Mahakama Kuu imetupilia mbali leo maombi ya dhamana ya Yusuf Manji

K

kirerenya

JF-Expert Member
Joined
Aug 27, 2013
Messages
1,692
Points
2,000
K

kirerenya

JF-Expert Member
Joined Aug 27, 2013
1,692 2,000
manji-jpg.560213


Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam leo imeyatupilia mbali maombi ya dhamana yaliyowasilishwa na Mfanyabiashara maarufu nchini, Yusuf Manji baada ya kukubaliana na mapingamizi yaliyowasilishwa na DPP.

Maombi hayo yametupiliwa mbali na Jaji Isaya Arufani. Kabla ya kutupiliwa mbali, maombi hayo, Manji alisimama na kuieleza mahakama kukataa kuwakilishwa na Wakili Peter Kibatala kwa sababu za kisiasa. Amedai, alipopeleka maombi ya dhamana alimpa maelekezo wakili Joseph Tedayo lakini alishangaa kesi ilipofika mahakamani hapo kwa ajili ya kisikilizwa maombi yake ya dhamana wakili Kibatala ndiyo alifika kumuwakilisha.

Kutokana na hayo, Manji ameiomba Mahakama mawakili, Alex Mgongolwa, Hudson Ndusyepo na Seni Malimi ndio wawe wanamuwakilisha katika maombi hayo

Hivyo DPP akiwakilishwa na mawikili Paul Kadushi na Simon Wankyo walidai kuwa, wamewasilisha kiapo kinzani kupinga maombi hayo ya dhamana wakiwa na hoja tatu. Hoja hizo ni kuwa, Mahakama Kuu haina mamlaka ya kusikiliza maombi hayo ya dhamana na kwamba yanapaswa kusikilizwa na mahakama ya kifisadi kwa kuwa mshtakiwa anakabiliwa na makosa ya uhujumu uchumi.

Ameongeza kuwa vifungu vya kisheria vilivyotumika kuleta maombi hayo siyo sahihi na pia hati ya kiapo iliyoambatanishwa kuunga mkono maombi hayo ina dosari kisheria ambazo haziwezi kurekebishika.
Kadushi aliiomba mahakama kusikiliza kwanza mapingamizi ya DPP kabla ya kuanza kusikiliza maombi ya dhamana. Hata hivyo Wakili Mgongolwa akiwakilisha jopo la mawakili wa Manji walikubaliana na mapingamizi ya DPP kuwa ni kweli yana msingi na maombi ya dhamana yanadosari. Kufuatia kukiri huko, Kadushi aliiomba mahakama kutupilia mbali maombi hayo ya dhamana.

Akitoa uamuzi, Jaji Arufani amekubaliana na mleta Maombi (Manji) kuwa hawakilishwi na Kibatala. Pia amesema mahakama kuu haina mamlaka ya kusikiliza maombi hayo hivyo ameyatupilia mbali.

Katika maombi hayo ya dhamana, Yusuf Manji anaiomba Mahakama Kuu itengue hati ya kunyimwa dhamana iliyowasilishwa na Mkurgenzi wa Mashtaka (DPP) kwa kuwa ana matatizo ya kiafya akisumbuliwa na matatizo ya moyo.

Kwa mujibu wa hati ya maombi hayo, Manji anadai kuwa anasumbuliwa na maradhi ya moyo na kwamba ameambatanisha vyeti vya daktari katika maombi yake.

Katika kesi ya msingi, Manji na wenzake wanatuhumiwa kukutwa na mihuri mbalimbali ya JWTZ isilivyo halali vyote vikiwa na thamani ya Sh. milioni 236.5.
Mbali na Manji, washtakiwa wengine ni, Ofisa Rasilimaliwatu Deogratias Kisinda (28), Mtunza Stoo, Abdallah Sangey (46) na Mtunza Stoo msaidizi, Thobias Fwele (43)

Mfanyabiashara Yusuf Manji akiwa anatoka Mahakama kuu mara baada ya mahakama hiyo kutupilia mbali maombi ya dhamana yaliyowasilishwa na mfanyabiashara huyo.
 

Attachments:

Wervemarcel

Wervemarcel

JF-Expert Member
Joined
Apr 10, 2015
Messages
2,037
Points
2,000
Wervemarcel

Wervemarcel

JF-Expert Member
Joined Apr 10, 2015
2,037 2,000
Maskini Manji!
Rostam Aziz Hakutakiwa
Kukuacha Uandamwe Na
Visasi Vya Hali Hii.
Hata Iqbal Na Yale Magorofa
Aliamua Kuvuka Ng'ambo Kuliko
Kubaki Japo Alisaidia Kutoa Ajira 2000 . Sasa Majengo Yake Yanakuwa Magofu Dah!
Kwaajili Ya Conflict Of Interest.
My Take
Pambana Na Hali Yako Manji.
 
Lambardi

Lambardi

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2008
Messages
10,485
Points
2,000
Lambardi

Lambardi

JF-Expert Member
Joined Feb 7, 2008
10,485 2,000
Pole sana Manji.......ndio maisha hayooo!!!!
 
MKWEPA KODI

MKWEPA KODI

JF-Expert Member
Joined
Nov 28, 2015
Messages
26,299
Points
2,000
MKWEPA KODI

MKWEPA KODI

JF-Expert Member
Joined Nov 28, 2015
26,299 2,000
gwa myetu

gwa myetu

JF-Expert Member
Joined
Aug 18, 2014
Messages
4,389
Points
2,000
gwa myetu

gwa myetu

JF-Expert Member
Joined Aug 18, 2014
4,389 2,000
Poleni wana Yanga , angekuwa diwani wa chadema ungeona team Lumumba wanavyotoa mapovu kwamba kata ya Mbagala haina mwakilishi hadi sasa, na nyinyi wanaMbagala ndo mkome kuchagua pesa badala ya mtu
 
A

Adili

JF-Expert Member
Joined
Nov 3, 2007
Messages
3,019
Points
2,000
A

Adili

JF-Expert Member
Joined Nov 3, 2007
3,019 2,000
Hiyo inaitwa jaza ujazwe,manji alimfanyia mkulu kitu mbaya enzi za JK sasa mkulu nae zamu yake kulipa kisasi

Hizi ndizo siasa zetu za kiafrica
Kila siku anakumbusha watu kumuombea wakati yeye ni jino kwa mawili.
 

Forum statistics

Threads 1,315,991
Members 505,466
Posts 31,875,972
Top