Mahakama Kuu Tanzania imeamuru Jamhuri kurudisha fedha za faini za kesi ya Freeman Mbowe na wenzake 7 wa CHADEMA

Hahahaaa siku zote haki itakulinda.....huyu mama naanza kumsoma sasa...tulichelewa kumpata..jiwe alikua anatufukia walah
Mkuu Mama yupo vizuri sana tena sana.

Apewe muda tu. Na ndio maana tunasisitiza kwamba mama aachwe afanye kazi na neema zitapatikana kwa kila mmoja wetu
 
Hii ndio namna pekee ya kuwafanya polisi was Tanzania kufanya kazi kwa kutumia vichwa vyao sio matumbo yao, kila watakapokuwa wanafanya madudu kama haya na mahakama kutenda haki na kisha serikali kulipishwa fidia watakoma uonevu.
 
Naweza nkapingana na wewe mkuu.

Huoni kama hili linadhihirisha kwamba kumbe anaehitajika ni kiongozi muadilifu tu?? Kupitia katiba hii hii mbona haki zinapatikana??

Najaribu tu kujenga hoja na wala sio kwamba napinga katiba mpya movement
Sio kwel, vp huyo kiongozi akifa au akitoka madarakani?, ila kikuwa na katiba bora kna kuwa na miongozo thabiti itayom-guide huyo kiongoz na co kufanya hisan km sasa
 
viongozi utawala wa magu walimuangusha ila sidhani kama ni yeye alipiga hizo hela ,
 
.... Mama ana kazi sio ya kitoto; kuirudisha nchi kwenye mstari sahihi wa utawala bora ana kibarua kigumu sana. Huyu sasa ndiye wa kumwombea kweli kweli Mungu amjalie afya ya mwili, hekima na busara za kuwaongoza watu wake. Kila atokapo, aingiapo, na kila atendalo likapate kibali toka Kiti cha Enzi.
Namuunga mkono mama na ninamwombea mema milele
 
Kwanini ulikubali kuchangia (kama ulitoa mchango kweli)??
MasterP,

kukaa sero wakati unandugu wa kukuchangia ili utoke sero...! Wananchi tuliitika wito, na kwa heshima ya Mbowe, ki ukweli nilichangia, sasa zinaporudishwa tena, basi akumbuke kuturudishia tu basi...! siyo tena eti zikajenge ofis, inabidi atuulize tuliochanga tukubali, kwa mfano kama mimi, mimi ni CCM, Pesa yangu kwenda kujenga ofsi ya chama kingine, sikubali, lakini endapo Mtanzania yeyote akiwa kwenye mateso, nipo radhi kuchanga chochote ili atoke kwenye hayo mateso ila sio kuchangia chama
 
Kwahiyo ulichanga ya nini wakati ilikuwa hiari na watu walitoa kama msaada
Mkuu, nilichanga kumchangia Mtanzania mwenzangu ili atoke kwenye mateso hayo na si vingine, zinaporudi, pesa yangu sikubali ikajenge jengo la chama tena, hiyo hayakuwa malengo yangu
 
Kwani Mwendazake alikuwepo mahakamani wakati akina Mbowe na wenzake wanahukumiwa? Hakimu alikuwa ni Mwendazake?

Na leo hii hakimu ni Rais Samia?
Hukumu ilitolewa kwa kumwangalia kiranja mkuu..
Katika utawala ule waliibuka watesi na wakitaka kumrrifdhisha mkubwa.
Sasa walau haki inatamalaki. Angalia uchaguzi wababe walifanya watakavyo na hawakukemewa ili mradi waliibeba ccm. Ndivyo mkubwa alivyotaka na waovu walitumia nafasi hiyo kudhulumu.
Sasa tuna mtu mwema.
 
MasterP,

kukaa sero wakati unandugu wa kukuchangia ili utoke sero...! Wananchi tuliitika wito, na kwa heshima ya Mbowe, ki ukweli nilichangia, sasa zinaporudishwa tena, basi akumbuke kuturudishia tu basi...! siyo tena eti zikajenge ofis, inabidi atuulize tuliochanga tukubali, kwa mfano kama mimi, mimi ni CCM, Pesa yangu kwenda kujenga ofsi ya chama kingine, sikubali, lakini endapo Mtanzania yeyote akiwa kwenye mateso, nipo radhi kuchanga chochote ili atoke kwenye hayo mateso ila sio kuchangia chama
Tuliochanga kwa moyo mmoja kutokana na udhalimu wa yule mwovu, kwa moyo radhi kabisa, tunatamka kuwa pesa hiyo ni yao tuliowachangia. Ni kifuta machozi kwa mateso waliyopitia, na fursa walizozipoteza kwa kuwekwa ndani na yule mwovu shetani.
 
1624641176639.png
 
.... Mama ana kazi sio ya kitoto; kuirudisha nchi kwenye mstari sahihi wa utawala bora ana kibarua kigumu sana. Huyu sasa ndiye wa kumwombea kweli kweli Mungu amjalie afya ya mwili, hekima na busara za kuwaongoza watu wake. Kila atokapo, aingiapo, na kila atendalo likapate kibali toka Kiti cha Enzi.
Hakika. Huyu ndio anafaa kuombewa sana ili atuvushe, maana anaupiga mwingi sana kuweka mambo sawa pale palipokuwa pamepinda
 
Mahakama Kuu, imebatilisha hukumu ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ya kesi ya Jinai iliyokuwa ikimkabili Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na wenzake 7 na kuamuru warejeshewe fedha walizolipa kama faini, kiasi cha Sh.350 milioni. Uamuzi huo umetolewa leo na Jaji Irvin Mgeta.

====

Alipokuwa akisoma mashitaka hayo February 22, 2018, Wakili wa Serikali Mwandamizi, Faraja Nchimbi alidai mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri kuwa ,washitakiwa kwa pamoja walitenda makosa hayo Februari 16, mwaka 2018 maeneo ya Viwanja vya Buibui na Barabara ya Kawawa, Mkwajuni wilayani Kinondoni, Dar es Salaam.

Katika mashitaka ya kwanza la kula njama: Kwa pamoja inadaiwa Februari Mosi na 16, 2018, Dar es Salaam, walikula njama pamoja na wenzao ambao hawapo mahakamani, ya kutenda kosa la kufanya mkusanyiko usio halali, mkusanyiko wenye ghasia na kukiuka tamko kutawanyika.

Inadaiwa kuwa Februari 16,2018 katika ya Viwanja vya Buibui na Mwananyamala Kinondoni, washtakiwa hao wakiwa wamekusanyika na azma ya pamoja waliitekeleza, walifanya mkusanyiko usio halali na kusababisha watu waogope na kusababisha uvunjïfu wa amani.

Katika mashitaka ya tatu, Washitakiwa hao wanadaiwa kuwa Februari 16,2018 katika viwanja vya Buibui Mwananyamala na Barabara ya Kawawa Kinondoni, kwa pamoja na wenzao 12 ambao hawapo mahakamani, walitekeleza mkusanyiko ama maandamano yasiyo halali wakiwa na lengo la kuvamia ofisi ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni na kuĺeta hofu ya uvunjifu wa amani.

Nchimbi alidai kuwa Februari 16,2018 katika Barabara ya Kawawa Kinondoni Mkwajuni, washtakiwa hao wakiwa na wenzao 12 ambao hawapo mahakamani walikiuka tamko la kuwataka kutawanyika la Ofisa wa Polisi, Gerald Ngiichi kwa kugoma kutawanyika na kupelekea uvunjifu wa amani, ambao ulisababisha hofu na hatimaye kifo cha Akwilina na majeruhi kwa askari wawili ambao ni H.7856 PC Fikiri na E.6976 CPL Rahim Msangi.

Katika mashitaka ya tano, linamkabili Mbowe ambalo ni la kuhamasisha chuki inadaiwa kuwa Februari 16, 2018 katika viwanja vya Buibui wilayani Kinondoni, Dar es Salaam, Mbowe wakati akihutubia wananchi wa jimbo hilo, alihamasisha chuki isivyo halali kwa kutoa matamshi yafuatayo “Ninapozungumza hapa kiongozi wetu wa Kata ya Kinondoni Hananasif yupo mochwari..amekamatwa na makada wa CCM kwa msaada wa vyombo vya ulinzi na usalama...wamemnyonga wamemuua.

Halafu sisi tunaona ni jambo la kawaida...tunacheka na polisi...tunacheka na CCM” Nchimbi alidai kuwa maneno hayo, yalikuwa na lengo la kuamsha hisia za chuki miongoni mwa Watanzania.

Katika mashtaka ya sita, Mbowe anadaiwa kuwa Februari 16, 2018 katika mkutano wa umma uliofanyika viwanja vya Buibui wilayani Kinondoni Dar es Salaam, Mbowe alitamka maneno yafuatayo “Tumejipa kibali cha kutangulia mbele ya haki...haiwezekani wanaume wazima na akili zetu na wake zetu na watoto wetu tukafanywa ndondocha..hiii ni nchi ya ajabu. Mimi leo nipo hapa kulinda taifa...kule Afrika Kusini Jacob Zuma amelazimishwa kujiuzulu...Robert Mugabe wa Zimbabwe kang’olewa, kang’olewa Waziri Mkuu wa Ethiopia...juzi ameondoka kwa People’s Power. Magufuli ni mwepesi kama karatasi”.

Nchimbi alidai kuwa maneno hayo, yalikuwa ya kuinua hali ya kutoridhika miongoni mwa watanzania dhidi ya serikali halali iliyopo Mdee anadaiwa kuwa Februari 16,2018 akiwahutubia wakazi wa Kinondoni alitamka kuwa “Sihitaji kuwasïmuĺia madhila yanayomkumba kila mmoja wetu kutokana na utawala wa awamu ya tano... tunamba kesho tukamchinje Magufuli na vibaraka wake wote...kama mbwai na iwe mbwai”.

Nchimbi alidai kuwa maneno hayo, yalikuwa na lengo kuhamasisha hisia za chuki miongoni mwa watanzania.

Katika mashtaka ya nane, la kuhamasisha hali ya kutoridhika, Heche anadaiwa kuwa Februari 16,2018 katika Viwanja vya Buibui alitamka kuwa “Kesho patachimbika, upumbavu ambao unafanywa kwenye nchi hii... wizi unaofanywa na serikali ya awamu ya tano...watu wanapotea...watu wanauawa wanaokotwa kwenye mitaro lazima ukome..”.

Nchimbi alidai kuwa maneno hayo, yalikuwa na lengo kuamsha hali ya kutoridhika miongoni mwa watanzania dhidi ya utawala uĺiopo madarakani. Katika mashtaka ya tisa ya uchochezi wa uasi, linalomkabili Mbowe, anadaiwa kuwa Februari 16,2018 katika maeneo hayo, alihutubia mkutano wa hadhara, alitamka maneno kuwa

“Ninaongoza mapambano nchi hii kwasababu tumechoka kuuawa...matokeo ya watanzania mia watakaokufa wataleta haki katika taifa hili. Wangapi wapo tayari kuchukua bei hiyo.” Nchimbi alidai kuwa maneno hayo, yalikuwa na nia ya kuleta chuki na hali ya manung’uniko miongoni mwa jamii dhidi ya utawala ulïopo madarakani.

Katika mashitaka ya 10 ya uchochezi wa uasi, linalomkabili tena Mbowe anadaiwa kuwa Februari 16,2018 katika maeneo hayo mkoani Dar es Salaam, Mbowe alitoa matamshi ya kupandikiza chuki na dharau kwa upande wa raia wa Tanzania dhidi ya mamlaka halali kuwa “Hii nchi inadharaulika...imejengewa misingi wa uwoga, kwa lugha nyingine wanaume ni kama mademu, si unawaona hao wanavaa suruali, waoga, bure kabisa...juzi ametekwa kijana wetu wanasema yupo mochwari, haki ya Mungu ingekuwa nchi nyingine Kinondoni ingekuwa majivu...

Lissu amepigwa risasi machine gun na vyombo vya dola...watanzania mnarudi nyuma...kuna mwandishi wa habari leo ana siku 86 amebebwa na vyombo vya dola... suluhu ya nchi hii haipi bungeni. Suluhu ya nchi jii ipo kwa wananchi wenyewe...

lakini ili tupate suluhu hiyo, ni lazima tukubali kubeba majeneza...Inawezekana leo mnaogopa kufa...Ni bora tuwabebe wachache hata wakiwa 200 waliokufa katika ukombozi ili hatimaye nchi hii isimame kama nchi ya wanaume wengine katika dunia hii” Mbowe pia anadaiwa kuwa alishawishi wakazi wa Kinondoni, kutenda kosa la kufanya maandamano na mkusanyiko usio halali.

Katika mashitaka ya 12 ya kushawishi utendaji wa kosa la jinai, linalomkabili mshtakiwa wa pili Msigwa, katika maeneo hayo hayo, Msigwa anadaiwa kushawishi raia na wakazi wa eneo hilo, kutenda kosa la jinai, kwa kutembea mbele ya umma wakiwa na silaha

Mashtaka ya 13 ambayo yanamkabili mshtakiwa, Ester Bulaya anadaiwa kuwa Februari 16, mwaka huu katika Viwanja vya Buibui wilayani Kinondoni, Dar es Salaam alïtenda kosa la kukaïdi amri halaĺi ya tamko.

HUKUMU

Mahakama yawakuta na hatia washtakiwa kwenye mashtaka 12 kati ya 13

Hakimu Simba alisema maneno haya yaliyotamkwa na Mbowe kwenye kampeni ni ya uchochezi ''Nchi imedharaurika,kwa lugha nyingine wanaume tunaonekana kama mademu,Lissu amepigwa risasi na vyombo vya dola watanzania mko kimya,ili tupate haki nchi hii Lazima tubebe majeneza''

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu iliwatia hatiani washtakiwa wote katika mashtaka 12, isipokuwa shtaka la kwanza ambalo ni kula njama ambalo limefutwa na Mahakama. Ndugu wa washtakiwa waanza kuangua vilio ndani ya Mahakama.

UPDATE: Wakili Kibatala aomba washtakiwa kulipa faini

Wakili Kibatala alimwomba Hakimu kutoa hukumu ya washtakiwa walipe faini badala ya kuwapa adhabu ya kifungo baada ya washtakiwa wote kukutwa na Hatia kwenye makosa 12 kati ya makosa 13 yaliyokuwa yanawakabili.

ADHABU
Baada ya kuwatia hatiani washtakiwa kwa makosa 12, Mahakama ilitoa adhabu kama ifuatavyo;

Hakimu: Madai ya kesi ya Akwilina hapa haipo. Isipokuwa maelezo yaliyopo hapa ni kwamba hali ile ilisababisha kuuawa kwa mtu anayeitwa Akwilina. Siwezi sema Akwilina alikufa maana sina ripoti ya daktari inayothibitisha hilo. Suala la Akwilina siwezi kulizungumzia na siligusii kabisa.

Shtaka la 2: Mahakama iliamuru washtakiwa kulipa faini ya Tsh. Milioni 10 au kwenda gerezani miezi mitano

Shtaka la 3: Mahakama iliamuru washtakiwa kulipa faini ya Tsh. Milioni 10

Shtaka la 4: Mahakama iliamuru washtakiwa kulipa faini ya Tsh. Milioni 10

Shtaka la 5: Mahakama iliamuru Freeman Mbowe kulipa faini ya Tsh. milioni 10

Shtaka la 6: Mahakama iliamuru Freeman Mbowe kulipa faini ya Tsh. million 10

Shtaka la 7: Mahakama iliamuru Halima Mdee kulipa faini ya Tsh. milioni 10

Shtaka la 8: Mahakama iliamuru John Heche kulipa faini ya Tsh. millioni 10

Shtaka la 9: Mahakama iliamuru Freeman Mbowe kulipa faini ya Tsh. milioni 5

Shtaka la 10: Mahakama iliamuru Freeman Mbowe kulipa faini ya Tsh. milioni 5

Shtaka la 11: Mahakama iliamuru Freeman Mbowe kulipa faini ya Tsh. million 10

Shtaka la 12: Mahakama iliamuru Peter Msigwa kulipa faini ya Tsh. million 10

Shtaka la 13: Mahakama iliamuru Ester Bulaya kulipa faini ya Tsh. milioni 10

JUMLA YA KIASI CHA FAINI ALICHOTAKIWA KULIPA KILA MSHTAKIWA
John Mnyika - Tsh. milioni 30
Salum Mwalimu - Tsh. milioni 30
Ester Matiko - Tsh. milioni 30
Vincent Mashinji - Tsh. milioni 30
John Heche - Tsh. milioni 40
Peter Msigwa - Tsh. milioni 40
Halima Mdee - Tsh. milioni 40
Ester Bulaya - Tsh. milioni 40
Freeman Mbowe - Tsh. milioni 70

Mahakama iLIsema endapo washtakiwa wakishindwa kulipa faini, wataenda gerezani kwa miezi mitano kwa kila kosa. Wote Walilipa faini na kuachiwa Huru.

Zaidi,soma:

1). Mbowe na viongozi 6 wa CHADEMA wafikishwa Mahakamani Kisutu, wasomewa mashitaka 8, wanyimwa dhamana hadi Machi 29

2). Mahakama ya Kisutu imewatia hatiani Viongozi wa CHADEMA na kuwahukumu kulipa faini ya Tsh. Milioni 350 au kwenda jela, Wapelekwa Segerea
Aliyewahukumu kwa uonevu na kuchukua hela zao kafa.
Waliohukumiwa bado wanaishi na hela zao wanarudishiwa.

Damu ya binti yetu Akwilina isingeweza kupotea hivi hivi.

Kweli wahenga hawakukosea waliposema "He who pursues an innocent chicken often stumbles....and most likely collapses for keeps"
 
Back
Top Bottom