beth
JF-Expert Member
- Aug 19, 2012
- 3,877
- 6,326
Mahakama Kuu Divisheni ya Rushwa na Uhujumu Uchumi leo Februari 18, 2022 inatarajiwa kutoa uamuzi kama Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe pamoja na Washtakiwa wengine watatu wana Kesi ya Kujibu au Hapana
Februari 15, 2022 Upande wa Mashtaka katika Kesi hiyo ya Uhujumu Uchumi yenye Mashtaka ya Ugaidi inayowakabili Wanne hao ulifunga Ushahidi baada ya Shahidi wa 13 kumaliza kutoa Ushahidi wake
Mawakili wa Jamhuri waliomba Mahakama hiyo chini ya Jaji Joachim Tiganga kuona ikiwa Washtakiwa wana Kesi ya kujibu ili hatua nyingine zifuate