Mahakama imetoa zuio la kujadili taarifa ya CAG kuhusu Tegeta escrow Bungeni.

Saint Ivuga

JF-Expert Member
Aug 21, 2008
54,363
58,385
Source kutoka kwa Zitto
 
Attachments

  • image.jpg
    image.jpg
    54.8 KB · Views: 909
Last edited by a moderator:
mahakama nayo ipo kwa.mujibu wa sheria so sheria lazima iheshimiwe

Sheria hii iheshimiwe tafadhali.

Ibara ya 100.-(1) Kutakuwa na uhuru wa mawazo, majadiliano na utaratibu katika Bunge na uhuru huo hautavunjwa wala kuhojiwa na chombo chochote katika Jamhuri ya Muungano, au katika
Mahakama au mahali penginepo nje ya Bunge.

(2) Bila ya kuathiri Katiba hii au masharti ya sheria nyingine yoyote inayohusika, Mbunge yeyote hatashtakiwa au kufunguliwa shauri la madai mahakamani kutokana na jambo lolote alilolisema
au kulifanya ndani ya Bunge au alilolileta Bungeni kwa njia ya maombi, muswada, hoja au vinginevyo
 
Atakaye walawiti ni makinda.

Mwishoni mwa kipindi cha bunge la jioni spika amesema bunge halina taarifa yeyote ya ki mahakama iloletwa bungeni kuzuia sakata hili kujadiliwa pia wamegawiwa wote report ya cag ola nina wasiwasi kama haitakua imechakachuliwa!
 
Source kutoka kwa Zitto

1. Jambo haliwezi kuwa subjudice kama haliko mahakamani tayari. Hivyo kwenda mahakamani ili kulifanya jambo linalojadiliwa liwe subjudice ni kinyume na maana na makusudi ya convention yenyewe
2. Mahakama haina mamlaka Si kisheria wala Kwa convention au precedent kuliamrisha Bunge lisijadili jambo lolote. Hivyo kama wameandika barua hiyo ni muhimu kwa Bunge kufungua shauri la kuwa-impeach majaji waliotoa amri hiyo batili.
3. Bunge ni wawakilishi wa wananchi.. Wanananchi ndio wenye mamlaka Ya mwisho ndani Ya nchi na ndio msingi wa immunity ya Bunge. Kwamba wananchi wako huru kujadili jambo lolote, wakati wowote ikiwa ni pamoja na mahakama yenyewe. Na uhuru huo wanajipa wenyewe maana ndio wenye nchi.
4. Mfano Nchini UK kulikuwa na amri Ya mahakama(Super Injunction order) Kuwa watu Fulani maarufu wasitajwe kuhusika na mchepuko (extra marital affairs) kitendo hiki kiliwaudhi wabunge wakaamua kuwajadili na kuwataja majina bungeni hivyo zile amri zikabidi zifutwe maana zilipoteza maana.
 
Last edited by a moderator:
Bunge ni mhimili unaojitegemea sasa mahakama inatoa wapi uwezo wa kusimamisah bunge.
 
Mbona wakati wa katiba walisema mahakama haiwezi kuingilia bunge?!

Leo sijui jeuri wameitoa wapi. Fuatilia Mkuu, utaona katika wale waliosema hawawezi kuingilia bunge, wapo kwenye mgao wa escrow. Tanzania inapumulia mashine labda muujiza utokee hapa katikati.
 
1. Jambo haliwezi kuwa subjudice kama haliko mahakamani tayari. Hivyo kwenda mahakamani ili kulifanya jambo linalojadiliwa liwe subjudice ni kinyume na maana na makusudi ya convention yenyewe
2. Mahakama haina mamlaka Si kisheria wala Kwa convention au precedent kuliamrisha Bunge lisijadili jambo lolote. Hivyo kama wameandika barua hiyo ni muhimu kwa Bunge kufungua shauri la kuwa-impeach majaji waliotoa amri hiyo batili.
3. Bunge ni wawakilishi wa wananchi.. Wanananchi ndio wenye mamlaka Ya mwisho ndani Ya nchi na ndio msingi wa immunity ya Bunge. Kwamba wananchi wako huru kujadili jambo lolote, wakati wowote ikiwa ni pamoja na mahakama yenyewe. Na uhuru huo wanajipa wenyewe maana ndio wenye nchi.
4. Mfano Nchini UK kulikuwa na amri Ya mahakama(Super Injunction order) Kuwa watu Fulani maarufu wasitajwe kuhusika na mchepuko (extra marital affairs) kitendo hiki kiliwaudhi wabunge wakaamua kuwajadili na kuwataja majina bungeni hivyo zile amri zikabidi zifutwe maana zilipoteza maana.

Well said Mkuu!
 
Back
Top Bottom