Mahakama Kanda ya Dar imepanga kusikiliza Kesi ya Madai Na. 8/2018 iliyofunguliwa na chama cha ACT wazalendo

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,899
Mahakama Kuu Kanda ya Dar Es Salaam imepanga kusikiliza Kesi ya Madai Na. 8/2018 iliyofunguliwa na chama cha ACTwazalendo dhidi ya Jeshi la Polisi kutokana na kuingilia shughuli za ziara ya chama. Kesi hiyo itasikilizwa Aprili 5, 2018.

mahakama.jpg

========

Kesi za ACT Wazalendo Dhidi ya Jeshi la Polisi Kuanza Kusikilizwa Aprili 5.

Machi 18 tulizungumza na umma juu ya hali mbaya ya nchi Kiuchumi, na tukaeleza hatua ambazo kama chama tutachukua katika kutatua masuala kadhaa ya kinchi. Kwenye eneo la DEMOKRASIA tulieleza kuwa tumefungua Kesi ya Madai Na. 8/2018 Mahakama Kuu hapa Dar Es Salaam, kulishtaki Jeshi la Polisi, kutokana na Jeshi hilo kuingilia, visivyo halali shughuli za ziara yetu ya kuhamasisha maendeleo katika Kata tunazoziongoza.

Leo Mahakama imeipangia tarehe kesi husika, itasikilizwa kwa mara ya kwanza, Aprili 5, 2018 chini ya Majaji watatu, Jaji Ferdinand Wambari, Jaji Sameja na Jaji Rose Teemba.

Abdallah Khamisi
Afisa Habari, ACT Wazalendo
Machi 23, 2018
Dar Es Salaam
 
Zitto kuliburuza Jeshi la Polisi Mahakamani


Mahakama Kuu Kanda ya Dsm imepanga tarehe ya kusikiliza kesi iliyofunguliwa na Chama cha ACT Wazalendo kinachoongozwa na Mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Kabwe dhidi ya jeshi la polisi ambapo itatangazwa Aprili 5.




zitto%20kabwe%20tff_0.jpg

Taarifa iliyotolewa na Afisa Habari, ACT Wazalendo ndg Abdallah Khamisi, imesema kuwa Chama hicho kilifungua kesi ya Madai Na. 8/2018 Mahakama Kuu hapa Dar Es Salaam, kulishtaki Jeshi la Polisi, kutokana na Jeshi hilo kuingilia, visivyo halali shughuli za ziara yao ya kichama.

Mahakama imeipangia tarehe kesi husika, itasikilizwa kwa mara ya kwanza, Aprili 5, 2018 chini ya Majaji watatu, Jaji Ferdinand Wambari, Jaji Sameja na Jaji Rose Teemba.

Hivi karibuni Msafara wa ACT Wazalendo ukiongozwa na kiongozi wa chama mkoani Morogoro uliripotiwa kuzuiliwa kwa muda kufanya shughuli zao za kichama katika kata wanazoziongoza.
 
Kongole kwa kufuata sheria! Ila nilitaka kujua kama kesi za namna hii zilishawahi kufunguliwa katika tawala zilizopita!
 
Kwa maoni yangu kesi hii itqkufa kifo cha mende. Polisi watasema wanatekeleza agizo la rais la kuzuia shughuli za vyama vya siasa mpk 2020 ili watu wafanye kazi.

Kwahiyo mtuhumiwa namba moja wa ACT Wazalendo na vyama vyote vya siasa ni rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, lkn kwa bahati mbaya katiba imempa kinga ya kutoshitakiwa.
 
Back
Top Bottom