Mahakama kuu Arusha yamvua ubunge Onesmo Ole Nangole (CHADEMA), yaamuru uchaguzi urudiwe

ZamdaIssa

JF-Expert Member
Nov 10, 2015
879
1,456
Kesi iliyokuwa inaunguruma kuanzia tarehe 29.02.2016 katika mahakam kuu jijini Arusha imetolewa hukumu leo hii

Katika shauri hilo aliyekuwa mgombea ubunge wa CCM jimbo la Longido Dr KIRUSWA alifikisha mahakamni shauri hilo la kupinga matokeo ya ushindi dhidi ya mbunge wa Longido mh ONESMO NANGOLE.

Akisoma hukumu hiyo,Jaji MWAGESI alisema kwamba mlalamikaji ndugu Kiruswa aliwakilishwa na Wakili msomi Dr.Masumbuko Lamwai na Wakili Haraka.

Katika shauri hilo,dai la msingi la mlalamikaji bwana Kiruswa lilikua ni
1.Kutumika kwa lugha ya matusi na kashfa wakati wa kampeni kutoka kwa mh Onesmo Nangole

2.Kuwepo kwa wapiga kura kutoka nchi jirani ya Kenya walioletwa na Mh Nangole

3.kutumika kwa magari ya Chadema kwenye kusindikiza na kubebea masanduku ya kupigia kura

4.Mkurugenzi wa Uchaguzi kutangaza matokeo baada ya mgombea wa CCM kutolewa nje.

5.Kutokea kwa vurugu ndani ya chumba cha kuhesabu matokeo

Kutokana na madai hayo na kwa kuzingatia kanuni,sheria na ushahidi uliotolewa pamoja na vielelezo na mashahidi wa pande zote mbili,Jaji kutoka mahakama kuu Bukoba Mh.Jaji Mwagesi alisema;

"Kutokana na kuzingatia viini vyote vya shauri hili kama vilivyosikilizwa na kwa mujibu wa sheria,Natamka kwamba;

Mahakama hii imetengua shauri hili na kwa kujirisha kwamba mchakato mzima haukuwa wa haki na huru hivyo mahakama inaamuru uchaguzi urudiwe upya.

====

MAHAKAMA Kuu Kanda ya Arusha, jana imetengua ubunge wa Mbunge wa Longido, Onesmo ole Nangole (Chadema) kutokana na kesi ya uchaguzi namba 36 ya mwaka 2015, iliyofunguliwa na aliyekuwa mgombea wa Chama cha Mapinduizi (CCM), Dk. Steven Kiruswa akipinga ushindi wake.

Katika uchaguzi huo, Nangole alitangazwa mshindi kwa kupata kura 20,076 dhidi ya Dk. Kiruswa aliyepata 19,352.

Hukumu hiyo ilisomwa jana kuanzia saa 3:23 asubuhi hadi saa 6:20 mchana na Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu, Kanda ya Bukoba, Sivangilwa Mwangesi aliyekuwa akiisikiliza.

Akisoma hukumu hiyo, Jaji Mwangesi alisema mahakama imebatilisha matokeo hayo kutokana na kasoro zilizojitokeza kwenye uchaguzi, hasa ndani ya chumba cha majumuisho ya kura ambapo kulitokea fujo zilizoanzishwa na Nangole.

Alisema kasoro hizo ziliathiri uchaguzi na hivyo akaelekeza ufanyike upya ili kuwawezesha wananchi wa Jimbo la Longido kuchagua mbunge atakayewawakilisha kwa ridhaa yao.

“Mahakama inatamka kwamba, uchaguzi wa Longido ulikuwa batili, hivyo hati itolewe kwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), kuhusu ubatilishaji wa matokeo hayo ili kuwezesha uchaguzi urudiwe na mdai atalipwa gharama zake za kesi.

“Mdaiwa bado ana fursa ya kukata rufaa endapo atakuwa hajaridhishwa na uamuzi uliotolewa,” alisema Jaji Mwangesi.

Kuhusu kasoro zilizojitokea na kufanya matokeo hayo kubatilishwa, Jaji Mwangesi alizitaja kuwa ni kutokea kwa fujo ndani ya chumba cha majumuisho ya kura, zilizosababisha wagombea kutolewa nje ya chumba na kuhitimisha majumuisho bila kuwapo Dk. Kiruswa na mawakala wake.

Kuhusu vurugu hizo, jaji huyo alisema ushahidi wa upande wa mdai uliotolewa na shahidi wa tano, ambaye ni Mkuu wa Polisi wa Wilaya (OCD) ya Longido, ulithibitisha jinsi fujo zilivyotokea ndani ya chumba cha majumuisho.

Hoja ya pili iliyotajwa katika hukumu hiyo iliyosababisha kutenguliwa kwa ubunge wa Nangole ni kuwapo kwa kasoro kwenye nakala halisi namba 21(b) ambapo katika vituo vitatu zilitumika fomu namba 21(c) ambazo zilitumika kujaza matokeo ya udiwani.

Jaji Mwangesi alisema Msimamizi wa Uchaguzi, Felix Kimario, aliyekuwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Longido, ambaye ni mdaiwa wa pili katika kesi hiyo, hakutoa maelezo ni kwanini fomu hizo za udiwani zilitumika kujaza matokeo ya ubunge badala ya kutumika fomu za ubunge.

“Kwahiyo, mahakama hii imeona hizo ni kasoro ngumu na si za kawaida ambazo zinaonyesha kulikuwa na lengo la kudanganya na kupotosha ukweli wa matokeo hayo,” alisema Jaji Mwangesi.



HOJA ZILIZOKATALIWA

Wakati kesi hiyo ikiendelea, hoja za mdai zilikataliwa na mahakama hiyo baada ya kuonekana hazikuathiri matokeo ya uchaguzi kwa kuwa makosa yaliyokuwa yakilalamikiwa yalikuwa ni ya kibinadamu.

Hoja hizo ni uhamishaji wa matokeo ya fomu namba 21(b) kwenda kwenye ‘spread sheet’ kuonekana ni tofauti ambapo mahakama iliona kura 730 zilikuwa na kasoro zikionyesha Dk. Kiruswa alikuwa amedhulumiwa kura 379.

“Ni kweli hiyo ndiyo idadi ya kura ambazo hazikuingizwa kwa mdai wa kesi, ila hazijaathiri matokeo yake kwani hata angeongezewa kura hizo, bado Ole Nangole angekuwa amemshinda kwa idadi ya kura nyingi.

“Kasoro nyingine ni uingizaji wa matokeo kutoka fomu namba 21(b) kwenda fomu namba 24 (b), zenye matokeo ya jumla ya jimbo hilo na kudaiwa kutumia lugha zisizo za kiungwana na zenye ubaguzi dhidi ya Dk. Kiruswa aliyedaiwa kuwa ni Mmarekani.

“Maneno ya kuitwa Mmarekani yamekuwa yakiitwa ni siasa za majitaka, na yalitamkwa kwa ajili ya kupakana matope wala hayakuwa ya ubaguzi.

“Hoja nyingine ambayo mahakama imeona haikuwa na madhara ni iliyosema raia wa Kenya walipiga kura katika uchaguzi, baadhi ya vituo kuchelewa kufunguliwa na magari ya wafuasi wa Chadema kudaiwa kubeba na kusindikiza masanduku ya kura,” alisema Jaji Mwangesi.

Katika kesi hiyo, Nangole aliwakilishwa na mawakili John Materu na Method Kimomogolo wakati Dk. Kiruswa akiwakilishwa na Daudi Haraka na Dk. Masumbuko Lamwai.

Msimamizi wa Uchaguzi na Mwanasheria Mkuu wa Serikali waliwakilishwa na Wakili David Kakwaya.

Shauri hilo lilianza kusikilizwa Februari 29, mwaka huu ambapo Dk. Kiruswa aliwasilisha mashahidi 28 na vielelezo vinane, huku Nangole aliwasilisha mashahidi tisa.



NJE YA MAHAKAMA

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya hukumu hiyo, Nangole alisema mahakama haikumtendea haki kwani anaamini alishinda kihalali.

“Mahakama haijatenda haki, ila nitakaa na mawakili wangu ili nikate rufaa,” alisema Nangole aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Arusha kabla hajajiunga na Chadema mwaka jana.

Wakati Nangole akisema hivyo, Dk. Kiruswa aliishukuru mahakama kwa kusema imetenda haki.

Chanzo: Mtanzania
 
hatupendi kurudia uchaguzi, ni matumizi mabaya ya bajeti...hakimu analo
 
Kesi iliyokuwa inaunguruma kuanzia tarehe 29.02.2016 katika mahakam kuu jijini Arusha imetolewa hukumu leo hii

Katika shauri hilo aliyekuwa mgombea ubunge wa CCM jimbo la Longido Dr KIRUSWA alifikisha mahakamni shauri hilo la kupinga matokeo ya ushindi dhidi ya mbunge wa Longido mh ONESMO NANGOLE

Akisoma hukumu hiyo,Jaji MWAGESI alisema kwamba mlalamikaji ndugu Kiruswa aliwakilishwa na Wakili msomi Dr.Masumbuko Lamwai na Wakili Haraka.

Katika shauri hilo,dai la msingi la mlalamikaji bwana Kiruswa lilikua ni
1.Kutumika kwa lugha ya matusi na kashfa wakati wa kampeni kutoka kwa mh Onesmo Nangole
2.Kuwepo kwa wapiga kura kutoka nchi jirani ya Kenya walioletwa na Mh Nangole
3.kutumika kwa magari ya Chadema kwenye kusindikiza na kubebea masanduku ya kupigia kura
4.Mkurugenzi wa Uchaguzi kutangaza matokeo baada ya mgombea wa CCM kutolewa nje.
5.kutokea kwa vurugu ndani ya chumba cha kuhesabu matokeo

Kutokana na madai hayo na kwa kuzingatia kanuni,sheria na ushahidi uliotolewa pamoja na vielelezo na mashahidi wa pande zote mbili,Jaji kutoka mahakama kuu Bukoba Mh.Jaji Mwagesi alisema;
"Kutokana na kuzingatia viini vyote vya shauri hili kama vilivyosikilizwa na kwa mujibu wa sheria,Natamka kwamba;

Mahakama hii imetengua shauri hili na kwa kujirisha kwamba mchakato mzimahaukuwa wa haki.
 
6 Reactions
Reply
Back
Top Bottom