Mahakama itamleta IGP Sirro na Sabaya Mahakamani kama ilivyoombwa na Wakili Kibatala

Imekaa vizuri.

1) IGP alisema kwenye vyombo vya habari kwamba Freeman Mbowe ni Gaidi, alitaka kufanya ugaidi. Alienda mbele kumshutumu (Sio kumsadiki) na kumhukumu mtuhumiwa hata kabla ya kufikishwa mahakamani.

Hivo ni muhimu wa yeye kuletwa mahakamani ili atueleze na kutuweka sawa;

● Juu ya ufahamu wake dhidi ya Freeman Mbowe kuwa gaidi. Na atueleze kwanini alimshutumu na kumhukumu kwenye vyombo vya habari kwamba Freeman Mbowe ni gaidi kinyume na "Presumption Of Innocence (Everyone Is Pressumed To Be Innocent Until Proved Guilty Before A Court Of Law)" - Kila mtu hana hatia ya kosa lolote mpaka pale itakapothibitishwa mbele ya mahakama.

● Atuweke sawa kwanini kwa utemi, ukaidi, ujeuri, mabavu yeye kama IGP aliongelea kwenye vyombo vya habari swala hilo wakati akijua sheria haitaki swala kama hilo la kimahakama na kitafia kuongelewa mbele ya vyombo vya habari. Kwasababu, mahakama ndio ina kazi ya kumhukumu mtuhumiwa, na yeye kama IGP ana ushawishi mkubwa kwa asakari police wake wa chini hivo inaweza kupelekea swala hilo askari police tanzania nzima kumhukumu Freeman Mbowe na kusababisha haki isitendeke.

● Atueleze, yeye kama IGP kwanini aliruhusu vijana wake kuwatesa watuhumiwa kana kwamba wana hatia. Na aliruhusu vijana wake kuvunja sheria pindi wanakwenda kuwakamata watuhumiwa. Na kwanini yeye kama IGP ana ruhusu jeshi la police kuwa na askari vilaza, viazi, mbumbumbu wasiojua hata kusoma CPC wala PGA.

● Pia atuimbie ule wimbo usiokua na kiitikio wa PGA na CPC. Kama vijana wake waliotangulia kabla yake.

2) Ole Sabaaya ni jambazi lililo thibitishwa mbele ya mahakama. Anahitajika kutumika kama chambo, kwasababu yeye ndio aliasisi kukamatwa kwa watuhumiwa. Sasa inabidi atujuze aliwahi kuona wapi "MHALIFU AKAENDA KUMKAMATA MHALIFU".

NINA MENGI SANA YA KUANDIKA, ILA. . . .
 
IGP ni msimamizi mkuu wa usalama wa raia na mali zao.

Ole sabaya ni jambazi aliyehukumiwa kwa unyang'anyi wa kutumia silaha.

Sasa, nilimsikia wakili Peter Kibatala akidai hawa wawili watakuwa ni miongoni mwa mashahidi wa upande wa utetezi.

Aliyemuelewa Kibatala anifafanulie Tafadhali!
Tunamsubiri Sirro Mahakamani , hana ujanja wowote
Kuna tetesi kwamba Sirro atahojiwa na Wakili mpya atakayetambulishwa Mahakamani next week aitwaye Tundu Lissu
 
Shida sana, na ikitokea 'aijipii' nae ile pgo inampiga chenga si itakuwa aibu sana kwa nchi?
 
IGP ni msimamizi mkuu wa usalama wa raia na mali zao.

Ole sabaya ni jambazi aliyehukumiwa kwa unyang'anyi wa kutumia silaha.

Sasa, nilimsikia wakili Peter Kibatala akidai hawa wawili watakuwa ni miongoni mwa mashahidi wa upande wa utetezi.

Aliyemuelewa Kibatala anifafanulie Tafadhali!
Mqenye akili tu ndiye anaweza kumuelewa wakili mtaalamu wa sheria.
 
Ndugu Babati inaonekana unamfahamu vema Bwana JOHNTHEBAPTIST maana sio kwa kumchana huko mpaka kaingia mitini
 
IGP ni msimamizi mkuu wa usalama wa raia na mali zao.

Ole sabaya ni jambazi aliyehukumiwa kwa unyang'anyi wa kutumia silaha.

Sasa, nilimsikia wakili Peter Kibatala akidai hawa wawili watakuwa ni miongoni mwa mashahidi wa upande wa utetezi.

Aliyemuelewa Kibatala anifafanulie Tafadhali!
Sio habari za status ya MTU ni habari ya shahidi.. Shahidi anaweza kuwa hata rais
 
Sabaya wamemfunga haraka Ili asiwe shahidi.Kesi ya Mbowe ikiisha watamuachia sabaya
 
Tunamsubiri Sirro Mahakamani , hana ujanja wowote
Kuna tetesi kwamba Sirro atahojiwa na Wakili mpya atakayetambulishwa Mahakamani next week aitwaye Tundu Lissu
Acha kuexpose mambo ndg yangu, mtu risasi zote zile bado unaweka mambo hadharani, je, ikiwa kweli unataka wamtoe roho kabisa!!?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom