Mahakama kuballance kesi, chadema tujiandae kwa hili' | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mahakama kuballance kesi, chadema tujiandae kwa hili'

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by AdvocateFi, May 1, 2012.

 1. AdvocateFi

  AdvocateFi JF-Expert Member

  #1
  May 1, 2012
  Joined: Jan 15, 2012
  Messages: 10,705
  Likes Received: 592
  Trophy Points: 280
  Ni ukweli ulio wazi kwamba mahakama zetu hazipo huru so hata siku moja CHADEMA tusitegemee haki iliyo kamili kutoka ktk mahakamA hizi za CCM,. Tumeshuhudia jinsi kesi ya G. Lema ilivyohujumiwa na mahakama ili ku-neutralize furaha ya ushindi wa CHADEMA arumeru. Pia na kwa mfululizo wa ushindi wa kesi 3 za wabunge wa CHADEMA mahakamani (lissu, nyasebo, mbasa), na endapo mpendazoe atashinda kesi segerea, Ni wazi kwamba CCM hatakubali kushindwa huko na badala yake itajitahidi kufanya juu chini kupitia hiz mahakama zake ili ku-neutralize tena furaha ya ushindi wa CDM kama ilivyokuwaKwa lema. Hivyo
  CDM tujiandae kumpoteza Mnyika(ubungo) au opulukwa (meatu).
   
 2. Tume ya Katiba

  Tume ya Katiba JF-Expert Member

  #2
  May 1, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 4,892
  Likes Received: 732
  Trophy Points: 280
  Mkuu wangu shardcole, naona leo umekuja na single mpya!

  Iacheni sheria ifuate mkondo wake kaka! na sumbawanga mmeonewa?
   
 3. KOMBESANA

  KOMBESANA JF-Expert Member

  #3
  May 1, 2012
  Joined: Jun 18, 2009
  Messages: 862
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Ni vibaya kuwa na wazo hilo maana Mh Jonh Mnyika hajaonesha kutokuwa na imani na Mahakama wala kutokuwa na imani na sisi tuliomchagua wala kutomwamini Mungu wake.Tusiposhinda Mahakamani tutashinda kwenye ballot kwa kutumia peoples power!tusitake kutishiana wote sisi ni wanadamu
   
 4. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #4
  May 1, 2012
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,180
  Likes Received: 897
  Trophy Points: 280
  Assumption za kimasaburi.
   
 5. AdvocateFi

  AdvocateFi JF-Expert Member

  #5
  May 1, 2012
  Joined: Jan 15, 2012
  Messages: 10,705
  Likes Received: 592
  Trophy Points: 280
  Mkuu tatizo hizi mahakama zenu haziaminiki hata kidogo kwani zinan'gata na kupuliza na siku zote chama chako CCM kinatafuta majimbo ya CDM yale mjini na yenye umuhimu hapa nchini kama arusha.
  Time will tell
   
 6. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #6
  May 1, 2012
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,203
  Likes Received: 867
  Trophy Points: 280
  Invalid assumption; usahihi au uharamu wa kesi unatokana na jaji anayeisimamia kesi hiyo, hautegemei na mahakama kama institution.
   
 7. Duble Chris

  Duble Chris JF-Expert Member

  #7
  May 1, 2012
  Joined: May 28, 2011
  Messages: 3,487
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  wasiwasi wako tu hakuna kitu kama hicho
   
 8. AdvocateFi

  AdvocateFi JF-Expert Member

  #8
  May 1, 2012
  Joined: Jan 15, 2012
  Messages: 10,705
  Likes Received: 592
  Trophy Points: 280
  mkuu unayoyasema ni kweli kabisa lakini kazi ya ccm kupitia mahakama ni ku-neutralize ushindi wa CDM kama Arusha even if CCM wanajua kwamba hawatachukua hayo majimbo.
  Time will tell.
   
 9. AdvocateFi

  AdvocateFi JF-Expert Member

  #9
  May 1, 2012
  Joined: Jan 15, 2012
  Messages: 10,705
  Likes Received: 592
  Trophy Points: 280
  majibu ya kesi ya lema ni ishara tosha kwamba what will later.
   
 10. N

  Ndinani JF-Expert Member

  #10
  May 1, 2012
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 5,413
  Likes Received: 734
  Trophy Points: 280
  Mahakama zetu hazifanyikazi zake kwenye kisiwa cha Robinson Crusoe bali zinafanyakazi katika mazingira ya Afrika Mashariki; na hawa majaji wetu wanasoma kile kinachotokea kwa majaji wenzao hapo Kenya kwamba hukumu zao walizotoa hapo awali kuwakandamiza wananchi ndio hizo zinazotumika kuwachuja kama wanastahili kuendelea na kazi ya ujaji under the new Kenya constitution!! Jaji aliyehukumu kesi ya Lema ajue wazi kuwa hukumu yake ile will haunt him for the rest of his life as long as he will be allowed to continue sitting on the bench!! Wanajua kuwa hukumu wanazotoa zinaweza kuja kutumika baadae kuwafukuzisha kazi kama ilivyotokea kwa majaji hapo kwa jirani zetu Kenya; hivyo they are very careful na judgements wanazotoa kuwa hazipindishi haki na hiyo itadhihilika kwenye kesi ya Segerea kesho!!
   
