Mahakama Kuu Dodoma: Joshua Nassari ashindwa kesi yake ya kuvuliwa ubunge

Kama sio mbinu chafu basi muda utasema..

Sent from my iPhone using Tapatalk
Hivi kweli kaka unaweza kutofika kazini week 1 bila taarifa yoyote. Yaani alishindwa kumuandikia barua Spika wa bunge? Alishindwa kwenda bungeni mara 1 kutoa taarifa.?

Ni ujinga kujifanya kaonewa. Huyu kauza ubonge wake.

Sent using my Nokia Torch
 
Ndio maana nikasema ukweli haujifichi kaka

Sent from my iPhone using Tapatalk
 
safi....kiburi na kujazwa upepo kutamshinda AJIFUNZE kunyenyekea anapokosea.
 
Taarifa za hivi punde kutoka Mahakama Kuu Kanda ya Dodoma ni kuwa, Joshua Nassari ameshindwa katika Shauri alilofungua Dhidi ya Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano na Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya kupinga kuvuliwa Ubunge.

Kesi hiyo ambayo uamuzi wake umetolewa leo katika hatua ya mapingamizi yaliyowasilishwa na upande wa Serikali kupitia Wakili Mkuu wa Serikali imefikia mwisho katika hatua ya Mapingamizi.

Mahakama imefuta kesi hiyo na hivyo, Nassari sio Mbunge tena.

-------
Jaji Mansour ametumia dakika 44 kusoma maelezo yaliyomweka katika wakati mgumu Nassari.

Machi 14, 2019 Ndugai aliiandikia Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) barua akiieleza kuwa Nassari amepoteza sifa ya kuwa mbunge baada ya kutohudhuria mikutano mitatu mfululizo bila kutoa taarifa.

Spika Ndugai aliitaja mikutano hiyo kuwa ni wa 12 ulioanza Septemba 4 hadi 14; Novemba 6 hadi 16, 2018 na wa Januari 29 hadi 9.

Baada ya uamuzi huo, mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe alisema amemuagiza Nassari kuzungumza na wananchi na wanachama wa jimbo lake kuwaeleza kilichotokea.

Akisoma uamuzi wake leo Ijumaa Machi 29, 2019 Jaji huyo ametumia kifungu cha 5 (4) kuwa Nassari alipaswa kupeleka malalamiko yake kwa Katibu wa bunge wala si kama alivyofanya.

Kifungu kingine kilichombana Nassari ni cha kanuni ya 146 (2) kwamba alijifukuzisha mwenyewe kwa kutohudhuria vikao vitatu mfululizo vya Bunge bila taarifa.

Mawakili wa Serikali, Alesia Mbuya, Masunga Kamuhanda na Pius Mboya walipangua hoja za wakili wa utetezi, Fred Kalonga aliyekuwa akipinga kuwa mbunge huyo alifukuzwa bila utaratibu hivyo kuitaka Tume ya Uchaguzi (NEC) isitangaze jimbo kuwa wazi.

Nje ya Mahakama Nassari amesema hakuna dhahabu nzuri isiyopita kwenye moto na kubainisha kuwa alishakoswa risasi iliyompiga mbwa wake, alinusurika ajali ya ndege na kwamba hili la ubunge halimtishi

Chanzo: Mwananchi
Mbona kama kuna pre judgement hapa au mimi ndio sifahamu sheria au mwandishi hujaelezea kwa kina?!
Kwamba kesi ilikuwa kwenye pingamizi la awari sio? Sasajaji anaingiaje kwenye kuongelea contents za main case badala ya Ku deal na hoja za pingamizi?!
Jaji akisema Nassari alifukuzwa kihalali wakati ndio ilikuwa hoja ya msingi, anakuwa ametumia ushahidi gani kufikia hii conclusion??
 
ni sawa tu waondolewe wote wapinzani wasiojielewa ili wabaki wachache maana mpaka sasa wapinzani wengi hawajielewi halafu wanailalamikia serikali inawaonea kumbe wenyewe hawajitambui.
 
Nna mashaka sana na huyu kijana mwenzangu.anatafuta kujikosha tu wakati hata ukimuangalia alipoongea na waandishi body language unaisoma vizuri tu kuwa anaficha vitu.
Kabisaa.Kashindwa kesi kirahis namna hiyoo??
Hakuna hata kukata rufaa
 
Huyo mtoto asitake kujifanya Mjanja wakati kashachukua pesa ya ccm. Anadhani akienda mahakamani ndio atatuhadaa kwamba hajachukua pesa ya ccm?
kashauriwa na gwiji la sheria Tanzania Professor Tundu Antipas Lissu. Hawa wabunge wa Tanzania wote akili zao si nzuri wawe wa CCM ama wa Upinzani. Uliona wapi wabunge wanazira bunge na kutoka nje huku wamefunga midomo na vitambaa vyeusi ni Tanzania peke yake.

