Mahafali ya Chuo kikuu Dodoma; Rais Magufuli atunukiwa shahada ya Heshima ya Udaktari wa Falsafa

Mwl.RCT

JF-Expert Member
Jul 23, 2013
8,792
2,000
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli atunukiwa Shahada ya Heshima ya Udaktari wa Falsafa katika Sayansi ya Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM). Shahada hiyo imetolewa na Rais Mstaafu Benjamini Mkapa katika mahafali ya 10 ya chuo hicho.


EJ42VVgWsAAM2Rn.jpg

EJ49ZUxW4AA44pL.jpg
====

Rais Magufuli awasili UDOM

Dodoma. Rais wa Tanzania, John Magufuli amewasili kwenye ukumbi wa Chimwaga uliopo Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom) kutunukiwa shahada ya heshima ya udaktari wa falsafa.

Kiongozi mkuu huyo wa nchi anatunukiwa shahada hiyo leo Alhamisi Novemba 21, 2019 katika mahafali ya 10 ya chuo hicho. Mkuu wa chuo hicho Rais mstaafu, Benjamin Mkapa naye amehudhuria.

Wengine waliohudhuria mahafali hayo ni Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa; Spika wa Bunge, Job Ndugai mawaziri na wabunge.

Makamu Mkuu wa chuo hicho, Profesa, Faustine Bee amesema shahada hiyo inatolewa kwa Rais Magufuli kutokana na uongozi wake uliotukuka hususan katika ujenzi wa uchumi wa viwanda kwa kuwekeza katika elimu, miundombinu, mawasiliano, nishati, utalii na kuimarisha utawala bora na mapambano dhidi ya rushwa.

Amesema shahada hiyo imewahi kutolewa kwa Rais mstaafu Jakaya Kikwete mwaka 2010. Amesema waziri mkuu wa zamani, Rashid Kawawa (marehemu) naye amewahi kupewa shahada hiyo.

Wahitimu 6,488 watatunukiwa astashahada, shahada, stashahada ya juu, shahada ya umahiri na shahada ya uzamivu.

UDOM yamuomba Rais Magufuli bilioni 731

Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom) kimemuomba Rais Magufuli Sh735 bilioni kwa ajili ya ujenzi wa ndaki (College) mbili na ukarabati wa ukumbi wa Chimwaga.

Makamu Mkuu wa chuo hicho, Profesa Faustine Bee amesema hayo katika mahafali ya 10 ya chuo hicho na kuongeza kuwa ujenzi wa ndaki hizo unahitaji Sh731 bilioni akibainisha kuwa kukamilika kwake kutafanikisha lengo la kudahili wanafunzi 40,000 kwa mwaka. “Tunaomba Serikali itusaidie ujenzi wa ndaki na ukarabati wa ukumbi huu," amesema.

Rais Magufuli atunukiwa Shahada ya Heshima ya Udaktari wa Falsafa

Akimtunuku Shahada hiyo, Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma, Mh. Benjamin William Mkapa amesema: ‘’Kwa mamlaka niliyokabidhiwa, namtunukia Dkt John Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Digrii ya Doctor of Science (Honoris Causa) ya Chuo Kukuu cha Dodoma’’

Hotuba ya Rais Magufuli baada ya kutunukiwa

‘’Wakati mwingine inakuwa ngumu kutoa hotuba wakati wahitimu wenzako wakiwa hawajatunukiwa digrii zao huku wakiwa wamejiandaa na familia zao kwa ajili ya kusherehekea, na hasa ukizingatia digrii zao wamezisotea tofauti na yangu ya dezo’’

‘’Nilipopata barua kutoka kwa Mkuu wa Chuo, Mzee Mkapa, ya kuniarifu kuwa Chuo Kikuu cha Dodoma kimeamua kunipa Shahada ya Heshima ya Udaktari wa Falsafa, nilijuliza maswali mengi sana. Na maswali haya ukweli sikupata majibu yake.’’

‘’Swali la kwanza lilikuwa: Kwanini mimi, lakini, kwanini sasa? Kwasababu mimi nimekuwepo tu siku zote. Kwanini nipate Shahada ya bila kusota.’’

“Sijawahi sana kupewa vitu vya burebure ama vitu vya dezo, kwa Kiswahili cha mjini. Nakumbuka zamani hata nikenda kuomba hela ya kalamu, baba alikuwa hanipi kirahisi, alinipa kazi ya kufanya kama vile kuchunga ng’ombe ili akikupa hela na wewe uwe umeilipia”

“Wakati mwingine ujiulize unapopewa kitu cha bure kwasababu mtu hakupi tu kitu chake bure pengine anakupa bure ili na yeye akuombe kitu fulani,”

“Lakini baadae nikasema nikubali kutunikiwa kwa heshima ya Rais Mstaafu Mkapa (Mkuu wa Chuo Kikuu UDOM) na sababu ya pili niliona kuwa Shahada hii ya Heshima niliyopewa ni heshima sio tu Kwangu bali kwa wote waliowezesha mafanikio tuliyofikia kwa miaka hii minne”

‘’Ahsante wasaidizi wangu wote kwa kuniwezesha kutunukiwa hii Shahada’’

‘’Tumeshatumia bilioni 985 kwa ajili ya elimu bure’’

‘’Tumeongeza bajeti ya mikopo ya elimu ya juu. Mpaka sasa kwenye bajeti ya mwaka huu tumefikia bilioni 450’’

"Nitoe ombi kwa Vyuo Vikuu hapa Tanzania vianze kuwafundisha wanafunzi wetu kuhusu kujitegemea, na si kuwafundisha kuwa watumishi wa umma"
 
For the English Audience
The University of Dodoma (UDOM) has conferred an honorary doctorate degree to President John Magufuli during its 10th graduation ceremony.

UDOM chancellor and former President Benjamin Mkapa, conferred the degree on President Magufuli, in recognition of his exceptional leadership.

Previous recipients of the honorary degree include former President Jakaya Kikwete and the late Rashid Kawawa, who were awarded in 2010.

During his acceptance speech, President Magufuli said the honorary degree is on behalf of all Tanzanians, who in one way or another contributed towards the triumphs made by his administration in the past four years.

For the most part, many have congratulated the President. Others have pointed out that this is just the beginning.

Retired

JF-Expert Member
Jul 22, 2016
25,355
2,000
Karibu.

Ukumbi umesheheni na wahitimu na waalikwa mbalimbali wameshaketi katika nafasi zao wakisubiri kuingia kwa mgeni rasmi.

Up dates;
Graduates wake ni wa mashaka kidogo! Nimewafanyia usaili wengu tu! Sisemi kwa kuwabeza. Wajiongeze. Ukweli ni kuwa wale wa E& D.. zile D mbili.... Pricipal ndio wanakwenda UDOM hakuna wa A &B anakwenda pale! John nadanganya?
 

DiasporaUSA

JF-Expert Member
Aug 27, 2016
22,939
2,000
Kweli tumepata kiongozi, kwa hotuba ninayosikia hapa ni nondo tupu

Anagusa kotekote. Anatia vijana hamasa. Mambo ni mengi tumfatilie kupitia luninga
CCM Inavofanya Maisha haya kuwa Magumu Kuna kipindi mtu unakosa hela mpaka unajihisi labda Ulisomea BACHELOR OF POVERTY AND APPLIED SUFFERING.

Basi haya maisha acha tu na Ukijinyonga Police wanakuja kushuhudia na ku-confim..
 

mwayena

JF-Expert Member
Apr 21, 2016
2,892
2,000
Hakuna kipya, reli km kadhaa, watalii wameongezeka, tumejenga madaraja, uchumi unapaa kwa "7%".....hivi hua anarudia hotuba hiyo hiyo miaka yote?
 

Abou Saydou

JF-Expert Member
Dec 1, 2014
2,737
2,000
Graduates wake ni wa mashaka kidogo! Nimewafanyia usaili wengu tu! Sisemi kwa kuwabeza. Wajiongeze. Ukweli ni kuwa wale wa E& D.. zile D mbili.... Pricipal ndio wanakwenda UDOM hakuna wa A &B anakwenda pale! John nadanganya?

Una matatizo yako binafsi

Udom kama mbovu basi Udsm ndio imesababisha Udom iwe na graduates wabovu kwanini nasema hivi. Sababu ni moja tu walimu waliopo udom % kubwa wamepitia UDSM kitaaluma kama sio degree ya kwanza basi degree ya pili nakuendelea wamezichukulia Udsm, hivyo basi Udsn iliandaa watu wa hovyo hovyo ambao Leo hii wanafundisha vyuo mbali mbali Tanzania na kuzalisha bidhaa za hovyo hovyo.

N.B mtu anaweza kuwa na D&D au E&D kichwani akawa yupo makini kuliko mwenye A&A.
 

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
39,335
2,000
“Wakati naipokea shahada hii ya heshima, kwa heshima, furaha na unyenyekevu mkubwa, natambua kuwa si yangu binafsi bali ni ya watanzania wote”-Rais @MagufuliJP

Nitashangaa kuanzia leo nikiona au kusikia kuna Watu wanahangaika kwenda Vyuoni ili wakasome Shahada ya Uzamivu ( Doctorate / PhD ) wakati tayati yupo Mtanzania Mmoja ambaye anatupenda kuliko Maelezo na ameweza Kuipata hiyo Shahada kwa niaba ya Watanzania wote.

Kwa maana hiyo basi Kuanzia leo kila Mtu nchini Tanzania ukianza Kumtaja jina lake yakupasa Kwanza uanze na neno Dakta. Kwa mfano Kuanzia leo hii nami Jina langu linabadilka na sasa nitakuwa naitwa Dkt GENTAMYCINE kwani hata Mimi kama Mtanzania nimepata PhD kutoka kwa aliyetusaidia Kuisomea na Kutunukiwa leo Mheshimiwa Rais JPM.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom