Mahakama Kuu Mtwara yatupilia mbali ombi la kupitiwa (judicial review) kwa Kanuni za Maudhui Mtandaoni 2018

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,746
11,876
Mtwara: Mahakama Kuu kanda ya Mtwara leo tarehe 9.01.2019 imetoa uamuzi katika kesi ya kupinga Kanuni za Maudhui Mtandaoni iliyofunguliwa na Baraza la Habari Tanzania, Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu na Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, TCRA na Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo.

Katika shauri hilo jaji Ndyasobera amesema Waziri alienda mbali na mamlaka aliyonayo nayo kisheria kutunga kanuni hizo lakini hiyo haimaanishi kwamba Kanuni hizo ni batili.

Aidha Jaji amesema kuwa Waziri alienda kinyume na Sheria mama ya Mawasiliano juu ya maana ya neno Maudhui. Hivyo katika hukumu hiyo jaji Ndyansobera ametoa amri kwamba neno Maudhui kama lilivyowekwa kwenye Kanuni za Maudhui limekiuka sheria mama na hivyo ameamuru liondolewe.

Upande wa waleta maombi wameonesha wazi nia yao ya kukata rufaa dhidi ya uamuzi huo kwa kile walichodai kuwa yapo mambo ya msingi waliyotaka ufafanuzi wa mahakama lakini hayakugusiwa kwenye uamuzi huo.

"MAHAKAMA IMETUPILIA MBALI"

MOSI: Judicial review in kitendo cha mahakama kuingilia maamuzi yaliyofanywa na vyombo vya maamuzi ama mamlaka fulani kwenye suala la umma.

PILI: Mahakama kuu masjala ndogo (District Registry) Mtwara imesema WAZIRI ALIENDA NJE YA MAMLAKA YAKE" imeamuru neno "MAUDHUI" ....... Mkuu mbona kama tayari Mahakama imeshaingilia (judicial intervention/judicial review) na kutoa maelekezo kuhusu suala hilo?.

TAMATI: ndo kutokana na kiasi/namna ambavyo mahakama imeingilia na kuagiza wadai hawakuridhika.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom