Mahakama Kuu imewaruhusu Halima Mdee na wenzake 18 kufungua kesi ya kupinga CHADEMA kuwavua uanachama

Quinine

JF-Expert Member
Jul 26, 2010
21,271
47,269
#HABARI MAHAKAMA Kuu imewaruhusu wabunge 19 wa Viti Maalum kufungua kesi ya kupinga kuvuliwa uanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)./bit.ly/3OUFVbx

==========

Mahakama Kuu imewaruhusu waliokuwa wanachama wa CHADEMA, Halma Mdee na wenzake 18 kufungua shauri la kupinga uamuzi wa chama hicho kuwavua uanachama.

Mahakama hiyo imetoa ruhusa hiyo kwa kina Mdee leo Ijumaa Julai 8, 2022, baada ya kukubaliana na hoja za maombi yao ya ridhaa ya kufungua shauri hilo la kupinga kuvuliwa uanachama.

Maombi hayo ya kina Mdee yalisikilizwa na Jaji Mustapha Ismail Juni 30 mwaka huu na CHADEMA kupitia kwa jopo la mawakili wao linaloongozwa na Peter Kibatala, walipinga hoja za mawakili wa kina Mdee kuwa hazikidhi matakwa ya kisheria kupewa ruhusa hiyo

Hata hivyo Jaji Ismail katika uamuzi wake leo amekubaliana na vigezo na hoja zote za kina Mdee, zilizowasilishwa na mawakili wao, Ipilinga Panya, Aliko Mwamanenge, Edson Kilatu na Emmanuel Ukashu.

Kwa uamuzi huo sasa kina Mdee wanatakiwa kufungua shauri lao hilo ndani ya siku 14 kuanzia leo.

Covid19.jpg
 
Huyo jaji ndie aliahirisha huo uamuzi last time ili akapewe maelezo ya kuikanyaga haki.

Hii kesi kuanzia mwanzo imeshaonekana kuna external force inatumika kuwalinda hao wanawake 19, hivyo sitashangaa kama wakishinda hiyo kesi yao licha ya Chadema kufuata taratibu zote kuwavua uanachama.

Vinginevyo inaweza kucheleweshwa mpaka 2025 huku muda huo wakiendelea kuwepo bungeni wanakula posho, Samia wa maridhiano hajawahi kuwa serious kwenye hii issue.
 
Yule mama aliekuwa kwenye clip akishangilia nadhani analia saa hii.

Ngoja iungurume kesi tujuwe nani aliandika ile barua.
 
Timu gaidi kwisha habari yao

Safi.sana Mdee waonyeshe kazi mpaka Joyce Mukya akome kupewa ubunge wa kupanua mapaja.
Kweli kabisa Hata yule ALIYETOLEWA GEREZANI USIKU MNENE tutamjua aliyemtoa
 
#HABARI MAHAKAMA Kuu imewaruhusu wabunge 19 wa Viti Maalum kufungua kesi ya kupinga kuvuliwa uanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)./bit.ly/3OUFVbx

==========

Mahakama Kuu imewaruhusu waliokuwa wanachama wa CHADEMA, Halma Mdee na wenzake 18 kufungua shauri la kupinga uamuzi wa chama hicho kuwavua uanachama.

Mahakama hiyo imetoa ruhusa hiyo kwa kina Mdee leo Ijumaa Julai 8, 2022, baada ya kukubaliana na hoja za maombi yao ya ridhaa ya kufungua shauri hilo la kupinga kuvuliwa uanachama.

Maombi hayo ya kina Mdee yalisikilizwa na Jaji Mustapha Ismail Juni 30 mwaka huu na CHADEMA kupitia kwa jopo la mawakili wao linaloongozwa na Peter Kibatala, walipinga hoja za mawakili wa kina Mdee kuwa hazikidhi matakwa ya kisheria kupewa ruhusa hiyo

Hata hivyo Jaji Ismail katika uamuzi wake leo amekubaliana na vigezo na hoja zote za kina Mdee, zilizowasilishwa na mawakili wao, Ipilinga Panya, Aliko Mwamanenge, Edson Kilatu na Emmanuel Ukashu.

Kwa uamuzi huo sasa kina Mdee wanatakiwa kufungua shauri lao hilo ndani ya siku 14 kuanzia leo.

Tuliposema kuwa hawa watakuwepo Bungeni hadi 2025 ili Kuilinda Kauli ya Kimakosa ya Madam Spika Ackson na pia kuonyesha kuwa Serikali ya CCM chini ya Rais Samia inajali Wapinzani na kwamba kuna Demokrasia nchini hadi Bungeni mlikuwa hamjatuelewa Waona Mbali tuliobarikiwa?

Kitakachofanyika just to buy time na waendelee kuwepo Bungeni ni kwamba hii Kesi itapigwa Danadana / Kalenda kila mara ili mradi tu ifike na wafike hadi hiyo 2025.
 
Back
Top Bottom