Mahakama Kuu Dar, imetupilia mbali kesi ya Kikatiba iliyofunguliwa dhidi ya Spika Ndugai kwa kumtambua Mwambe kama Mbunge baada ya Kujiuzulu

ngoshwe

JF-Expert Member
Mar 31, 2009
4,137
2,000
1591186270045.png

Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam imetoa uamuzi na kutupilia mbali shauri la Kikatiba Na. 10 la mwaka 2020 lililofulinguliwa na Wakili wa Kujitegemea Revocatus Paul Kaunda kupinga Kauli ya Mhe. Spika aliyoitoa Bungeni kumtambua Mhe. Cecil Mwambe kuendelea kuwa Mbunge.

Mahakama Kuu kupitia Jopo la Majaji watatu ambao ni Mhe. Jaji Issa Maige, Stephen ,Mrimi Magoiga na Seif Mwinshehe Kulita, wametupilia mbali shauri hilo kwa uamuzi kuwa "SHAURI HILO HALINA MSINGI KISHERIA NA LENYE LENGO LA KUSABABISHA USUMBUFU KWA MAHAKAMA ". Mahakama imeona kuwa hoja zilizoletwa Mahakamani hapo zinahusu kuitaka Mahakama kutoa tafsiri iwapo Mhe. Mwambe ni Mbunge au sio mbunge. Hoja hiyo ingepaswa kuletwa kupitia shauri la Uchaguzi chini ya Ibara ya 83 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na sio suala la Maombi ya Haki ya Kikatiba kama Mleta maombi hayo alivyofanya kupitia Ibara ya 26(2) ya Katiba. Mahakama imeona kuwa suala ambalo limejitokeza Bungeni kuhusu kukoma au kutokoma kwa Ubunge wa Mhe. Mwambe linahusu pia uamuzi wa Spika chini ya Kifungu cha 37 Cha Sheria ya

Katika shauri hilo Mleta Maombi waliwakilishwa na Wakili Daimu Halgfani, Steven Mwakibolwa, Fulgence Massawe. Mwambe aliwakilishwa na Wakili wa Kujitegemea Raphael na Upande wa Mhe Spika na Mwanasheria Mkuu wa Serikali wamewakilishwa na Bw. Vicent Tangoh (Wakili wa Serikali) Mkuu) , Bw. George Mandepo (Wakili wa Serikali Mkuu), Bibi Alesia Mbuta (Wakili wa Serikali Mkuu), Bw. Erigh Mrisha (Wakili wa Serikali) na NBibi Narindwa Sekimanga.

Mahakamani hapo leo pia, Mahakama ilitaja kesi inayofafana iliyofunguliwa na Arusha na kuhamishiwa Masijala ya Dar es Salaam. Kesi hiyo Na. 12 ya 2020 imefunguliwa na Asasi iliyo ya Kiserikali ya Civic and Legal Organisation ikipinga pia ubunge wa Mhe. Mwambe. Wadawa katika kesi hiyo ya kikatiba ni Mhe. Spika , Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Cecil Mwambe.

Kesi hiyo itakuja kwa kutajwa tena Mahakamani hapo tarehe 11 Juni, 2020.

=====

Kuu Kanda ya Dar es Salaam imetupilia mbali kesi ya Kikatiba iliyofunguliwa na wakili Paul Kaunda dhidi ya Spika wa Bunge, Job Ndugai akiomba mahakama hiyo kutengua amri ya Spika kumtambua Cecil Mwambe kama mbunge halali wa Ndada ikisema amekosea kufungua shauri hilo.

Mbali na Ndugai, walalamikiwa wengine katika shauri hilo ni aliyekuwa mbunge wa Ndanda, Cecil Mwambe na Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Taarifa kwa kina.....

Mahakama yatupilia mbali kesi dhidi ya Spika, AG, Mbunge

MAHAKAMA Kuu, Kanda ya Dar es Salaam, imetupiliwa mbali kesi ya Kikatiba dhidi ya Spika wa Bunge la Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Jobu Ndugai na wenzake kwamba imefunguliwa kinyume na utaratibu.

Kesi hiyo ilifunguliwa na Wakili Paul Kaunda dhidi ya Spika Ndugai, Mbunge wa Jimbo la Ndanda kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), ambaye kwa sasa amehamia CCM, Cecil Mwambe na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG).

Mahakama hiyo iliyoketi chini ya jopo la majaji watatu likiongozwa na Mwenyekiti, Issa Maige, akisaidiana na Stephen Magoiga na Seif Kulita, ilitoa uamuzi huo baada ya kusikiliza pingamizi la awali lililowasilishwa na Mwanasheria Mkuu.

Jaji Maige alisema jopo wamekubaliana na hoja za Mwanasheria Mkuu kwamba mlalamikaji amekosea kufungua kesi hiyo kwa kutumia ibara ya 26, bali alipaswa ajiegemeza katika ibara ya 83 ya Katiba ikiwa sambamba na kifungu cha 37 cha Sheria ya Uchaguzi.

Ibara hiyo inaelekeza utaratibu wa kuwasilisha malalamiko kama yaliyowasilishwa na mlalamikaji.

Alisema maneno aliyotamka Spika yako katika msingi na utaratibu wa kawaida katika utendaji wake.

Katika kesi ya msingi, Wakili Kaunda anadai Mwambe alitangaza kujivua uanachama wa Chadema na kujiunga na CCM kauli ambayo iliungwa mkono na Katibu Mkuu wa CCM, Dk. Bashiru Ally, aliyempokea rasmi Mwambe mbele ya hadhira kwa kumkabidhi kadi ya CCM, na Mwambe naye alimkabidhi Katibu Mkuu huyo kadi yake ya Chadema.

Wakili Kaunda anadai kitendo cha Spika kumtambua Mwambe kama Mbunge halali wakati ameshajivua uanachama wa chama kilichomdhamini kama Mbunge wa Ndanda (2015-2020), ni ukiukwaji wa ibara ya 71(1)(f) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 1977 na hakuna mamlaka yoyote nchini, achilia mbali Spika, yenye uwezo wa kumrudisha bungeni mbunge ambaye kwa hiyari yake mwenyewe ameamua kujivua uanachama wa chama cha siasa kilichomdhamini kupata ubunge.

Katika hoja za awali za serikali, pamoja na mambo mengine ilidai kuwa shauri hilo halistahili kwa kuwa linakinzana na Sheria ya Utekelezaji wa Haki na Wajibu wa Msingi, pamoja na Ibara ya 26(2) ya Katiba ya nchi.

Pamoja na pingamizi hilo pia serikali katika majibu yake inadai kuwa Mwambe bado ni Mbunge halali wa Ndanda kwa mujibu wa Katiba na sheria nyingine za nchi na anastahili stahiki zote kwa mujibu wa sheria na kanuni zinazotumika kusimamia masuala ya Bunge.

Serikali inadai kuwa Spika hajavunja sharti lolote la Katiba ya nchi kama inavyodaiwa, na hivyo inamtaka mdai kuthibitisha madai yake.

 

Attachments

paul sylvester

JF-Expert Member
Mar 18, 2020
1,451
2,000
Mzigo ukidondoka huwa unatoa mlio wa puuuu!!! Na sasa mlio unzidi kuwa mkubwa zaidi Kwa ndugu zetu, badala ya mlio huo sasa unatoa mlio wa Pwaaaaa!! Ukiona hivyo, mzigo hauko mbali kupasuka

Utakapoona mtu mzima akilia Kwa sauti, usishangae Kwa sababu ni Mengi yanayompata! Hata huko mzigo unapigwa chini??😂
 

denooJ

JF-Expert Member
Mar 31, 2020
1,180
2,000
Ok, na hao wengine waliobaki wa Arusha bora waondoe shauri lao mapema kukwepa gharama.
 

feyzal

JF-Expert Member
Apr 20, 2016
3,180
2,000
Kosa walilofanya chadema ni kama lile lile walilofanya CUF kwa Lipumba.
Mahakama ime-site vifungu na ibara za katiba juu ya kutupilia mbali shauri hilo na imeshauri utaratibu ambao ulipaswa kufuatwa. Sasa ni kazi kwako kujibu kwa kupangua vifungu hivyo na sio porojo.
 

El Roi

Member
May 29, 2020
18
75
Hicho kinachoitwa technicalities, ndo kinafanya vyombo vya kutoa haki vionekane Kama hata hiyo haki hawaijui. Naona ile dhana ya justice doesn't necessarily mean lawful inaanza kuondoka kwenye legal fraternity. My heart is really crying for justice and not this animal" technicalities".
 

dubu

JF-Expert Member
Oct 18, 2011
3,333
2,000
Tuseme haki imetendeka ili kuiondolea aibu Mahakama Kuu.
 

JOHNKEKE

JF-Expert Member
Mar 30, 2011
970
1,000
Hata mtoto wa Darasa la pili alijua aliyefungua kesi hana hoja, labda anatafuta kiki. Alafu bado eti ni "mwanasheria", tuna safari ndefu.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom