Mahakama kusaidia watumishi wake walioathirika

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
54,441
27,210
Wafanyakazi mahakamani kupewa bonasi wakipimwa ukimwi
Na Omary Magongo, Same


KATIKA juhudi za kuhamasisha upimaji wa virusi vya ukimwi kwa hiari, Idara ya Mahakama imeahidi kutoa bonasi kwa watumishi wake watakaojitokeza kupima kwa hiari na kubainika kuambukizwa.


Mtumishi atakayepima kwa hiari na kugundulika kuwa meambukizwa ugonjwa wa ukimwi, atalipwa bonasi ya Sh100,000 kila mwezi ili kumsaidia kuimarisha afya yake na kujikimu.


Akizungumza na watumishi wa Idara ya Mahakama katika Wilaya ya Same, mkoani Kilimanjaro juzi, Jaji Kiongozi wa Mhakama Kuu Tanzania, Salum Massati, alisema Ukimwi bado ni tishio kwa nguvukazi katika Idara hiyo na�Taifa kwa ujumla.


Hata hivyo, Jaji Massati alitahadharisha kuwa, kutolewa kwa motisha kusije kukapelekea baadhi ya watumishi wasiowaaminifu kutumia mwanya huo kupanga matokeo na madaktari wasio waaminifu na kuwaandikia kuwa wameathirika, kumbe sivyo ili wapate bonasi hiyo.


Pia aliwaonya watumishi walioathirika kutonyanyapaliwa kazini na badala yake wajengewe upendo, faraja, ushauri nasaha kwani kwa kufanyiwa hivyo kutawapunguzia msongo wa

mawazo na kurefusha maisha yao.


Aliwataka watumishi hao kujenga tabia na utamaduni wa kupima afya zao mara kwa mara na wakijua wameathirka itairahisishia serikali kujua ni msada gani unafaa kuwapatia kuliko kujificha wakati wameambukizwa.


Jaji Kiongozi alikuwa wilayani hapa kwa ziara ya siku moja, ambapo pamoja na mambo mengine, alikagua miundombinu ya Idara hiyo katika Wilaya ya Same.


Katika hatua nyingine, Mahakimu watakaokiuka taratibu na kanuni za matumizi ya fedha za serikali zinazotokana na makusanyo ya maduhuli mbalimbali, watasimamishwa kazi mara moja.


Kauli hiyo ilitolewa juzi na Jaji Massati, alipokuwa anazungumza na wafanyakazi wa Idara ya Mahakama katika Wilaya ya Same na kuongeza kuwa matumizi hayo yanailetea Idara hiyo dosari za kihasibu.


Jaji Massati alisema kuna baadhi ya Mahakimu hawapeleki benki fedha zinazopatikana kutokana na faini na mapato mengineyo na kuzipangia matumizi bila kibali na kufafanua kuwa kufanya hivyo ni sawa na kuiibia serikali.


Alisema serikali haitavumilia vitendo vya baadhi ya Mahakimu visivyozingatia maadili ya kazi na kuwa mahakimu wazembe, wavivu, walevi, wala rushwa na wanaowanyanyasa wananchi wanaisababishia Mahakama kutoaminiwa kama chombo cha kusimamia na kutoa haki
 
Last edited by a moderator:
Samahani,

Je Afande Lawrence Masha anahusiana vipi na mahakama? Wizara yake ya mambo ya ndani haisimamii Mahakama zetu! Je mwenzetu ulikosea au kuna habari nyingine?

Tukirudi kwenye context ya motisha kutoka kwa Jaji Kiongozi, nafikiri hili ni jambo jema na la busara. Taifa letu linakabiliwa na janga kubwa la Ukimwi na tumeendelea kulipuuzia tukidhani kuwa ni suala dogo.

Ukimwi unatishia uhai wa Taifa letu. Ikiwa 50% ya Watanzania wa umri kati ya miaka 12-45 wako hatarini ama kwa kuwa tayari wana virusi au wanaweza kupata virusi kirahisi, hamasa kubwa ni kama kutoa motisha ambao utawafanya wafanyakazi na hasa kundi hili kujifikiria upya na kuliangali suala la ukimwi kwa makini.
 
Back
Top Bottom