 11. K

  Keil JF-Expert Member

  #11
  May 1, 2012
  Joined: Jul 2, 2007
  Messages: 2,214
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Bwana Shardcole,

  Huna haja ya kuanza kuwa na mawazo mabaya. Subirini hukumu ndipo mfanye hizo postmortem zenu ili kuona kama haki haikutendeka. Ni rahisi kusema hayo baada ya kupitia hukumu na kuona ni wapi sheria imepindishwa.

  Majaji nao wanaona upepo unaovuma, ipo siku nao watakuja kuhojiwa kuhusu hukumu wanazozitoa. Tumeona Kenya Majaji wakivuliwa u-Jaji wao. Rais wa Zambia ameunda tribunal kuangalia swala la Jaji mmoja kuhusu hukumu zake kwenye kesi 3. Kwa hiyo chochote ambacho majaji wanakifanya sasa hivi kina athari kubwa kwenye career yao, maana CCM haiwezi kutawala milele and some of them still have more than 10 yrs za ku-serve Mahakama as Judges.

  Judge anaesikiliza kesi ya Opurkwa nina imani nae, labda kama amekuwa compromised hivi karibuni baada ya kupandishwa kwa kasi nikilinganisha na wale ambao alianza nao au waliomtangulia kidogo. When it comes kwenye utendaji kazi bado huwa naona ni mtenda haki. Jaji Upendo Msuya, sijui. Judge Prof. Ibrahim Juma, tangu akiwa UD alikuwa ni mtu wa haki sana unless kama amelishwa madudu recently kwa ajili ya kumkoroga.

  So, tuache kupiga kelele, tusubiri hukumu zitolewe ndipo tuanze kuona kasoro ambazo zimejitokeza kwenye hukumu badala ya kupiga kelele wakati hatujui. Pia inategemeana na ushahidi uliopelekwa mahakamani na namna wahusika walivyojitetea.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 12. k

  kadidu Member

  #12
  May 1, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 39
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  kweli mkuu,hizi hukumu ni za kimtego hawaaminiki hata kidogo.wana lao jambo
   
 13. B

  Bubona JF-Expert Member

  #13
  May 1, 2012
  Joined: Aug 31, 2011
  Messages: 449
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Mimi siziamini kabisa mahakama zetu!! Lo lote linaweza kutokea, yaani hili la ku-balance naliona linawezekana sana! Ngoja tusubiri!
   
 14. Gsana

  Gsana JF-Expert Member

  #14
  May 1, 2012
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 4,387
  Likes Received: 348
  Trophy Points: 180
  naogopa sana kuzihusisha mahakama na ujangili wa ccm. Labda tuwahusishe majaji as individuals ila si kama mahakama. Tusianze kumtafta aliyemuua mgonjwa wakati hata mgonjwa hajafa. Wakimuondoa mnyika si tunarudia uciaguzi?na ubungo si mnajua kuwa piga ua mnyika ndo chaguo?Tulienda mambo yataenda vema.
   
 15. Pendael laizer

  Pendael laizer JF-Expert Member

  #15
  May 1, 2012
  Joined: Jan 14, 2012
  Messages: 961
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Hakuna mahakama hata moja iliyohuru hapa tz
   
 16. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #16
  May 1, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,202
  Likes Received: 1,978
  Trophy Points: 280
  Ndio tumeonewa kwasababu Yule mbunge wa magamba alitumia rushwa na imethibitishwa lakini mahakama ikamfutia ubunge tu badala na ya kumhukumu na kifungo na fimbo nyingi!!!!!!!
   
 17. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #17
  May 1, 2012
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Kuna vijana wazuri sana kwenye benchi la U-Jaji hapa nchini wenye uwezo mkubwa KUTOA HAKI isioacha chachu mdomoni.

  Umahiri wao hakika unaweza tu kudhihirika endapo tu watajiruhusu kuwa na FIKRA HURU NA KUEGEMEA WELEDI TU mbali na REMOTE YA MAGOGONI ili heshima ipate kuwafuata kama Musa Mzuna wa Singida na Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar.
   
 18. Foundation

  Foundation JF-Expert Member

  #18
  May 1, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 1,458
  Likes Received: 256
  Trophy Points: 180
  Tatizo sio mahakama kama taasisI ILA tatizo ni hakimu au jaji.Na hii inaweza kuwa kwa sababu ya incompetency au kulipa fadhila. Kama uliteuliwa kuwa jaji au hakimu wa ngazi ya juu kwa mizengwe hata hukumu zako haziwezi kuwa against ya waliokupa ujaji.
   
 19. AdvocateFi

  AdvocateFi JF-Expert Member

  #19
  May 1, 2012
  Joined: Jan 15, 2012
  Messages: 10,705
  Likes Received: 592
  Trophy Points: 280
  mkuu hapo umesema point 1 nzuri sana, kwani mahakama ilitakiwa kumvua ubunge na kumpa kifungo cha miaka ya kutosha jela kwa kosa la rushwa maana ushahidi ulikuwa wazi kabisa lakini mahakama imelifumbia macho swala hilo.
  HIVI KWELI KOSA LA LEMA NI SWA NA HILI KOSA YA YULE MLA RUSHWA WA CCM HADI WOTE WAPATE ADHABU SAWA?! Kwa hii hoja ni dhahiri kwamba mahakama hazipo huru na hii inatoa picha ya nini kitatokea hapo baadae kwenye kesi za wapambanaji wetu.
   
 20. W

  WAMURUBHERE JF-Expert Member

  #20
  May 1, 2012
  Joined: Apr 21, 2010
  Messages: 337
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  mkatae msikatae,mtukane msitukane kesho mahanga anashinda kesi,mtanambia
   
Loading...