Mahakama Kuu imetoa kibali kuchunguzwa wizi wa fedha za ruzuku ya CUF

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,898
THE CIVIC UNITED FRONT
(CUF - Chama Cha Wananchi)

TAARIFA KWA UMMA NA VYOMBO VYA HABARI

TAREHE: 3 MARCH, 2019

 BAADA YA MAHAKAMA KUU KUTOA AMRI YA KUZUIA KUFANYIKA KWA MKUTANO MKUU FEKI WA LIPUMBA NA GENGE LAKE.

 MAHAKAMA KUU PIA IMETOA KIBALI KUCHUNGUZA WIZI WA FEDHA ZA RUZUKU YA CUF, USHAHIDI NA VIELELEZO KUTOLEWA MAHAKAMANI:

 BODI YA WADHAMINI YA CUF YAFUNGUA MASHAURI MAPYA NAMBA 2/2019 NA NAMBA 7/2019 DHIDI YA MSAJILI WA VYAMA VYA SIASA NA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI:

 BODI INAOMBA AMRI YA MAHAKAMA (PREROGATIVE ORDERS OF PROHIBITION) KUMZUIA MSAJILI KUENDELEZA WIZI WA FEDHA ZA RUZUKU YA CUF:

 BODI INAOMBA AMRI YA MAHAKAMA YA SHURTI (PREROGATIVE ORDERS OF MANDAMUS) KUMTAKA MSAJILI AWEKE FEDHA YA RUZUKU YA CUF KATIKA AKAUNTI MAALUM YA RUZUKU INAYOTAMBULIWA NA KUMILIKIWA NA BODI HALALI YA WADHAMINI YA CUF:

Tarehe 22/2/2019 na Tarehe 27/2/2019 THE REGISTERED TRUSTEES OF THE CIVIC UNITED FRONT (CUF-Chama cha Wananchi) imefungua mashauri mawili kwa hati ya dharura yote yakihusiana na FEDHA ZA RUZUKU YA CUF. Kwanza ni shauri la msingi Miscellaneous Civil Cause No. 2/2019 na la pili ni shauri dogo Miscellaneous Application No. 7/2019. Mashauri hayo yalifunguliwa Mahakama Kuu ya Tanzania Masjala Kuu ya Dar es salaam, na yamepangwa kutajwa kwa mara ya kwanza siku Tarehe 14/3/2019 mbele ya Mheshimiwa Jaji Firmin Nyanda Matogolo.

Kufunguliwa kwa mashauri hayo kunatokana na Bodi halali ya Wadhamini ya THE CIVIC UNITED FRONT (CUF- Chama cha Wananchi) kupewa kibali (leave) kuwasilisha maombi rasmi ya amri za shurti (prerogative orders of mandamus) kumtaka Msajili kuweka Ruzuku ya CUF katika akaunti iliyoidhinishwa na Bodi halali ya Chama, pia amri za kumzuia (prerogative orders of prohibition) Msajili kuendelea kumpatia Lipumba na genge lake Ruzuku ya CUF-Chama cha Wananchi, kinyume cha Katiba ya CUF, Sheria na taratibu za masuala ya fedha. Mashauri haya yanategemewa kuhitimisha suala la nani mwenye uhalali wa kupokea Ruzuku ya CUF kwa mujibu wa Sheria.

Itakumbukwa kuwa licha ya Msajili wa Vyama vya Siasa Francis Katabazi Mutungi kuendelea kushikilia msimamo wake kuwa hatoi fedha za Ruzuku kwa Lipumba, lakini kwa kumbukumbu zilizopo na za kuthibitika hadi kufikia Tarehe 20/1/2018 alikwisha mpatia Lipumba jumla ya Tshs. 1,076,982,032.12 (Bilioni moja na milioni sabini na sita) kupitia akaunti ya Wilaya ya CUF Temeke No. 2072300456 ya tawi la Benki ya NMB Temeke. Tawi la Benki ya NMB Temeke limekuwa likishiriki katika utakatishaji wa fedha za wizi wa Ruzuku ya CUF licha ya Bodi ya Wadhamini ya CUF kuziandikia barua Bank zote nchini kusitisha utowaji wa huduma kupitia akaunti zote zenye jina la CUF-Chama cha Wananchi na kutoidhinisha ufunguwaji wa akaunti mpya kwa jina la Chama.

Taarifa hiyo ya Bodi ilifuatiwa na amri tatu za zuio za Mahakama Kuu (Court Injunction Orders). Benki ya NMB imekaidi mambo yote mawili na ilimruhusu Lipumba kufungua akaunti mpya katika tawi lake Zanzibar ili kumwezesha kutoroshea fedha huko kipindi cha zuio la Mahakama. Hata hivyo baada ya Bodi ya Wadhamini ya CUF kuigundua akaunti hiyo Msajili alishindwa kuitumia badala yake akaendelea kutumia Akaunti ya tawi la Temeke.

Kutokana na uchafu uliofanywa na Mutungi, Msajili wa Vyama vya Siasa na Ofisi yake dhidi ya CUF, mara zote amekuwa akienda mbio kuhakikisha kuwa Lipumba na genge lake wanaitisha Mkutano Mkuu FEKI ili kuchagua viongozi wapya wa CUF wakidhani kuwa kwa kufanya hivyo itakuwa ndio manusura ya kuficha madudu mengi machafu waliyoyafanya dhidi ya CUF ikiwemo wizi wa Fedha za Ruzuku.

TUKUTANE MAHAKAMA KUU TAREHE 14/3/2019 NA TAREHE 18/3/2019

HAKI SAWA KWA WOTE

Imetolewa na Kurugenzi ya Habari CUF-Taifa

SALIM BIMANI,
MKURUGENZI WA HABARI,
+255777 414112 / +255655 314112

MBARALA MAHARAGANDE,
NAIBU MKURUGENZI WA HABARI

maharagande@gmail.com
+255715 062577
+255767 062577
FB_IMG_1551605141672.jpg
FB_IMG_1551605134825.jpg
FB_IMG_1551605128529.jpg
FB_IMG_1551605119277.jpg
 
Mkuu Mwanahabari Huru umehamia CUF au ndio ile spirit ya UKAWA? Sijaona taarifa ya UKAWA ama CHADEMA kuhusu mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA kukihama Chama. Nasikia mjumbe huyo/mwanachama huyo alikuwa muhimu sana kiasi kwamba Mwenyekiti wa Chama alikuwa akikimbia kwenda kumfungulia mlango wa gari ili ashuke toka garini japo mjumbe huyo alikuwa na mlinzi. Toa taarifa mkuu tufahamu faida ama madhara ya kuondoka kwa mjumbe hiyo.
 
Back
Top Bottom