EFF ya Malema kule sotuh africa ni kuwatoa ni mbinde hapa wanakuwa kama wanawake changudoa na wanashangiliwa na wananchi wa nchi ya mitandaoni ikiongozwa na raia namba moja Salary Slip na BAK. Ifike wakati huu ujinga wa kuwachekea wanasiasa sababu tu hatumpendi ama tunampenda JIWE uishe.

Hawa ndiyo wapinzani wanataka kieleweke hapo hapo

Linganisha na hawa mashoga wenu wakiongozwa na shoga wa ukweli James Mbatia

... katika wajinga Nassary yumo! Katika mazingira ya kisiasa yaliyopo huwezi kufanya upumbavu kama ule. Ila kwa upande mwingine inaweza kuwa ni well organized trick ya Nassary "kujivua" ubunge.

Absolutely, it is...!!

Mimi nilisema tangu mwanzo wa sakata hili kuwa, huyu ndugu hamna kitu, anachezea akili za watu tu...

Hivi hatujiliulizi ni kwa nini hata chama chake hakimtetei na ni kama hakipo pamoja naye?

Ni kwa nini wabunge wenzake, ukiachilia Lijualikali hawamtetei, wamemwacha peke yake?

Ni kwanini chama chake (M/kiti ambaye pia ni KUB na Katibu mkuu wake wa chama) hawakuwa hata na taarifa juu ya kuuguliwa kwake na mkewe?

That was a planned move!!
 
Mbona kama kuna pre judgement hapa au mimi ndio sifahamu sheria au mwandishi hujaelezea kwa kina?!
Kwamba kesi ilikuwa kwenye pingamizi la awari sio? Sasajaji anaingiaje kwenye kuongelea contents za main case badala ya Ku deal na hoja za pingamizi?!
Jaji akisema Nassari alifukuzwa kihalali wakati ndio ilikuwa hoja ya msingi, anakuwa ametumia ushahidi gani kufikia hii conclusion??
Nasari alipeleka ombi la kutaka kumshitaki spika kwamba alimvua ubunge kimakosa.
Serekali ikaweka pingamizi. Kwamba hakuna haja ya kushtaki kwani spika alitumia taratibu za kisheria

Sent using Jamii Forums mobile app
 
tapatalk_1553873360781.jpeg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
kashauriwa na gwiji la sheria Tanzania Professor Tundu Antipas Lissu. Hawa wabunge wa Tanzania wote akili zao si nzuri wawe wa CCM ama wa Upinzani. Uliona wapi wabunge wanazira bunge na kutoka nje huku wamefunga midomo na vitambaa vyeusi ni Tanzania peke yake.

EFF ya Malema kule sotuh africa ni kuwatoa ni mbinde hapa wanakuwa kama wanawake changudoa na wanashangiliwa na wananchi wa nchi ya mitandaoni ikiongozwa na raia namba moja Salary Slip na BAK. Ifike wakati huu ujinga wa kuwachekea wanasiasa sababu tu hatumpendi ama tunampenda JIWE uishe.

Hawa ndiyo wapinzani wanataka kieleweke hapo hapo

Linganisha na hawa mashoga wenu wakiongozwa na shoga wa ukweli James Mbatia

Umeona askari hapo wakiingilia? Huku kwetu askari huwa wanaingia na mbwa.
 
Si ndiyo saafi kuuonyesha ulimwengu? halafu mkuu mimi nimeweka na ushahidi wakitoka nje na wewe ingekua nzuri zaidi kama ungeonyesha wanavyoshurutishwa na mbwa kutoka nje.
 
Sina harddisk ya kutunza hayo matukio na mimi Sikai na Hansard za bunge, lakini hayo ni matukio yaliyotokea. Hata mwaka jana Ufaransa ndio walibeba kombe la dunia lakini sina hata picha moja kudhibitisha hilo kama ndio lengo lako. Ila nyuzi zenye matukio ya wapinzani kutolewa nje na polisi na mbwa juu zipo humuhunu jukwaani.
 
Back
Top Bottom