Mahakama Kuu iliwakataa hawa watu, Mahakama ya Rufaa ikarudisha kwa rufaa ya Mwanasheria Mkuu. Hivi Mwanasheria Mkuu ana jicho kali la kisheria?

Mwanamayu

JF-Expert Member
May 7, 2010
10,302
2,000
Kesi ilifunguliwa mahakama kuu kukataa wakurugenzi wa halmashauri ambao ni wateule wa Rais na baadhi yao wakiwa makada wa CCM kuwa wasimamizi wa uchaguzi mkuu. Mahakama kuu iliona kuwa hawana sifa ya kuwa wasimamizi. Mwanasheria mkuu wa serikali alikata rufaa kwa madai kuwa wanakula kiapo, hivyo hakuna tatizo la kisheria, lakini sasa tunaona matatizo ya hoa jamaa kuwa wasimamizi wa uchaguzi.

Kwa mujibu video (angalia hapo chini), sasa huyo bwana 'kala' kiapo halafu inaonekana alipoenda uhani wote tunajua kinachotokea huko (kiapo kiko kwenye shimo la maji taka) ndio maana hajatekeleza maagizo ya tume, na hajafanywa lolote na tume hiyo.

Maswali: 1. hivi huyu mwanasheria mkuu kweli kaiva kisheria na kuzingatia maadili ya taaluma yake? Shangazi anaweza kutusaidia kwenye hili. 2. hivi hii mahakama kuu kwa nini inawaangusha sana watanzania kwenye masuala ya demokrasia; mfano, suala la mgombea binafsi? Hivi kwa nini mahakama kuu inaona mambo kwa weledi kwenye masuala ya demokrasia kuliko mahakama ya rufani? 3. je, sio kwamba huyo jamaa anatetea gari zuri la ofisi na mshahara mnono, ikiwezekana na cheo kukubwa zaidi? 4. hivi na hii sio hongo?

 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom