MAHAKAMA ispotutuendea haki tunaweza kushitaki wapi?

Bongolander

JF-Expert Member
Jul 10, 2007
5,038
2,000
Wakuu nina swali. Hivi sasa si wengi tunaziamini mahakama zetu, mahakama zinatenda "haki" kwa matajiri kama wakitoa chochote au wakiwa wazito, lakini ukiwa maskini hasa pale unapovutana na mzito basi ujue huna chako, hata kama haki ni yako.

Sasa kama mahakama haikutenda haki kwenye mazingira kama hayo, haki inaweza kupatikana wapi?

Kwa mfano, hivi karibuni mahakama tuyliskia mahakama imeenda kinyume kabisa na issue ya mgombea binafsi (issue ya katiba), au kwa maneno mengine imechekelea ukiukaji wa katiba. kwenye mazingira kama haya issue kama hizi zinashghulikiwa vipi?

Lakini pia kuna wakati mahakama pia haitendewi haki. Kama Mahakama haitendewi haki inaweza kudai haki yake wapi? Maswalia haya najiuliza majibu sipati, naona kama hakuna wanaojali huko juu, lakini waathirika ni sisi watu wa chini.
 
Mtazamaji

JF-Expert Member
Feb 29, 2008
5,943
0

Interesting question. wajuvi wa sheria watuelimishe.

Niliwasi kusikia yule Proffesor Mahahlu aliyekuwa balozi wa italy ndiye wakili wa Mahakamu kuu. Kama mahakama kuu ina wakili then inaonyesha inaweza kushtakiwa au kushtaki. LOL . Tuelimisheni na tupeni mwanga
 
Buchanan

JF-Expert Member
May 19, 2009
13,202

Ibara ya 107A (1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 1977 kama ilivyorekebishwa mara kwa mara, inasema kwamba chombo chenye kauli ya mwisho katika utoaji haki katika Jamhuri ya Muungano (wa Tanzania) ni Mahakama.
1. Mahakama haiwezi kukiuka katiba ila watendaji wake (majaji, mahakimu, mawakili, nk), katika utekelezaji wa majukumu yao wanaweza kukiuka katiba ambayo wameapa kuilinda na kuitetea. Ikitokea wamefanya hivyo basi wanaweza kushtakiwa kwenye chombo chenye kauli ya mwisho katika utoaji haki, Mahakama.
2. Endapo pia kuna ushahidi kwamba MZITO fulani ametoa hongo au kwa nafasi yake amependelewa na Jaji au Hakimu basi yafaa afikishwe kwenye vyombo husika kama TAKUKURU ambao baada ya uchunguzi kuthibitisha tuhuma, watapeleka suala hilo katika chombo chenye kauli ya mwisho katika utoaji haki, yaani Mahakama!
3. Endapo baada ya shauri lililokuwa mahakamani kumalizika, hukuridhika na uamuzi uliotolewa basi unatakiwa ukate rufaa ndani ya muda uliotajwa kisheria katika mahakama ya juu ya ile iliyotoa uamuzi. Fanya hivyo hadi utakapoona haki inatendeka. Hata hivyo endapo shauri limefika katika Mahakama ya Rufani na hukuridhika na uamuzi wa Mahakama hiyo basi huo ndio utakuwa mwisho wa shauri hilo.
4. Nashauri kwamba utafute ushauri wa kisheria kabla ya kuchukua hatua yoyote inayohusu shauri lako, maana mambo ya kisheria yako complicated kuliko unavyoyaona kwa haraka haraka.
5. Hakuna wakati ambao Mahakama inaweza isitendewe haki! Ni watendaji wake tu ndio wanaweza wakapokonywa haki zao na ikitokea hivyo basi waende Mahakamani kudai haki zao kama watumishi wa Serikali wengine wanavyofanya!
Thanks!
 
Thnks kwa shule lakini mbona niliwai kusikia Prfssor mahalu aliwaikuwa wakili wa mahakama kuu. ? JeriaE mahaka inaweza kushatakiwa kama sio kazi ya wakili au mwanasheria wa mahakama kuu ni nini
 
Nanren

JF-Expert Member
May 11, 2009
1,882
2,000
Wakuu nina swali. Hivi sasa si wengi tunaziamini mahakama zetu, mahakama zinatenda "haki" kwa matajiri kama wakitoa chochote au wakiwa wazito, lakini ukiwa maskini hasa pale unapovutana na mzito basi ujue huna chako, hata kama haki ni yako.

