Mahakama Kuu Dodoma: Joshua Nassari ashindwa kesi yake ya kuvuliwa ubunge

Hivi Inakuwaje U-drwaw Ww Application Then Ufanye Attentions Ww Mwenyewe? Hizi Legal Technicalities Mawakili Mda Mwingine Wanafanya Kuharibu Kesi Za Clients.
Tena Hii Errors Ambayo Haiwezi Kuwa Curable Hata Kidogo

Sent using Jamii Forums mobile app
Duu, Kalonga anawezaje kufanya kosa hilo aise, halafu kwanini hawakumshirikisha Elias Machibiya!
 
Jibu maswali yafuatayo kupata jibu kuhusu Nassari kuvuliwa ubunge (CHEZEA MSHAHARA ILA USICHEZEE KAZI)
1. Je alipo ondoka na kukaa huko nchi ya kigeni hakujua sheria zinamtaka afanye nini muda wa kikao unapofika? je alifanya kama sheria zinavyomtaka?
2. Je haruhusiwi mtu mwingine yeyote yule kukaa na mgonjwa hospitalini majukumu yanapokuwa yametokea kama dharura au ya kawaida kama mgonjwa sio serious sana,
3. Ni aina gani ya ugonjwa aliokuwa nao mkewake hadi asijifungulie kwenye hospitali mojawapo hapa nchini (Aghakhan, Muhimbili, au private hospital yoyote ile) ubishoo ni shida sana,
4. Miezi yote hiyo huko hospitali alikuwa tu ndani ya wodi hadi vikao vyoooote vinapita mke alikuwa maututi?

Ukijibu haya maswali vizuri utaelewa kuwa alifanya anachokifanya kama plan ili asishtukiwe kwa alichokusudia, baada ya kubanwa na chama aende mahakamani sasa chama kitaelewa kuwa hajaonewa alikusudia ili ahamie upande wa pili.
 
Acheni uoya oya jemeni!!? Bunge lilimsamehe lini huyu dogo. Fuatilieni mwenendo wa taarifa, vinginevyo mtalishwa matango pori kila siku. Msamaha mnaouzungumzia ni wa mkutano wa mwaka juzi wala sio mwaka jana ambapo labda mngeweza kuchanganya!! Dogo ndo hvyo tena!
Hata nami nashangaa kesi ya nin wakat bunge lilishasamehe au ?? sielewi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jamaa ni mpuuzi kama hajanunuliwa Bhasi hajitambui... Mbunge mzima unasema ulikuwa unashinda hosp kumhudumia mkeo?????? Upuuzi wa hivi akawaambie wajinga wenzieee

Sent using Jamii Forums mobile app
Mim nmepiga hesabu ya vile vikao alivyokosa mfululizo ni takriban miez 10 sasa yote hyo unauguza na bado unashindwa kutoa taarifa kwa boss wako? Akamleekwa nafasi sasa mwanae huko Marekani
 
Kama sio mbinu chafu basi muda utasema..


Sent from my iPhone using Tapatalk
 
View attachment 1056846
Dodoma. Jaji wa Mahakama Kuu Dodoma, Latifa Mansour amekubaliana na uamuzi wa Spika wa Bunge, Job Ndugai kumvua ubunge Joshua Nassari (Arumeru Mashariki).

Jaji Mansour ametumia dakika 44 kusoma maelezo yaliyomweka katika wakati mgumu Nassari.

Machi 14, 2019 Ndugai aliiandikia Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) barua akiieleza kuwa Nassari amepoteza sifa ya kuwa mbunge baada ya kutohudhuria mikutano mitatu mfululizo bila kutoa taarifa.

Spika Ndugai aliitaja mikutano hiyo kuwa ni wa 12 ulioanza Septemba 4 hadi 14; Novemba 6 hadi 16, 2018 na wa Januari 29 hadi 9.

Baada ya uamuzi huo, mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe alisema amemuagiza Nassari kuzungumza na wananchi na wanachama wa jimbo lake kuwaeleza kilichotokea.

Akisoma uamuzi wake leo Ijumaa Machi 29, 2019 Jaji huyo ametumia kifungu cha 5 (4) kuwa Nassari alipaswa kupeleka malalamiko yake kwa Katibu wa bunge wala si kama alivyofanya.


Kifungu kingine kilichombana Nassari ni cha kanuni ya 146 (2) kwamba alijifukuzisha mwenyewe kwa kutohudhuria vikao vitatu mfululizo vya Bunge bila taarifa.

Mawakili wa Serikali, Alesia Mbuya, Masunga Kamuhanda na Pius Mboya walipangua hoja za wakili wa utetezi, Fred Kalonga aliyekuwa akipinga kuwa mbunge huyo alifukuzwa bila utaratibu hivyo kuitaka Tume ya Uchaguzi (NEC) isitangaze jimbo kuwa wazi.

Nje ya Mahakama Nassari amesema hakuna dhahabu nzuri isiyopita kwenye moto na kubainisha kuwa alishakoswa risasi iliyompiga mbwa wake, alinusurika ajali ya ndege na kwamba hili la ubunge halimtishi.

Chanzo:- https://www.mwananchi.co.tz/habari/...ge-Nassari/1597296-5047468-nr4hf3z/index.html
Tatizo la kuleta watu Bungeni kutafuta pesa za kulipa mahali.
Eti alitamani sana kupata mtoto!
Eti anaijali sana familia yake kuliko kikao cha bunge.
 
Mambo hapa bongo hayaeleweki, nilisikia swala lake lilipelekwa Bungeni na Bunge likaafikiana kufuta adhabu aliyopewa na spika ndugai, ukweli ukoje hapa wadau ??
 
Mambo hapa bongo hayaeleweki, nilisikia swala lake lilipelekwa Bungeni na Bunge likaafikiana kufuta adhabu aliyopewa na spika ndugai, ukweli ukoje hapa wadau ??
Zilikua propaganda za bavicha

We think too small, like the frog at the bottom of the well. He thinks the sky is only as big as the top of the well. If he surfaced, he would have an entirely different view.
 
Dogo mpuuzi sana - hakuna alikoonewa
Bunge liende mbali zaidi kwa kumtaka Nassar arejeshe mshahara kwa kipindi chote alichokuwa mtoro - fedha hizo zinaweza kufanya kazi nzuri kwenye Zahanati
 
Nanukuu maneno ya Joshua nasary saa chache baada ya spika kuiomba NEC itoe ratiba ya uchaguzi alsema mh nasary "hata spika anajua kuwa nauguza mke wangu nje ya nchi na ya kwamba hata siku namvisha Pete mke wangu hata spika alishuhudia hvo ni wajibu wangu kumsimamia mke wangu wakat wa kujifungua .....
Kwani mke wake hawezi kujfungua nchini Tanzania? Au anataka history ya mwanae kuwa alizaliwa nje ya nchi?
Hoja za nasary hata mm skuzipenda na hazina mashiko ......
Ngoja tuone nn kitafuata
Joshua uliyataka kabsa yani kisa ndugai alfika kwenye harusi yako unataka ajue na siku ya kujifungua kwa mkeo?
 
Back
Top Bottom