Kurzweil
JF-Expert Member
- May 25, 2011
- 6,622
- 8,410
Jopo la majaji watatu wa mahakama ya rufaa nchini Kenya wameoneza siku saba zaidi kwa wapatanishi wa kutafuta suluhu kwa mgomo wa madaktari kupata dawa ya mgomo huo kwa masharti kuwa mazungumzo hayo yafanywe kwa siri.
Chama cha wanasheria nchini na tume ya kitaifa ya kutetea haki za kibinadamu zimeiambia mahakama kuwa hatua kadha zimepigwa ila yapo baadhi ya mambo ambayo hayajapata tiba itakayo sitisha mgomo ambao umedumu kea siku 81.
Kenya wameshindwa kupata suluhu kwa mgomo huo kwa siku saba baada ya mahakama ya rufaa kuwapa hukumu hilo wakati ilipowaachilia huru viongozi saba wa chama cha madaktari waliokuwa gerezani kwa kosa la kukaidi amri ya mahakama ya kusitisha mgomo.
Chanzo: ITV