodoma basi ni muhimu wakalipa deni hilo kwa Dowans potelea mbali hata kama ni kwa miaka 100.
 
Ni dawa chungu kumeza, lakini Dowans ilishashinda kwenye int courts, parties walikubaliana mashauri yoyote ya kimkataba yaasisiwe na kusimamiwa na tribunal za nje....

Kwaajili ya pressure za hapa na pale ndio maana tukaipinga hii hukumu locally, cha msingi kuangalia na kuupitia upya mikataba ambayo iko current, ambayo tunaweza kuirekebisha...

Yaliyopita si ndwele...
 
Huu ndiyo wakati haswa wa upinzani kuwaeleza uma wa wanaigunga vile Rostam na CCM walipotufikisha
 
Jamani huu upole wetu huu tutajaingizwa kidole machoni huku tunaangalia tu. Hili sakata toka mwanzo ni wiiiiizi mtupuu. Tulitegemea mwisho ingekuwa hivi.

Nifahamuvyo mimi hili deni tutakao lipa indirectly ni sisi watanzania na anayelipwa kimsingi ni Rostam Aziz mana ndo mwenye Power of Attoney ya kisanii sanii. Kwa kweli tukishindwa kuresist hili basi sisi ni wakupima akili, Mahakama ya kimataifa my foot!!!
 
hakuna huruma..ushabiki wenu na akina sitta ndo umewafikiasha hapo..tanesko lipa hiyo hela
 
jaji msaaafu wa mahakama kuu aliisha sema japo jina lake nimelisahau lakini naamini wana jf wenzangu mtalikumbuka alisema amewahi kuhukumu kesi japo hakuitaja kwa shinikizo za wanasiasa itakuwa hii ya dowans? huyo hakimu kashurutishwa kuamua hivyo ni pamoja na njaa yake.

CCM imeamua kunywea kwa rostam azizi na ccm inajua ufahamu wa watz waliowengi uko chini wengi mikoani na vijijini hawajui hata kinachoendelea nchi za majirani zetu kesho tu wangekuwa barabarani masikini watz kwanza kwa umeme upi hadi tulipishwe???ama kweli mtaji wa kutawala ccm ni ujinga wa watz.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom