Mahakama itamleta IGP Sirro na Sabaya Mahakamani kama ilivyoombwa na Wakili Kibatala

Shujaa Mwendazake

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
3,735
6,292
Wakili Peter Kibatala kwa niaba ya jopo ameiomba Mahakama imlete IGP Sirro na Ole Sabaya kuja Mahakamani kutoa ushahidi katika kesi ya Freeman na wenzake Aidha.

Pia Washtakiwa watatu wamekataa maelezo yaliyosomwa Mahakamani hapo na kusema sio maelezo waliyotoa.

Je, Mahakama itaridhia na kumuita IGP kuja kuhojiwa na kina Kibatala, kuna uwezekano wa Sabaya pia kuletwa kwa maombi hayo?

Kuna mambo mengi kwenye hizi kesi mbili.

N anweka Mkeka (Mechi hii haina Sare) kuwa Aidha SABAYA au MBOWE mmoja anakula mvua ya kutosha.

Kazi na iendelee!
 
Wakili anayemuwakilisha freeman mbowe na wenzake, Peter Kibatala amesema, wanakusudia kumuita Lengai Ole Sabaya na IGP Simon Sirro kama miongoni mwa mashahidi kwa upande wao kutokana na maelezo ya Kesi kumtaja Sabaya huku wakimuacha kwenye ushahidi.

Darmpya
 
Hapa naona Sabaya akisema live kama Sirro kanituma nije hapa kusema kama Mbowe gaidi. Kwahio nimetekeleza amri ya IGP Sirro ila sijaona Mbowe kuwa mkosa.


Lunatic
 
Kuna thread ya IGP Sirro kuongea kuhusu Freeman Mbowe nliwahi kusema kwamba IGP na Ole Sabaaya wataletwa mahakamani kwa maombi ya upande wowote ule, iwe upande wa mashtaka au utetezi.

Nikasema siku hio namuonea huruma sana IGP Sirro kwa maswali atakayokutana nayo kutoka kwa Kibatala and Co. Atajuta kwanini alifanya ile press conference siku ile.

Ole Sabaaya ushahidi wake hautakuwa na mashiko kwa kuwa na historia ya kutenda makosa ya jina - Mhalifu (Criminal Record).

Yametimia sasa.
 
Hakuna awezaye kupinga wito wa Mahakama m, hakuna na hatakuwepo. Late president Ben Mkapa ashawahi kuitikia wito wa Mahakama...
huu mchezo wasipokaa vyema CHADEMA Watakimbiana MAHAKAMANI.
Ila uwepo wa KIBATALA ni hatari, jamaa ana akili kubwa sana na anapenda sana kutumia Akili yake kama silaha yake
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom