Mahakama Kuu Dodoma: Joshua Nassari ashindwa kesi yake ya kuvuliwa ubunge

Tindikali Kali

JF-Expert Member
Jan 9, 2018
531
500
alishakoswa risasi iliyompiga mbwa wake
Kwa wale ambao hamna kumbukumbu
IMG-20171203-WA0015.jpg
 

Tumbo Tumbo

JF-Expert Member
Sep 10, 2018
1,282
2,000
It;s so sad fikiria mnavyotumia muda wenu kumpigania mtu wenu mtaa kwa mtaa kipindi cha kura mnakesha kuzilinda leo anashindwa kuthamini utu na juhudi zenu, kasahau taabu na mashaka yote. waana sitaka kwenye foleni ya kupiga kura tena. Haya nenda kauguze mkeo,
The Application Is Incompetent and Unmaintainable and ts dismissed WITH COST'S

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Mama Amon

JF-Expert Member
Mar 30, 2018
1,105
2,000
Taarifa za hivi punde kutoka Mahakama Kuu Kanda ya Dodoma ni kuwa, Joshua Nassari ameshindwa katika Shauri alilofungua Dhidi ya Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano na Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya kupinga kuvuliwa Ubunge.

Kesi hiyo ambayo uamuzi wake umetolewa leo katika hatua ya mapingamizi yaliyowasilishwa na upande wa Serikali kupitia Wakili Mkuu wa Serikali imefikia mwisho katika hatua ya Mapingamizi.

Mahakama imefuta kesi hiyo na hivyo, Nassari sio Mbunge tena.
.
Tumekupata.

Lakini stori haijakamilika.

Tujuze haya:

1. Mapingamizi ni yapi?

2. Uamuzi wa mahakama ni upi kwa kila pingamizi?

3. Nassari amesema nini baada ya hukumu?
 

ntamaholo

JF-Expert Member
Aug 30, 2011
12,455
2,000
Taarifa za hivi punde kutoka Mahakama Kuu Kanda ya Dodoma ni kuwa, Joshua Nassari ameshindwa katika Shauri alilofungua Dhidi ya Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano na Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya kupinga kuvuliwa Ubunge.

Kesi hiyo ambayo uamuzi wake umetolewa leo katika hatua ya mapingamizi yaliyowasilishwa na upande wa Serikali kupitia Wakili Mkuu wa Serikali imefikia mwisho katika hatua ya Mapingamizi.

Mahakama imefuta kesi hiyo na hivyo, Nassari sio Mbunge tena.

-------
Jaji Mansour ametumia dakika 44 kusoma maelezo yaliyomweka katika wakati mgumu Nassari.

Machi 14, 2019 Ndugai aliiandikia Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) barua akiieleza kuwa Nassari amepoteza sifa ya kuwa mbunge baada ya kutohudhuria mikutano mitatu mfululizo bila kutoa taarifa.

Spika Ndugai aliitaja mikutano hiyo kuwa ni wa 12 ulioanza Septemba 4 hadi 14; Novemba 6 hadi 16, 2018 na wa Januari 29 hadi 9.

Baada ya uamuzi huo, mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe alisema amemuagiza Nassari kuzungumza na wananchi na wanachama wa jimbo lake kuwaeleza kilichotokea.

Akisoma uamuzi wake leo Ijumaa Machi 29, 2019 Jaji huyo ametumia kifungu cha 5 (4) kuwa Nassari alipaswa kupeleka malalamiko yake kwa Katibu wa bunge wala si kama alivyofanya.

Kifungu kingine kilichombana Nassari ni cha kanuni ya 146 (2) kwamba alijifukuzisha mwenyewe kwa kutohudhuria vikao vitatu mfululizo vya Bunge bila taarifa.

Mawakili wa Serikali, Alesia Mbuya, Masunga Kamuhanda na Pius Mboya walipangua hoja za wakili wa utetezi, Fred Kalonga aliyekuwa akipinga kuwa mbunge huyo alifukuzwa bila utaratibu hivyo kuitaka Tume ya Uchaguzi (NEC) isitangaze jimbo kuwa wazi.

Nje ya Mahakama Nassari amesema hakuna dhahabu nzuri isiyopita kwenye moto na kubainisha kuwa alishakoswa risasi iliyompiga mbwa wake, alinusurika ajali ya ndege na kwamba hili la ubunge halimtishi

Chanzo: Mwananchi
Nasari ni disgrace mwehu mkubwa kabisa

Sent using Jamii Forums mobile app
 

tpaul

JF-Expert Member
Feb 3, 2008
16,420
2,000
Hii movie mimi hata siilewi. Katika wakati huu wa kuwindwa na CCM na serikali yake ya kishetani, Nassari alipaswa kuwa makini zaidi. Halafu miongoni mwa wabunge wote wale Ndugai alijuaje kuwa Nassari hajahudhuria mikutano 3? Huu uvuaji wa ubunge ni wa kihistoria.
 

JokaKuu

Platinum Member
Jul 31, 2006
22,278
2,000
..nina mashaka na usahihi wa taarifa hii.

..Nassari amekwenda mahakamani akipinga uamuzi wa uongozi [ spika + katibu ] wa bunge kumvua nafasi yake ya uwakilishi.

..mahakama inawezaje kusema imekubaliana na uamuzi wa bunge wakati shauri lilikuwa limewekewa PINGAMIZI?

..naamini mahakama imetupilia mbali kesi ya Nassari lakini naamini ni kwasababu tofauti na hizi tulizoletewa na mtoa mada.

..Nassari bado ana nafasi ya kufungua upya shauri lake akizingatia mapingamizi aliyowekewa mwanzo.

..Mahakama inatakiwa itoe maamuzi baada ya kusikiliza upande wa Nassari na upande wa uongozi wa bunge.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom