Mahakama kutoa hukumu juu ya Ubunge wa Mnyika Septemba 27

Habarindiyohiyo

JF-Expert Member
Aug 11, 2008
263
13
Ng'umbi ataka utetezi wa Mnyika usikubaliwe. Jaji Msuya alisema uamuzi wa maombi hayo atautoa Septemba 27 mwaka huu.

Mbali na Mnyika walamikiwa wengine ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Msimamizi wa Uchaguzi wa jimbo la Ubungo.

Miongoni mwa madai katika kesi ya msingi, Ng'humbi anadai Mnyika, wasaidizi na mashabiki wake walifanya vitendo ambavyo ni ukiukwaji wa sheria kwa makusudi kwa madhumuni ya kushinda uchaguzi.

Anadai Mnyika mara kadhaa alitumia barua ya Wakala wa Barabara (Tanroads) ya Machi 30, 2010 iliyotumwa kwa CCM kuwadanganya wakazi wa Kimara kwamba nyumba zao zitabomolewa kama watamchagua Ng'humbi na kwamba Mnyika aliwanunulia pombe na kuwalipa Sh 20,000 wananchi wa Kimara Saranga wampigie kura.

....ndiyo hiyo;

HabariLeo | Ng'humbi akiri hati ya madai ina makosa
 
huyu mama ana mapepo? Ashukuru kwa vikura alivyopata. Wanaomdannganya hawampendi
 
Ngoja tuone maamuzi ya mahakama yatakuwaje maana kuna vitu vingine vipo wazi kabisa lakini kisheria hatujui ikoje? Ukiangalia mama alishindwa kwa tofauti kubwa ya kura licha ya system ya tume ya uchaguzi kuwa slow kwa mara ya kwanza na kutumika nguvu kubwa mno kunusuru wizi wa kura. Yoye hayo hayaonekani ila hili la kuhonga limeonekana!
 
Mbali na Mnyika walamikiwa wengine ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Msimamizi wa Uchaguzi wa jimbo la Ubungo.

Hapa mbona sielewi inakuwaje mgombea wa chama tawala anamshitaki CJ wa serikali iliyoundwa na chama tawala, na pia mwanaCCM mwenzie (Msimamizi wa uchaguzi)
 
ng'umbi ataka utetezi wa mnyika usikubaliwe. Jaji msuya alisema uamuzi wa maombi hayo atautoa septemba 27 mwaka huu.

Mbali na mnyika walamikiwa wengine ni mwanasheria mkuu wa serikali na msimamizi wa uchaguzi wa jimbo la ubungo.

Miongoni mwa madai katika kesi ya msingi, ng'humbi anadai mnyika, wasaidizi na mashabiki wake walifanya vitendo ambavyo ni ukiukwaji wa sheria kwa makusudi kwa madhumuni ya kushinda uchaguzi.

Anadai mnyika mara kadhaa alitumia barua ya wakala wa barabara (tanroads) ya machi 30, 2010 iliyotumwa kwa ccm kuwadanganya wakazi wa kimara kwamba nyumba zao zitabomolewa kama watamchagua ng'humbi na kwamba mnyika aliwanunulia pombe na kuwalipa sh 20,000 wananchi wa kimara saranga wampigie kura.

....ndiyo hiyo;

habarileo | ng'humbi akiri hati ya madai ina makosa

tusubiri tuone
 
Hapa mbona sielewi inakuwaje mgombea wa chama tawala anamshitaki CJ wa serikali iliyoundwa na chama tawala, na pia mwanaCCM mwenzie (Msimamizi wa uchaguzi)


Anawashtaki kwa sababu walikataa kusikiliza maagizi ya wakubwa wao kupindua matokeo ya Uchaguzi kama wenzao wa Segerea, Shinyanga, Kibaha Mjini nk walivyofanya.
 
Kwani lazma wote tuwe wabunge. Kama umeshndwa si usubiri msimu mwingine mama?
 
Jamani muacheni huyu mama wamlie viela vyake vya pension ya ukuu wa wilaya akija stuka ana kitu kweli nimeamini siasa ni kama kamari ukicheza vibaya 2 unaliwa zote.
 
Anafikiri ubunge ni sawa na UKUU WA MKOA? Mi natamani uchaguzi urudiwe tuone jinsi atakavyo pigwa gap mara kumi ya kura atakazopata ndo magamba waache kukata rufani

Hata mimi natamani iwe hivyo,this time atajua nini maana ya nguvu ya umma.
 
Huyu mama anapoteza muda wake.
Mie ni CCM damu lakini ubungo najua tumeshindwa kihalali kabisa.
Na sababu ni kwamba mnyika hakupambanishwa na size yake....huyu mama sijui alitolewa wapi...
Hii mentality ya kutokubali matokeo sio nzuri hata kidogo maana yapoteza muda na rasilimali badala ya kujenga nchi.
Huyu mama anafanana na mwenzie batilda kupinga matokeo wakati na yeye alishindwa kwa landslide.
 
Kwanza ifahamike kuwa kura za Mnyika zilipunguzwa kwa zaidi ya 5000. Hesabu zetu na hesabu za tume ya Taifa ni tofauti kwa zaidi ya kura 5000. Huyo mama hata akishinda mahakamani atavuna aibu huku mtaani, tukirudi uwanjani kwenye Bi election.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom