Mahakama kuu kanda ya dar es salaam kutoa maamuzi juu ya pingamizi la dowans. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mahakama kuu kanda ya dar es salaam kutoa maamuzi juu ya pingamizi la dowans.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Jan 30, 2012.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Jan 30, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145

  January 28 2012

  Na Grace Ndossa

  MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam, imesema itatoa uamuzi wa pingamizi lililowasilishwa na Kampuni ya Dowans la kuitaka mahakama hiyo isiwape Tanesco kibali cha kukataa rufaa Febuari 16 mwaka huu .

  Amri hiyo ilitolewa mahakamani hapo jana na Jaji Fauz Twalib ambapo alieleza kuwa hawawezi kusikiliza kesi hiyo leo kwani Wakili wa Kampuni ya Dowans Bw. Kennedy Fungamtama ameshawasilisha pingamizi.

  Pingamizi hilo la Dowans l;inahusu kupinga Tanesco wasipewe kibali kwani hukumu iliyotolewa hawawezi kukata rufaa kutokana na makubaliano waliyokubaliana kwenye mkataba.

  Jaji Twaib alidai kuwa hataweza kusikiliza kesi hiyo hadi hapo watakaposikiliza pingamizi lilowasilishwa na Kampuni Dowans.

  Awali baada ya hukumu kutolewa na mahakam kuu Tanesco iliwasilisha maombi yao kuomba kibali cha kukata rufaa kupinga hukumu iliyotolewa na Jaji Mushi ya kuitaka tanesco kusajili tuzo ya fidia ya sh bilioni 94 ya kampuni ya Dowans mahakama hiyo kwa njia ya maandishi

  Kesi hiyo ambayo ilifunguliwa na wakili wa Dowans,Bw. Kennedy Fungamtama kwa ajili ya kuiomba mahakama hiyo iiweze kuisajili tuzo waliyoipewa Novemba 15 mwaka juzi na Mahakama ya Kimataifa na Usuluhishi wa Migogoro ya Biashara(ICC)   
 2. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #2
  Jan 30, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Mahakama kuu inasubiri nini? ni miaka mingapi inasema itatoa maamuzi?

  Our Court System is a Joke...
   
 3. BabuK

  BabuK JF-Expert Member

  #3
  Jan 30, 2012
  Joined: Jul 30, 2008
  Messages: 1,847
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 145
  ..Tanzania Nakupenda...... Haki yangu naililia.....
   
 4. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #4
  Jan 31, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Hata Mimi nakupenda Tanzania; Siwapendi Viongozi woote wa Sasa Wanasafiri Wanatuliza Matumbo Yao na Watoto Wao

  Kwanini Hawaijali Tanzania ninayokupenda kwa Moyo wangu Wote?
   
 5. EMT

  EMT JF-Expert Member

  #5
  Jan 31, 2012
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 14,464
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  This appeal is unnecessary, costly and time consuming. The Court of Appeal will not reverse the ruling of the High Court because it does not lightly entertain appeals from arbitration awards. It is in the interests of international commerce that arbitration awards should be final, and it is to be hoped that the Court of Appeal will not only strongly support this policy but also ensure that Tanzania complies with the international agreements on the enforcement of arbitral awards to which it has ratified.
   
 6. EMT

  EMT JF-Expert Member

  #6
  Jan 31, 2012
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 14,464
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  Rufaa ikubaliwe au ikataliwe na mahakama ipi?
   
Loading...