Kididimo
JF-Expert Member
- Sep 20, 2016
- 4,017
- 3,656
Hivi karibuni Mamlaka za juu nchini ziliafiki ombi la Waziri wa Afya wa Kenya juu ya ajira ya madaktari wetu. Madaktari hawa wa Tanzania walikuwa waajiriwe Kenya kuziba pengo la Madaktari wenzao wa Kenya waliogoma. Chama cha Madaktari Tanzania (MAT) kilipinga hatua ya kuruhusu madaktari wetu kwenda Kenya kwa sababu kadhaa. Moja ya sababu ni usalama wao kuwa mdogo. Wadau mbalimbali nao walipinga kuwa wasiende kwani waliogoma walikuwa na haki za msingi wanazodai. Hata hivyo,uongozi wa juu wa Serikali yetu,uliziba masikio ,na kuendelea na maandalizi vijana wetu waende! Kwa kitendo cha jana Mahakama Kuu Kenya kuzuia wasiende,tumejifunza nini?
1. Ni walazimishaji mambo?
2. Uongozi wetu wa juu nchini,hauwaamini Watanzania waliotoa maoni yao kuwa wasiende?
3. Nani alaumiwe endapo mahakama isingezuia,na wakaenda,wakadhurika?
Tupeane ushauri ili,tusijeaibika tena mbeleni kama ilivyotokea!