Mahakama ina uwezo wa kukwamisha Kasi ya Magufuli

Genghis Khans

JF-Expert Member
Dec 5, 2015
502
462
Mahakama ya Tanzania imeshindwa kubadilika na kufanya kazi kwa kasi ya Rais JPM.
  1. Imeshindwa kufungua mahakama ya Rushwa.
  2. Kesi nyingi kubwa zinachukuwa miaka kumalizika na ukumu ikitolewa ni vichekesho()
  3. Imeshindwa kufukuza mahakimu walishindwa kusikiliza kesi 250 kwa mwaka.
Inajulika kuna tatizo ya fetha lakini bado ikawa ndio sababu kuu ya kucheleshwa kutoa uwamuzi wa kesi. Nathani watanzania tunatakiwa kusema tumechoka na hizi mahakama lazima wabadilike sasa.
 
Mahakama zinatakiwa ziwe huru... na kazi ya mahakama ni kutoa haki bila kushinikizwa au kuendeshwa na matashi ya wanasiasa. Na utendaji wa mahakama ni tofauti sana na wa production line ambayo ufanisi wake unapimwa na idadi ya bidhaa zinazozalishwa.
 
Mahakama ya Tanzania imeshindwa kubadilika na kufanya kazi kwa kasi ya Rais JPM.
  1. Imeshindwa kufungua mahakama ya Rushwa.
  2. Kesi nyingi kubwa zinachukuwa miaka kumalizika na ukumu ikitolewa ni vichekesho()
  3. Imeshindwa kufukuza mahakimu walishindwa kusikiliza kesi 250 kwa mwaka.
Inajulika kuna tatizo ya fetha lakini bado ikawa ndio sababu kuu ya kucheleshwa kutoa uwamuzi wa kesi. Nathani watanzania tunatakiwa kusema tumechoka na hizi mahakama lazima wabadilike sasa.
Mahakama ya Mafisadi iko njiani... ipo jirani sanaaa. Mahakimu wana utaratibu wao wa kuwawajibisha... sheria lazima izingatiwe na haki itendeke. Vuta subira Nchi itakaa sawa na itanyooka. Uchaguzi ujao utakuwa rahisi sana kwa JPM maana watu watakubali wenyewe... HAPA KAZI TU
 
Ujumbe wa rais Magufuli kwa mahakama ni mzito sana. Uchelewashaji wa kesi nyingi unawaumiza walio wengi. Na ukiyatazama mambo kwa undani ni kama vile jaji mkuu anaambiwa kuwa halingani na matarajio ya awamu ya tano. Sio kweli kwamba rais anataka sana kesi zisikilizwe kwa haraka kiasi cha haki kutokupewa kipaumbele. Rais hataki uzembe na mambo yote yanayotokana na tabia hiyo, ambayo kwa bahati mbaya imekuwa ndio kitu kinachoutambulisha utendaji kazi wa mtanzania.

Rais anataka efficiency inayoonekana, matokeo chanya yanayoonekana. Yupo tayari kutoa bilioni 250 ili kesi zisikilizwe upesi ili mazingira yanayokwamisha kazi za mahakama yaweze kutatuliwa mapema na mchango wa sekta ya utoaji wa haki kwa taifa uweze kuonekana dhahiri.
 
Umeongea vizuri sana.

Mhe. Rais anasisitiza effectiveness and efficiency kwenye mambo yote yanayohusu kesi na mahakama kwa ujumla.

Queen Esther

Ujumbe wa rais Magufuli kwa mahakama ni mzito sana. Uchelewashaji wa kesi nyingi unawaumiza walio wengi. Na ukiyatazama mambo kwa undani ni kama vile jaji mkuu anaambiwa kuwa halingani na matarajio ya awamu ya tano. Sio kweli kwamba rais anataka sana kesi zisikilizwe kwa haraka kiasi cha haki kutokupewa kipaumbele. Rais hataki uzembe na mambo yote yanayotokana na tabia hiyo, ambayo kwa bahati mbaya imekuwa ndio kitu kinachoutambulisha utendaji kazi wa mtanzania.

Rais anataka efficiency inayoonekana, matokeo chanya yanayoonekana. Yupo tayari kutoa bilioni 250 ili kesi zisikilizwe upesi ili mazingira yanayokwamisha kazi za mahakama yaweze kutatuliwa mapema na mchango wa sekta ya utoaji wa haki kwa taifa uweze kuonekana dhahiri.
 
MAGUFULI ANA KASI YA MAJUNGU NA KUFUKUZA WAFANYAKAZI NA KUTAFUTA SIFA ZA KIJINGA KWENYE VYOMBO VYA HABARI! KWA HIYO UNATAKA MAHAKAMA NAYO IANZE MAJUNGU, KUFUKUZA WAFANYAKAZI NA KUUZA SURA KWENYE VYOMBO VYA HABARI?!
 
uwe makini na uandishi wako. usidhani uhuru wa maoni maana yahe ni kumdhihaki rais. you have bee warned.
 
MAGUFULI ANA KASI YA MAJUNGU NA KUFUKUZA WAFANYAKAZI NA KUTAFUTA SIFA ZA KIJINGA KWENYE VYOMBO VYA HABARI! KWA HIYO UNATAKA MAHAKAMA NAYO IANZE MAJUNGU, KUFUKUZA WAFANYAKAZI NA KUUZA SURA KWENYE VYOMBO VYA HABARI?!
Unaweza ukawa kweli una hasira ya maisha lakini be careful na lugha unayotumia. Unamuongelea kiongozi mkuu wa nchi haumuongelei mtu wa kawaida wa mtaani ambaye umezoea kutaniana naye kila mkikutana.
 
Kwa hali ilivyo, Mtawala wa sasa atakuwa anasumbuka mno kwenye nafsi yake namna ambavyo anaweza kuyadhibiti Mahakama ya Tanzania ili yawe na tabia za hovyo kama za Bunge la Tanzania chini ya Ndugai na jeshi la polisi chini ya Sirro ... hicho ndo kikwazo pekee kwake, si ajabu wameamua kwenda kuchoma ofisi binafsi za Mawakili za IMMMA kwa sababu ya frustration ya kushindwa kuyadhibiti mahakama. Wanafikiri wakiwatumia Gestapo wao hapa wataweza kuzima sauti zinazopazwa kutetea utawala wa sheria nchini.

Manazi wa Ujerumani walipohisi hawawezi kutawala huku kukiwa na sauti kali za ukosoaji kutoka kwa Wabunge kwa jinsi Hitler alivyokuwa akiitawala nchi hiyo, waliamua kuchoma jengo la Bunge la Reischtag mwaka 1933...baada ya hapo tunajua aliyoyatenda Hitler!

Reischtag 1.jpg
Hitler.jpg
 
Attachments

  • Hitler.jpg
    Hitler.jpg
    16.3 KB · Views: 45
Unajua, ni hatari sana kusokota kamba wakati nyuma inaungua.

Ni hatari mno kwa kweli.
 
That is very true.

Katika mihimili yote mhimili ambao Magu utakuwa bado unamuumiza kichwa itakuwa ni mhimili wa mahakama.

Kule Bungeni tayari "ameuteka" kabisa kwa kuwa Spika, Naibu Spika na wabunge wa CCM wote hao wanapokea "maagizo" toka kwa Bwana mkubwa kwa namna anavyotaka mhimili huo uendeshwe.

Ushahidi mmojawapi ni namna alivyoagiza Bunge lisionyeshwe Live na "agizo" hilo likatekelezwa!

Kwa hiyo mhimili wa Mahakama ndiyo unaomsumbua hadi sass na hasa kutokana na muundo wake kikatiba, ambapo Rais ndiye mwenye mamlaka ya kumteua Jaji wa Mahakama kuu lakini hana mamlaka ya kumfuta kazi!

Kutokana na hulka ya Mheshimiwa wetu ya kupenda kuteua na kutengua kila baada ya muda mfupi inamfanya huu mfumo wa Mahakama uwe unamtesa sana kichwa chake........

Kwa mazingira hayo inawezekana ikawa sababu mojawapo inayofanya huo mhimili kwa zaidi 8 hivi sasa mhimili huo hauna Jaji Mkuu na badala yake una Kaimu Jaji Mkuu!

Haijawahi kutokea katika awamu zote zilizopita kwa mhimili huo kukaa kipindi kirefu kama cha safari hii kwa mhimili huo kuongozwa na Kaimu Jaji Mkuu.

Kwa maana hiyo Mkulu anajisemea kimoyo moyo I wish I could be CJ..........
 
Tanganyika mnavo tawaliwa utadhani nchi yenu ni ya kimapinduzi au sababu ya hiki chama ccm ?
 
Mahakama ya Tanzania imeshindwa kubadilika na kufanya kazi kwa kasi ya Rais JPM.
  1. Imeshindwa kufungua mahakama ya Rushwa.
  2. Kesi nyingi kubwa zinachukuwa miaka kumalizika na ukumu ikitolewa ni vichekesho()
  3. Imeshindwa kufukuza mahakimu walishindwa kusikiliza kesi 250 kwa mwaka.
Inajulika kuna tatizo ya fetha lakini bado ikawa ndio sababu kuu ya kucheleshwa kutoa uwamuzi wa kesi. Nathani watanzania tunatakiwa kusema tumechoka na hizi mahakama lazima wabadilike sasa.
Rubbish!
 
Kasi ipi ua udikiteita?
 
Ujumbe wa rais Magufuli kwa mahakama ni mzito sana. Uchelewashaji wa kesi nyingi unawaumiza walio wengi. Na ukiyatazama mambo kwa undani ni kama vile jaji mkuu anaambiwa kuwa halingani na matarajio ya awamu ya tano. Sio kweli kwamba rais anataka sana kesi zisikilizwe kwa haraka kiasi cha haki kutokupewa kipaumbele. Rais hataki uzembe na mambo yote yanayotokana na tabia hiyo, ambayo kwa bahati mbaya imekuwa ndio kitu kinachoutambulisha utendaji kazi wa mtanzania.

Rais anataka efficiency inayoonekana, matokeo chanya yanayoonekana. Yupo tayari kutoa bilioni 250 ili kesi zisikilizwe upesi ili mazingira yanayokwamisha kazi za mahakama yaweze kutatuliwa mapema na mchango wa sekta ya utoaji wa haki kwa taifa uweze kuonekana dhahiri.
Siyo kweli kwamba anataka kesi zisikikizwe tu yeye anataka watuhumiwa wote wafungwe. Muwe mnamsikiliza mtu anapoongea kwa mstari

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ujumbe wa rais Magufuli kwa mahakama ni mzito sana. Uchelewashaji wa kesi nyingi unawaumiza walio wengi. Na ukiyatazama mambo kwa undani ni kama vile jaji mkuu anaambiwa kuwa halingani na matarajio ya awamu ya tano. Sio kweli kwamba rais anataka sana kesi zisikilizwe kwa haraka kiasi cha haki kutokupewa kipaumbele. Rais hataki uzembe na mambo yote yanayotokana na tabia hiyo, ambayo kwa bahati mbaya imekuwa ndio kitu kinachoutambulisha utendaji kazi wa mtanzania.

Rais anataka efficiency inayoonekana, matokeo chanya yanayoonekana. Yupo tayari kutoa bilioni 250 ili kesi zisikilizwe upesi ili mazingira yanayokwamisha kazi za mahakama yaweze kutatuliwa mapema na mchango wa sekta ya utoaji wa haki kwa taifa uweze kuonekana dhahiri.

"...Yupo tayari kutoa bilioni 250 ili kesi zisikilizwe upesi....." Hapa ndio tatizo, hii si kazi ya Bunge?
 
Back
Top Bottom