Sasa kama mahakama haikutenda haki kwenye mazingira kama hayo, haki inaweza kupatikana wapi?

Kwa mfano, hivi karibuni mahakama tuyliskia mahakama imeenda kinyume kabisa na issue ya mgombea binafsi (issue ya katiba), au kwa maneno mengine imechekelea ukiukaji wa katiba. kwenye mazingira kama haya issue kama hizi zinashghulikiwa vipi?

Lakini pia kuna wakati mahakama pia haitendewi haki. Kama Mahakama haitendewi haki inaweza kudai haki yake wapi? Maswalia haya najiuliza majibu sipati, naona kama hakuna wanaojali huko juu, lakini waathirika ni sisi watu wa chini.

Ideally, mahakama inatoa haki na haitakiwa kukosea. Inaweza kuonekana haijatenda haki kwenye macho ya watazamaji, lakini ukweli ni kuwa vielelezo na ushahidi mbalimbali ndivyo vinavyokuwa havijairidhisha mahakama kufikia uamuzi unaotaka wewe. Ikitokea kuwa mahakama haijatenda haki, basi wewe muathirika unatakiwa kukata rufaa kwa mahakama ya juu. Kifupi ni kuwa haki yako itapatikana ndani ya mfumo wa mahakama..
 
Bongolander

JF-Expert Member
Jul 10, 2007
5,038
2,000
Ideally, mahakama inatoa haki na haitakiwa kukosea. Inaweza kuonekana haijatenda haki kwenye macho ya watazamaji, lakini ukweli ni kuwa vielelezo na ushahidi mbalimbali ndivyo vinavyokuwa havijairidhisha mahakama kufikia uamuzi unaotaka wewe. Ikitokea kuwa mahakama haijatenda haki, basi wewe muathirika unatakiwa kukata rufaa kwa mahakama ya juu. Kifupi ni kuwa haki yako itapatikana ndani ya mfumo wa mahakama..

Asante kwa kunielimisha wakuu, lakini bado maswali yanabaki, mahakama isitende haki halafu kwenda mahakamani tena, hapo bado kuna swali. Hivi karibuni tulisikia mahakama ikiitupilia mbali issue ya mgombea huru, na wao ndio walikuwa watu wa mwisho kutoa haki kuhusu suala hilo lakini wakalipiga chini. Kwa hiyo pamoja na kuwa tunaona ideally mahakama ndiyo ya mwisho lakini in reality nayo kuna wakati haitendi haki.
 
Buchanan

JF-Expert Member
May 19, 2009
13,202
2,000
Thnks kwa shule lakini mbona niliwai kusikia Prfssor mahalu aliwaikuwa wakili wa mahakama kuu. ? JeriaE mahaka inaweza kushatakiwa kama sio kazi ya wakili au mwanasheria wa mahakama kuu ni nini

Kesi ya Mahalu ambayo ni Namba 1 ya mwaka 2007 ni Kesi ya Uhujumu Uchumi ambapo Prof Mahalu na mwenzake aliyekuwa Ofisa Utawala wa Ubalozi wa Tanzania nchini Italia, Grace Martin wanatuhumiwa kwa kosa la uhujumu uchumi na kuisababishia hasara serikali ya zaidi ya sh bilioni 2. Kwa hiyo unaona kwamba Prof Mahalu hakushtakiwa kama wakili wa Mahakama Kuu bali kama Balozi wa Tanzania nchini Italia! Sasa sioni hapa Mahakama Kuu inaingiaje kwenye suala hili kwamba eti imedharauliwa!
 
Buchanan

JF-Expert Member
May 19, 2009
13,202
2,000
Asante kwa kunielimisha wakuu, lakini bado maswali yanabaki, mahakama isitende haki halafu kwenda mahakamani tena, hapo bado kuna swali. Hivi karibuni tulisikia mahakama ikiitupilia mbali issue ya mgombea huru, na wao ndio walikuwa watu wa mwisho kutoa haki kuhusu suala hilo lakini wakalipiga chini. Kwa hiyo pamoja na kuwa tunaona ideally mahakama ndiyo ya mwisho lakini in reality nayo kuna wakati haitendi haki.

Hiyo idea kwamba "Mahakama haitendi haki" sijui unaitoa wapi! Nafikiri ungesema kwamba Jaji fulani hakutenda haki katika Kesi fulani! Anyway, katika kesi ya Mgombea Binafsi Mahakama ya Rufani, ambacho ni chombo cha mwisho katika utendaji haki, ilirudisha suala hilo kwenye Bunge ambalo lingeweza kuhakikisha kwamba Sheria inatungwa ili kuruhusu mgombea binafsi! Kwa hiyo ni kazi ya Wabunge wetu tuliowachagua kulisimamia hilo!
Kwa upande wako kama unadhani kwamba endapo watendaji wa Mahakama hawatendi haki (au tuseme kwa maneno yako kwamba Mahakama haitendi haki), unashauri kuwe na chombo gani cha kupeleka malalamiko zaidi ya kuchukua administrative action kupitia Bodi za Mahakama na kuwashtaki kwenye Mahakama yenyewe ambacho ndicho chombo chenye kauli ya mwisho katika utendaji haki? Maana nimekupa majibu naona kama hujaridhika na vile vile hutoi jibu lako!
 
Mtazamaji

JF-Expert Member
Feb 29, 2008
5,943
0
Kesi ya Mahalu ambayo ni Namba 1 ya mwaka 2007 ni Kesi ya Uhujumu Uchumi ambapo Prof Mahalu na mwenzake aliyekuwa Ofisa Utawala wa Ubalozi wa Tanzania nchini Italia, Grace Martin wanatuhumiwa kwa kosa la uhujumu uchumi na kuisababishia hasara serikali ya zaidi ya sh bilioni 2. Kwa hiyo unaona kwamba Prof Mahalu hakushtakiwa kama wakili wa Mahakama Kuu bali kama Balozi wa Tanzania nchini Italia! Sasa sioni hapa Mahakama Kuu inaingiaje kwenye suala hili kwamba eti imedharauliwa!

OK buch nimekupata lakini sijaunganisha Tuhuma za mahal na wadhifa aliokuwa nao wa uwakili.

May be unilimishe kwa mfano wa swali hili

  • Je mahamakama kuu ina wakili au mwanasheria?
  • Kazi ya mwanasheria au wakili wa mahakam kuu ni nini?
 
Percival

JF-Expert Member
Mar 23, 2010
2,654
2,000
Ikiwa hukuridhika na uwamuzi wa mahakama - kuna kukata rufaa. Tatizo ni kuwa wananchi wengi wa kawaida hawana uwezo wa kufuatilia kesi zao kwa muda mrefu sababu za kimaisha na kipesa. Pia vyombo vya sheria ikiwa vimefisadika hapo ndio dhuluma inapata msingi. Ninavyo fikiria vyombo vya habari vina uwezo wa kubadilisha haya mambo kwa kuyabainisha na kuyajadili - lakini itachukua muda mrefu.
 
Bongolander

JF-Expert Member
Jul 10, 2007
5,038
2,000
Hiyo idea kwamba "Mahakama haitendi haki" sijui unaitoa wapi! Nafikiri ungesema kwamba Jaji fulani hakutenda haki katika Kesi fulani! Anyway, katika kesi ya Mgombea Binafsi Mahakama ya Rufani, ambacho ni chombo cha mwisho katika utendaji haki, ilirudisha suala hilo kwenye Bunge ambalo lingeweza kuhakikisha kwamba Sheria inatungwa ili kuruhusu mgombea binafsi! Kwa hiyo ni kazi ya Wabunge wetu tuliowachagua kulisimamia hilo!
Kwa upande wako kama unadhani kwamba endapo watendaji wa Mahakama hawatendi haki (au tuseme kwa maneno yako kwamba Mahakama haitendi haki), unashauri kuwe na chombo gani cha kupeleka malalamiko zaidi ya kuchukua administrative action kupitia Bodi za Mahakama na kuwashtaki kwenye Mahakama yenyewe ambacho ndicho chombo chenye kauli ya mwisho katika utendaji haki? Maana nimekupa majibu naona kama hujaridhika na vile vile hutoi jibu lako!

Mkuu nimeweka posti hii baada ya kusoma ripoti moja ya Redet kuhusu utawala bora. Nilichoona kwenye ripoti hiyo ni kwamba kuna malalamiko dhidi ya mahakama na polisi, na sio dhidi ya mahakimu na askari Polisi. Achana na suala la mgombea binafsi, ingawa ni muhimu lakini lakini haliuhusiana sana moja kwa moja na maingiliano yaliyopo kila siku kati ya watu wa kawaida na mahakama na Polisi.

Naweza kukubaliana na wewe kuwa kuna uwezekano kuwa tatizo ni individuals ambao wana abuse nyadhofa na ofisi zao kwa kutumia uelewa mdogo tulionao wananchi na kwa kutumia mianya ya sheria na taratibu za utendaji, lakini how do you we separate them from the system they work for? How do we tell them apart from institutions they work for? Hili linakuwa gumu kiasi.

There are times when we say "the judge ruled in favour or against........" lakini pia kuna wakati tunasema "the court has ruled........" Kwa hiyo unaweza kuona kuwa viwili vinaingiliana.

Niliuliza swali ili nijue, na nashukuru kwa kunielimisha. Si kama nilikuwa na lengo la kuleta suggestion ya kuunda chombo cha nne cha kuisimia mahakama.
 
Ni kweli kwamba kuna wakati watu wanalalamikia Mahakama kwa ujumla wake, lakini ukimwendea Jaji Mkuu kulalamikia jambo atakuuliza kuwa Hakimu/Jaji gani aliyefanya tendo fulani! Mwisho wa siku itajulikana ni nani aliyefanya kosa! Hata hivyo kosa hilo la mtu mmoja au wawili linaweza ku-tarnish image ya Mhimili wote, yaani Mahakama! Hata hivyo haimaanishi kwamba Mahakama ndio iliyomtuma mtumishi wake kufanya jambo ovu! Pamoja na hayo yote hakuna sehemu nyingine yenye kauli ya mwisho zaidi ya Mahakama katika utendaji kazi!
 
Buchanan

JF-Expert Member
May 19, 2009
13,202
2,000
OK buch nimekupata lakini sijaunganisha Tuhuma za mahal na wadhifa aliokuwa nao wa uwakili.

May be unilimishe kwa mfano wa swali hili

  • Je mahamakama kuu ina wakili au mwanasheria?
  • Kazi ya mwanasheria au wakili wa mahakam kuu ni nini?

Kulingana na section 66 of the Advocates Act, Cap. 341 [R. E. 2002] inasema kama ifuatavyo: "Any person duly admitted as an advocate shall be an officer of the High Court and shall be subject to the jurisdiction thereof." Kwa hiyo Mawakili wote waliokuwa dully admitted ni maofisa wa Mahakama Kuu.
Kama Officer of the Court Wakili anatakiwa amsaidie mteja wake (to the exclusion of others, although this is not absolute) na kuisaidia Mahakama kutenda haki (administration of justice)!
 
Ngambo Ngali

JF-Expert Member
Apr 17, 2009
3,518
2,000
Interesting question. wajuvi wa sheria watuelimishe.

Niliwasi kusikia yule Proffesor Mahahlu aliyekuwa balozi wa italy ndiye wakili wa Mahakamu kuu. Kama mahakama kuu ina wakili then inaonyesha inaweza kushtakiwa au kushtaki. LOL . Tuelimisheni na tupeni mwanga

Mtu yoyote anayeruhusiwa na kuingizwa katika orodha ya mawakili Tanzania anajulikana kama "wakili wa mahakama kuu na mahakama zote za chini ispokuwa mahakama ya mwanzo".

Hii iko hivi kwa sababu kisheria wakili huyo hataruhisiwa kuingia mahakama ya rufaa tanzania mpaka awe wakili kwa kipindi cha miaka mitano. Isipokuwa anaweza kwenda mahakama ya rufaa kabla ya hapo kama atapata kibali cha jaji mkuu.

Kwa upande wa mahakama ya mwanzo sheria hairuhusu mawakili kwenda kufanya utetezi huko.
 
The Advocate who has not practiced for five years may, however, apply for a waiver in a particular matter in writing to the Chief Justice or Presiding Justice, as the case may be, showing good grounds for seeking the waiver. [See Proviso to Rule 33 (3) of the Tanzania Court of Appeal Rules, 2009, GN No. 368, Published on Nov. 6th, 2009].
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom