Mahakama kuu Tanzania yaamuru IPTL ifilisiwe | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mahakama kuu Tanzania yaamuru IPTL ifilisiwe

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Bado Niponipo, Jul 20, 2011.

 1. Bado Niponipo

  Bado Niponipo JF-Expert Member

  #1
  Jul 20, 2011
  Joined: Aug 15, 2008
  Messages: 680
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Je baada ya kufilisiwa itapelekwa wapi, na je vipi kuhusu zile 10MW inazozalisha sasa?

  Mahakama yaamuru IPTL ifilisiwe

  MAHAKAMA Kuu Tanzania imetoa amri ya kuifilisi Kampuni ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL).

  Mahakama imeagiza kuwa, kazi hiyo ya kuifilisi IPTL ifanywe na mfilisi wa kampuni hiyo ambaye ni Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA).

  Uamuzi huo ulitolewa rasmi wiki iliyopita na Jaji wa mahakama hiyo, Semistocles Kaijage katika kesi ya madai namba 254 ya mwaka 2003 iliyofunguliwa na kampuni ya Vip Engineering and Marketing Ltd dhidi ya IPTL, Mechmar Corporation (Malaysia) Berhad na Mfilisi.

  Jaji Kaijage alisema, kutokana na ombi lililowasilishwa na Kampuni ya Vip Engineering and Marketing Ltd ambaye ni mmoja wa mshirika wa IPTL Februari 25, mwaka 2002 na baada ya kuwasikia mawakili wake kwa njia ya maandishi na ombi hilo kuchapishwa kwenye Gazeti la Serikali Oktoba 10, mwaka 2003, aliamuru kampuni hiyo ifilisiwe.

  Mawakili wa Vip Engineering and Marketing Ltd ni pamoja na Michael Ngalo wa Kampuni ya Mawakili ya Ngalo and Company, Respicius Didace wa Kampuni ya Mawakili ya Didace and Company na Dosca Baregu kutoka Kampuni ya Mawakili ya Mutabuzi & Company.

  “Mahakama hii inaamuru ifilisiwe kwa mujibu wa kanuni na kazi hiyo ifanywe na mfilisi anayeshughulika na masuala ya IPTL,” alisema Jaji Kaijage.

  Aidha, aliamuru mfilisi huyo ambaye ni Rita kwa kushirikiana na wadau wa IPTL kutumia kampuni inayotambulika katika shughuli za ukaguzi wa umma kuchunguza mali za IPTL, madeni yake na kama kuna tuhuma za rushwa na kisha kutoa ripoti hiyo kwa Mahakama Kuu.

  Akizungumza na blog hii jana, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Rita, Philip Saliboko alikiri kuwa Mahakama imewaagiza kuifilisi Rita, lakini bado wakala hao hawajapokea barua ya maagizo hayo rasmi kutoka Mahakama Kuu na kwamba, wanasubiri.

  “Ni kweli sisi kama wafilisi wa IPTL tumetakiwa tufanye kazi hiyo ya kuifililisi lakini kwa sasa hatujaanza hatua yeyote kwa kuwa bado hatujapata taarifa rasmi za maagizo kutoka Mahakama Kuu,” alisema.

  Alisema, iwapo watapatiwa barua na maagizo hayo rasmi, wataanza kwanza na kujitangaza kwenye vyombo vya habari ili wale wote wanaoidai au kudaiwa na IPTL wajitokeze wakiwa na ushahidi wao kwa Rita ambapo pia watatangaza zabuni kwa kampuni itakayochunguza kila kitu kuanzia gharama, madeni na madai ya IPTL.
   
 2. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #2
  Jul 20, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,641
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  itabidi waboreshe afu tatizo la umeme lipungue..
   
 3. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #3
  Jul 20, 2011
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Mshtaki ni nani?
   
 4. l

  lebabu11 JF-Expert Member

  #4
  Jul 20, 2011
  Joined: Mar 27, 2010
  Messages: 1,650
  Likes Received: 517
  Trophy Points: 280
  Life span ya plant kama IPTL ni miaka 20 hadi 25. Kwa sasa efficiency na value ya IPTL inashuka na miaka iliyobaki ni kati ya 5 hadi 10 unlless ifanyiwe major rehabilitation ambayo gharama itakuwa zaidi ya nusu ya kujenga kiwanda kipay kama hicho!
   
 5. l

  lebabu11 JF-Expert Member

  #5
  Jul 20, 2011
  Joined: Mar 27, 2010
  Messages: 1,650
  Likes Received: 517
  Trophy Points: 280
  Life span ya plant kama IPTL ni miaka 20 hadi 25. Kwa sasa efficiency na value ya IPTL inashuka na miaka iliyobaki ni kati ya 5 hadi 10 unlless ifanyiwe major rehabilitation ambayo gharama itakuwa zaidi ya nusu ya kujenga kiwanda kipya kama hicho!
   
 6. Zing

  Zing JF-Expert Member

  #6
  Jul 20, 2011
  Joined: Jun 24, 2009
  Messages: 1,780
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0
  hi habari sio ya kisisasa Ilitakiwa ikae kwenye jukwaa la biashara au Sheria.

  But nifahamisheni Je una habri zilinipta .

  Kwa nini au nini kimesababisha ifilisiwe.
  • Ni matatio kati ya share holders
  • Ni mtatizo ya kufilisika kwa kampuni mama huko malysia
  • au ni itu gani?
  wataaalam nijuzeni?
   
Loading...